Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,035
- 6,907
Poleni na harakati za kupambana na Uvico 19.
Turudi kwenye mada,kumekuwa na sintofahamu na kusita Kuhusu suala la kutolewa bure kwa huduma za matibabu nchini kwa kila mtanzania kuwa na bima ya Afya.
Ishu kubwa imekuwa ni gharama.Sasa serikali ingeanzisha utaratibu wa kuchangia gharama kwa makundi ya umri kwa kuweka kiwango cha sh.120,000 kwa mwaka kwa kila kaya kwa watu wazima wenye umri Kati ya miaka 25-65.
Watoto kuanzia mwaka 0-18 iwe ni sh.50,000 kwa mwaka na vijana wenye umri kuanzia miaka 19-24 iwe ni sh.80,000.
Kwa upande wa wazee zaidi ya miaka 65 iwe ni bure bila kuchangia chochote.Utaratibu huu utakuwa nafuu kuliko viwango vya sasa vya Bima ya Afya ya hiari.Kuchangia kutungiwe sheria na iwe ni LAZIMA ambako kila mtu atawajibika kulipa kwa mujibu wa sheria.
Uchangiaji huu ni affordable kwa kila rika na vipato endapo tuu utawekewa utaratibu mzuri wa kulipa kwa awamu au kwa mkupuo mmja.Hili likifanyika litamuwezesha kila mtu kuwa na Bima ya Afya na uhakika wa matibabu.
Kwa kuongezekae tuu serikali itakuwa na uhakika wa mapato ya kuendeshea sekta ya Afya.Kwa idadi ya wa watanzania zaidi ya mil.60 hapo unazungumzia wastani wa sh.320,000 kwa mtu mzima mwenye familia ya mtoto 1.Hii ni nafuu kuliko Bima ya hiari ya zaidi ya 480,000 kwa kichwa inayotolewa na NHIF.
Kama itafaa wafikilie kutunga sheria ya hivyo,watakaosema pesa ni kubwa hawatakosekana lakini this is cheapest way of funding universal health insurance.Watu tunalipa kodi za nyumba Kati ya 10,000-500,000 kwa mwezi ni dhahiri hiyo pesa ni ndogo Sana mtu kushindwa kulipa endapo itawekewa mkazo wa kisheria.
Karibuni kwa maboresho zaidi.