Ushauri kwa Rais wangu mpendwa: Chunguza na kushughulikia tatizo moja dogo - ufa wa ukabila na ukanda

MANILABHONA

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
458
500
Nakusalimia kwa salamu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Hongera sana kwa kazi mama yetu, Mama Samia Suluhu Hassan. Watanzania sasa tumekuelewa vizuri na tuko pamoja na wewe. Mabadiliko uliyoyafanya ndani ya muda mfupi yanaonesha kweli ulikuwa karibu na mtangulizi wako na ulielewa alichokuwa anakifanya. Tumejulishwa wizi wa Tanzanite, Hasara za ndege kwa miaka mitano iliyopita, Ukandamizaji katika kodi hadi wafanyabiashara kufunga biashara zao na kukimbia kuwekeza nchi nyingine. Hakika kwa mwendo wako huu tutafika mbali.

Naiona Tanzania ileeeeee ya watanzania wenye upendo, amani, ushirikiano, Tanzania inayoendelea kupambana na ujinga maradhi na umaskini-maadui wetu wa kihistoria. Tanzania ya ujamaa na kujitegemea. Pengine kizazi cha watoto wetu kitapona, kizazi cha kubet na kubahatisha maisha.

Pamoja na mafanikio haya mama, nashauri uchunguze na kushughulikia tatizo moja dogo-UFA WA UKABILA NA UKANDA. Bila kulishughulikia hili, mbeleni nchi itakulilia, wajukuu zetu watakapoanza kugombana-kisa ukabila. Katika wosia wa hayati Mwalimu J.K.Nyerere, Baba wa taifa alituasa sana kuhusu ufa huu. Hata mzee Abeid Amani Karume alituasa pia. Kwa bahati mbaya sana, tena sana sana Ufa huu ulikuwa mkubwa sana na kujidhihirisha waziwazi wakati wa serikali ya awamu ya tano.

Bila hata aibu ungeweza kukuta mfano wizara fulani waziri ni Gwajima (msukuma), Katibu mkuu Mabula (msukuma), Mganga mkuu wa serikali Makubi (msukuma), wakurugenzi karibu wote wasukuma (Magembe, Maduhu, Mbanga, n.k), manaibu wao vivo hivyo. Nenda kwenye mashirika na taasisi za serikali uzi ulikua huohuo, lazima utasikia, Luhemeja, Shija, Kichele, Mchele,Busungu, Msungu, Mayala, Maduhu, Masele, Kadogosi, Masanja, Maganga, Mabeyo, Maduki na majina mangine mengi ya namna hiyo.

Nenda kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi n.k vivo hivyo. Kuna wakati nilimwangalia mtangulizi wako nikakumbuka maneno ya baba wa taifa: " Tuchague kiongozi ambaye ukimsikiliza anachoongea jukwaani uone kweli anachosema kinatoka rohoni/moyoni". Mtangulizi wako kwenye ufa huu maneno yake yalikuwa hayatoki moyoni bali mdomoni, alikuwa hafanyi asemalo.

Nchi haiwezi kwenda kwa utaratibu huu, lazima tutafika sehemu tutakwama. Najua unajua kuwa hata viongozi wenzako kwenye mihimili mingine hawakuridhika na hali hii, walikaa kimya ili kulinda "collective responsibility and leadership" lakini wangepata nafasi wangekwambia hayo hayakuwa sahihi.

Nakushauri haya kwa sababu naipenda nchi yangu na ni mzalendo wa kweli

Mwenyezi aziweke roho za marehemu mahali panapowastahili
 

mandawa

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
284
250
Wacha tuamini Mama kasikia...na kwamba atafanyia kazi. Na kuongeza tu mama..ukabila huo ndio ulitufanya wafanyakazi tuonekane tumenyooshwa..na kwamba tunajituma..kumbe si kweli hata kidogo...tuliogopa kusemewa na kutumbuliwa. Wenzetu hawa walionekana kama manyampara..ni amri tu..wala haangalii mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa umma...basi nasi tukaenda hivo hivo...kimsingi hakuna mabadiliko ndani yetu...ni unyonge tu tuliouvaa ili tuonekane watiifu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom