NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 8,454
- 17,263
Kila mwaka wanavyuo wengi wana graduate na kurundikana mtaani bila ajira huku wakihangaika kutafuta ajira bila mafanikio. Serikali kama mdau wa ajira nchini inapaswa kuja na wazo la ajira za mkataba kama ifuatavyo;-
1.Kwenye utumishi wa umma:
Mfumo wa ajira za maisha uondolewe yaani nesi, daktari, mwalimu n.k badala ya ajira zao kuwa za maisha ziwe za mkataba wa miaka mitano hadi kumi tena wakilipwa mishahara minono ili mkataba unapoisha mtumishi akajiajiri ili kuendeleza maisha yake! Hii itasaidia serikali kuajiri watumishi wapya wanaotafuta ajira kila siku na kupunguza uhaba wa ajira nchini!
2.Kwenye siasa:
Serikali itunge sheria itakayosimamia vyama vya siasa kutorudia kuteua majina yale yale kwenye uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani kila baada ya miaka mitano. Kuwe na ukomo wa utumishi wa kisiasa kwa miaka mitano mitano ili kuwapa nafasi wengine wenye sifa na vigezo vya kielimu vikichukuliwa kama sifa kuu mojawapo ya uteuzi. Angalau Shahada ya kwanza kwa ubunge na Astashahada kwa udiwani. Hii itatoa fursa kwa wengi kupitishwa na vyama vya siasa kwenye uchaguzi na kusaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.
Nawakaribisha kwa mjadala huru na mwenye mawazo mbadala aongezee.