Ushauri kwa Sekretarieti ya Ajira Serikalini (PSRS)

Binafsi sijawahi kupata ujumbe wowote ninapo apply wala nipokua shortlisted.
 
Habari za muda huu wana jukwaa, leo ningependa kutoa ya moyoni kuhusu majanga yaliyonikuta katika mchakato wa kuomba kazi Serikalini. Huenda sio mimi tu bali wengi wetu yametutokea au yanatukwaza kwa namna moja au nyingine.

Nitazungumzia mambo matatu ambayo kwa maoni yangu yanapaswa kuangaliwa na chombo hiki muhimu cha ajira za Serikali. Lengo la kuandika bandiko langu hili ni kuangazia changamoto zilizopo na namna ya kutatua.

Moja, unapofanya maombi ya kazi kwenye mfumo wa ajira portal hakuna ujumbe wowote unaoupata kwenye barua pepe wala simu. Namna hii inaweza kubasabisha mtu akapishana na tarehe za usahili kwani hupigiwi simu wala kutumiwa ujumbe wowote kama wanavyofanya makampuni binafsi.

Maana yake unatakiwa kila mara uchungulie kwenye mfumo wa maombi, kwa karne hii ya teknolojia ya habari na mawasiliano ni kwanini basi Sekretarieti isifanye jambo hili kuwa jepesi kwa kuwatumia wahusika ujumbe aidha kwa simu au barua pepe? Hili bila shaka linawezekana na lipo ndani ya uwezo wenu, naomba mlifanyiekazi.

Pili, kuna ulazima gani mtu atoke mkoani aende hadi Dar es Salaam au Dodoma kufanya mtihani wa makaratasi? Kampuni nyingi kubwa na ndogo duniani zinafanya usaili wa awali kupitia mtandao.

Kama ni maswali yanawekwa kwenye mfumo wa usaili na mtu anafanya maswali hayo akiwa popote duniani na hata usaili wa ana kwa ana siku hizi unafanyika kwa mtandao. Hii inasaidia kuwapa fursa watu wengi zaidi na pia inawapa nafasi watu wengine waliotamani kushiriki ila wana dharura mbalimbali.

Tatu, kuna sehemu kwenye mfumo wa ajira unachagua aina ya notification na aina za jira unazotaka ili ikitokea utumiwe ujumbe lakini sidhani kama zinafanyakazi. Nadhani mna kazi kubwa ya kufanya ili kuuboresha mfumo huu, naamini inawezekana na italeta tija.

Wasalaam.
Uko sahihi na hoja yako inafanyiwa kazi. Mfumo wa online APTITUDE test system utaanza kujengwa na hivyo kuwafanya waombaji kazi kufanya usaili huko waliko.
 
Du!!! Basi tatizo lako kubwa sana maana hata namba za usaili unapata kwenye account( email) yako sasa hao woote wanaoitwa mbona wanakuja na namba zao.Na hata usipokuwa shortlisted unaelezwa sababu kwenye akaunti yako.
Hapo tatizo ni wewe kabisa labda ulisaidiwa kufungua hiyo akaunti na huisimamii wewe kwahiyo huijui ina features zipi nini na nini.Jipange upya

Back
Top Bottom