Ushauri kwa Serikali: Ajira za mkataba ndiyo suluhisho pekee la uhaba wa ajira nchini

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
42,910
2,000
kwa hio kila baada ya miaka mitano serikal ianze tena kuwafubdisha maana walr wenye uzoefu watakua wamesitishiwa mkataba.idea yako is pointress
Training inachukuaga miaka mitano kwani? Probation si huwa miezi mitatu mpaka 6!

Mbona mnaongea kama vile majuha?
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
42,910
2,000
Yaani baada ya kila miaka 5 watu wapya kazini
Huko kazini kutakua mchaka mchaka watu ni kuwaza kufanikisha mambo yao tu ubunifu utakua hakuna
Kwani hio miaka 60 kuna ambaye hawazii mambo yake binafsi? Wengi si wapigaji tu tena ubaya wa hii miaka 60 mtu akishapata mkataba wa Utumishi tu ana relax maana anajua follow ups huwa sio rahisi na kufukuzwa ni ngumu serikalini hata akivurunda! Ndio maana mtu yupo radhi aache mshahara wa million private company akimbilie laki 8 ya serikalini😅
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
42,910
2,000
MNHHHHH ugumu wa kijana aliyemaliza chuo kufanya biashara ni upi? Na urahisi wa mtu aliyekua ofisini kufanya biashara ikasimama ni upi?? Toa evidence tukuelewe maanake ni kama unasema watanzania wote tuingie kwenye ujasiriamali jambo ambalo ni ngumu haliko practical,,,,
We unaonekana unamenya serikalini wewe ndio maana hutamani ajira yako ikatishwe kwa mkataba! Mi nina hakika 80% ya waajiriwa ikatokea waambiwe ajira basi imetosha mpishe wengine basi kuna wengi tutawazika kwa presha.

Ugumu wakujiajiri uko pale pale ila utofauti utakuwa kwamba mwenye mtaji mkubwa ana chance kubwa yakutoboa mfano wewe umemeki 70M! Ukianza biashara ya 2M ikaanguka, ukarudia tena ikaanguka mpaka itakapokubali kuwork out you stand a chance by far!

Imagine graduate kafanya the same kwa 2M tu biashara imemkataa! Hela imepoteaa anarudishaje tumaini?
 
May 13, 2021
91
125
Kila mwaka wanavyuo wengi wana graduate na kurundikana mtaani bila ajira huku wakihangaika kutafuta ajira bila mafanikio. Serikali kama mdau wa ajira nchini inapaswa kuja na wazo la ajira za mkataba kama ifuatavyo;-

1.Kwenye utumishi wa umma:
Mfumo wa ajira za maisha uondolewe yaani nesi, daktari, mwalimu n.k badala ya ajira zao kuwa za maisha ziwe za mkataba wa miaka mitano hadi kumi tena wakilipwa mishahara minono ili mkataba unapoisha mtumishi akajiajiri ili kuendeleza maisha yake! Hii itasaidia serikali kuajiri watumishi wapya wanaotafuta ajira kila siku na kupunguza uhaba wa ajira nchini!

2.Kwenye siasa:
Serikali itunge sheria itakayosimamia vyama vya siasa kutorudia kuteua majina yale yale kwenye uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani kila baada ya miaka mitano. Kuwe na ukomo wa utumishi wa kisiasa kwa miaka mitano mitano ili kuwapa nafasi wengine wenye sifa na vigezo vya kielimu vikichukuliwa kama sifa kuu mojawapo ya uteuzi. Angalau Shahada ya kwanza kwa ubunge na Astashahada kwa udiwani. Hii itatoa fursa kwa wengi kupitishwa na vyama vya siasa kwenye uchaguzi na kusaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Nawakaribisha kwa mjadala huru na
Ohooo, izo stress za ajira kaka
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,554
2,000
Atleast ataachwa na kitu mkononi! Knowing thats your last bullet in hand itampa ujasiri wa kujaribu mishe kadhaa maana mtaji anao.

Kuisha kwa mkataba ukiwa na 70M mkononi inaweza kuwa sawa na kukabidhiwa cheti cha degree bila sent 5 kisha uambiwe jiajiri?
Mnhhh, hio million 70 inatoka wapi?? Au ume assume kila kitu nitakua constant? Hakuna ada za watoto,usafiri, chakula etc Anyway siku ambayo Tanzania inaweza kumpa kila mtu million 70 ndio siku ambayo Tanzania hakuna matatizo yoyote ikiwemo ukosefu wa Ajira!,

Pia sio wote wana utaalamu wa kujiajiri, mfano ni wastaafu, ni wangapi baada ya kupewa pensheni wameweza kuishi bila kutegemea ndugu? How long pension zao zili last au kufungua biashara??, kwa hio unaona ishu sio kupata mtaji,Ishu ni kujua kujiajiri na sio wote wana ujuzi huu,,,mnacho suggest ni kama WOTE tujiari jambo ambalo haliwezekani, ,

Kuhusu cheti bila senti 5 hili ndio tungepaswa kudiscuss na kubuni njia za kusaidia , sio kunyang'anya kazi wengine huwezi kutoa depression kwa huyu halafu umpe mwingine, no, haliko sawa, badala ya kupandisha mishahara mpaka million 70 kwa nini fungu hili hili lisitengwe kiasi kusaidia graduates wapya kujiajiri? Huoni this is more feasible than causing chaos/depression/job insecurity????
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
13,554
2,000
We unaonekana unamenya serikalini wewe ndio maana hutamani ajira yako ikatishwe kwa mkataba! Mi nina hakika 80% ya waajiriwa ikatokea waambiwe ajira basi imetosha mpishe wengine basi kuna wengi tutawazika kwa presha.

Ugumu wakujiajiri uko pale pale ila utofauti utakuwa kwamba mwenye mtaji mkubwa ana chance kubwa yakutoboa mfano wewe umemeki 70M! Ukianza biashara ya 2M ikaanguka, ukarudia tena ikaanguka mpaka itakapokubali kuwork out you stand a chance by far!

Imagine graduate kafanya the same kwa 2M tu biashara imemkataa! Hela imepoteaa anarudishaje tumaini?
Mimi siko kazini serikalini nfact ni jobless ila unaonekana unajua upotevu wa ajira unaweza kufanya mtu akaweza kupoteza maisha! Ndicho tunazungumza humu!

Biashara kumkataa graduate ndicho tunachosema humu sio kila mtu ataweza kujiajiri, una million 2 au 7 it doesn't matter, Kuna walioanza na million 2 wakafanya makubwa tu
 
raraa reree

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
888
1,000
Kwani hio miaka 60 kuna ambaye hawazii mambo yake binafsi? Wengi si wapigaji tu tena ubaya wa hii miaka 60 mtu akishapata mkataba wa Utumishi tu ana relax maana anajua follow ups huwa sio rahisi na kufukuzwa ni ngumu serikalini hata akivurunda! Ndio maana mtu yupo radhi aache mshahara wa million private company akimbilie laki 8 ya serikalini😅
Atawazia mambo yake ndio
Ila kazini yupo mda mrefu na yeye ana moyo kwa hiyo vitu vya uongo na kweli atafanya 😃😃😃
Si unaona hata viongozi wetu wanapiga lakin panadol angalau hazikosi hosp kutupoza maumiv ya kichwa
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,716
2,000
Kila mwaka wanavyuo wengi wana graduate na kurundikana mtaani bila ajira huku wakihangaika kutafuta ajira bila mafanikio. Serikali kama mdau wa ajira nchini inapaswa kuja na wazo la ajira za mkataba kama ifuatavyo;-

1.Kwenye utumishi wa umma:
Mfumo wa ajira za maisha uondolewe yaani nesi, daktari, mwalimu n.k badala ya ajira zao kuwa za maisha ziwe za mkataba wa miaka mitano hadi kumi tena wakilipwa mishahara minono ili mkataba unapoisha mtumishi akajiajiri ili kuendeleza maisha yake! Hii itasaidia serikali kuajiri watumishi wapya wanaotafuta ajira kila siku na kupunguza uhaba wa ajira nchini!

2.Kwenye siasa:
Serikali itunge sheria itakayosimamia vyama vya siasa kutorudia kuteua majina yale yale kwenye uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani kila baada ya miaka mitano. Kuwe na ukomo wa utumishi wa kisiasa kwa miaka mitano mitano ili kuwapa nafasi wengine wenye sifa na vigezo vya kielimu vikichukuliwa kama sifa kuu mojawapo ya uteuzi. Angalau Shahada ya kwanza kwa ubunge na Astashahada kwa udiwani. Hii itatoa fursa kwa wengi kupitishwa na vyama vya siasa kwenye uchaguzi na kusaidia kupunguza tatizo la ajira nchini.

Nawakaribisha kwa mjadala huru na mwenye mawazo mbadala aongezee.
Mkuu hivi unadhani kwa nini serikali haiajiri ?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom