Ushauri kwa Rais Samia; Azingatie bodi mbili tofauti kuendesha TPA na napendekeza "two tier board of directors"

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,395
Kwako Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwanza pole na majukumu makubwa ya kuongoza taifa hili, au nchi hii na bila shaka umethibitisha kwamba nchi hii ni ngumu.

Moja ya mambo mazito yanoisumbua nchi hii ni uwajibikaji na baadhi ya wananchi kupenda kupata bila jasho au kupiga kama ambavyo mtangulizi wako alitanabaisha.

Kama tulivyosikia bodi ya TPA umeivunja na yasubiriwa bodi mpya kuendesha taasisi hiyo au chombo cha kutuletea mapato nchi yetu kutuneemesha kama nchi na pia kuendelea kuzinufaisha nchi jirani ambazo zote twaweza sema kwa kiingereza hazina bandari yaani ni "landlocked".

Umeivunja si kama vile wavunja jungu bali umeivunja ili kuunda bodi mpya ambayo itakuwa tofauti na itakuletea matokeo chanya tofauti na bodi ilokuwepo ambayo imeshindwa kutekeleza majukumu yake na kushindwa kudhibiti shughuli za bandari na kuendeleza ufisadi na taarifa zote utakuwa nazo kapuni.

Bandari za nchi yetu zina umuhimu wa kihistoria, kibiashara na kimiundombinu.

Bandari ni sehemu ya mihimili ya kiuchumi au backbone kwa nchi yetu, nchi jirani na bandari zingine zinazoitegemea kama Mtwara na Tanga.

Bandari zikiendeshwa kiufanisi basi, nchi yaneemeka kiuchumi na pia kujisifia kwa kuwa na chombo hicho yaani "prosperity" kwa kizazi na kizazi.

Hata siku raisi Samia ukiondoka madarakani hutajutia maamuzi sahihi ya kuhakikisha bandari zetu zasimamiwa ipasavyo kutukumboa kiuchumi.

Nina imani utaiunda bodi sahihi yenye kuwajibika na kutekeleza mipango ya serikali na sera zake za kiuchumi likiwemo suala la mapato.

Sasa basi mheshimiwa Rais, ukiwa waunda bodi mpya ya TPA napendekeza aina tatu za bodi ambazo waweza kuzifikiria ili upate bodi imara ambayo itahakikisha shughuli za bandari haziingiliwi na wapigaji, na nchi yapata mapato sahihi.

1. Bodi ya wawakilishi.

Hii bodi yaundwa na watu ambao wanaelewa namna ya kuendesha shughuli za bandari yaani port operations. Hivyo ni muhimu kuangalia vijana na wazee wenye ueledi katika uendeshaji wa bandari hiyo na hata wale wa kutoka bandari zingine na waunde bodi ya pamoja.

Hapa watafuta mfano wa bandari bora kabisa na kisha utachukua "template" na kuitumia kuunda bandari zingine kama Tanga na Mtwara.

2. Bodi ya wataalam.

Hii hata mimi naipenda kwa sababu itaunda wataalam wa nyanja mbalimbali kutoka maeneo mengine kama jeshini, usalama, tehama, HR screening & vetting, TRA na "general security" ya bandari.

Nadhani bado mizigo yatoroshwa kule Shimo la Udongo kwenye ile njia maalum hivyo hii bodi ya wataalam itaunda mkakati wa kuhakikisha bandari ipo salama kimapato, kiuendeshaji na kiufanisi.

3. Bodi Mchanganyiko yaani two Tier Boards.

Huu ni mseto wa bodi namba 1 na 2 na bodi moja itasimamia uendeshaji wa shughuli za bandari za kila siku na bodi ingine itasimamia upangaji sera, kubuni mipango mipya na kuboresha iliyopo kama vile namna ya kukabiliana na wapigaji madili.

Tukumbuke uthibiti na uendeshaji bandari waendana na udhibiti matumizi ya fedha kwa uongozi yaani "overall cost leadership", kutumia mfumo sahihi ambao wahakikisha mapato yanapatikana (kupitia user payment system) ambapo utapelekea kuongoza idadi ya meli nyingi za kigeni ambazo zitaingiza ... Mapato ya kutosha.

Shughuli zingine ni kudhibiti gharama za uendeshaji na zile gharama za tozo kwa meli za kigeni zikaapo kwenye gati.

Mheshimiwa Rais, hayo yote yataleta faida kimapato kwa nchi yetu kama wamiliki na kisha kwa mji wa Dar-es-salaam ambao bado wahitaji miundombinu imara, mikoa jirani na taifa kwa ujumla.

Mwisho, ni kwamba bandari yetu itakuwa ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na wahitimu ambao badala ya kuanza kujishughulisha na umachinga basi angalau wanakuwa baadhi yao wanapata ajira ama za muda au za kudumu kujifunza shughuli mbalimbali za bandarini.

Mheshimiwa Rais nakutakia kila la kheri katika umakini wako wa kuunda bodi mpya ya TPA.
 
Mimi napendekeza kuwe na 'imaginary board'. Hii iundwe ndani ya wafanyakazi wa TPA, kuanzia wa ngazi za juu hadi wa chini (floor employees). Nasikia kuwa TISS huwa wapo kila sector (ina maana hata TPA wapo), na inasadikiwa kuwa kutokana na viapo walivyokula, kamwe hawawezi kuisaliti nchi, nadhani hawa nao wangekuwa ndani ya hii 'imaginary board'. Itakuwa haina maana kumuweka mtu kwenye board ambaye hayuko 'committed', kila siku tutalalamika.
 
Back
Top Bottom