Ushauri kwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mh. Hussein Ali Mwinyi

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,988
22,379
Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mimi kama kijana wako imenipitia tafakuri ambayo nimeona nikushauri kwayo. Inawezekana mada hii ikazuwa mjadala ambao ukawa na matokeo hasi kwako kama mtu au kwa taasisi ya Urais, hiyo siyo nia yangu mkuu na kwa kuwa wewe ni mtu muelewa sana basi najua in shaa Allah utaielewa dhamira yangu.

Mheshimiwa Rais binafsi naamini wewe ni mtoto kipenzi wa Mzee Rukhsa, yeye hajanukuliwa akisema hilo lakini yapo matukio kadhaa ambayo yaliashiria hilo. Pengine wewe na ndugu zako mnajua kwanini ni hivyo lakini sisi wa nje tunapata hisia hizo. Hongera kwa hilo na Mungu aibakishe hali hiyo. Mzee Mwinyi nina uhakika amepata mengi ambayo aliyatamani katika maisha yake ya dunia, lakini pia nahisi yapo mengi ambayo bado anayatamani. Mzee Mwinyi ni mcha Mungu na naamini anakaa na anafikiria Maisha yake baada ya kifo chake (Mungu amjaalie Maisha mema baada ya maisha haya ya dunia). Mheshimiwa, Mwenyezi Mungu anatuambia kila nafsi itaonja Mauti na tunaamini kikamilifu katika hilo.

Ushauri wangu kwako kupitia bandiko hili ni juu ya mambo mawili ambayo ikitokea Mzee Mwinyi ametangulia mbele ya haki basi ntafurahi na kujiskia raha mimi kama Mwananchi wako kukuona ukiyafanya.

(i) Wewe na ndugu zako (watoto wa Mzee Mwinyi) ndio mshiriki kikamilifu katika kuuosha na kuu-kafini mwili wa Mzee wetu. Mtume Muhammad (S.a.w) ameelekeza kwamba maiti ya Kiislam lazima ioshwe na ikafiniwe, na akaelekeza kuwa maiti zetu zioshwe na zikafiniwe na watu wao wa karibu ili kama kuna aibu yoyote kwa maiti huyo iweze kustiriwa na watu wake hao wa karibu. Najua kunaweza kukawa na changamoto kutoka kwa watu wa Usalama (TISS) lakini Mheshimiwa Rais mwisho ya siku sisi ni binaadam na tunayo majukumu zaidi ya haya ya kitaifa ambayo inatupaswa tuyatekeleze.

(ii) Wewe kama mtoto wake kipenzi uhusike kumlaza kwenye mwanandani (yaani uingie kaburini/ uwe miongoni mwa wale watu watano watakaoingia kaburini kumlaza Mzee Rukhsa). Katika mlango huo huo wa yanayompasa kufanyiwa maiti ya kiislam moja wapo ni kumzika, na katika kumzika sisi tunamfukia na mchanga awe rais awe kapuku. Najua pia zitakuwepo changamoto za kiusalama juu ya wewe kuingia kaburini lakini nakusihi uwaeleze hao watu wa system kwamba wewe umeamua hivyo. Uende ukampumzishe wako na hilo litakupa faraja na thawabu za hali ya juu kwa kufuata maelekezo ya Mtume wetu. Aibu yoyoyte ya marehemu wa kiislam inatakiwa istiriwe na watu wake wa karibu.

Angalizo: Bandiko hili si la kufanya Uchuro na sijaliandika kwa nia ovu, natambua kwamba unaweza kutangulia wewe na ukamuacha Mzee Rukhsa anadunda lakini matarajio ya kibinaadam ni kwamba Mzazi huwa anatangulia na kumuacha mtoto wake duniani.

Namuombea Mzee Rukhsa umri mrefu ili apate kuendelea kumtumikia mola wake na sisi huku tuendelee kuvuna busara zake.
 
Mbona ushauri mwingine nizaidi yavituko kimaadili.

Juzi hukuona mtoto aliyesoma hotuba take kwa niaba.

Kipenzi! Wewe nichonganishi hujui mzee ruksa ana watoto wengi.

Nakama yeye kipenzi niwajukuu utasemaje.

Huo ni udhaifu wako wafkra
 
Mbona ushauri mwingine nizaidi yavituko kimaadili.

Juzi hukuona mtoto aliyesoma hotuba take kwa niaba.

Kipenzi! Wewe nichonganishi hujui mzee ruksa ana watoto wengi.

Nakama yeye kipenzi niwajukuu utasemaje.

Huo ni udhaifu wako wafkra
Ok
 
Mshaanza imani kali, take easy and don't take things always too serious. Atakayekuzika humjui.
 
Mzee Mwinyi ni National Icon siyo mtu wa kuleta mambo ya dini sijui familia au anampenda mwanae flani, hapo ni full protocol, tunamuaga uwanjani na mizinga juu.
 
Back
Top Bottom