Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kwako Rais Samia. Suala la mgongano kati ya Hamza na Polisi sio jipya kutokea nchini, labda tofauti kubwa ni kwamba Hamza alichukua hatua ya kulipiza kisasi kwa kuwaua askari.
Kila siku malalamiko dhidi ya unyanyanyasasi au uonevu wa Polisi, na yanazidi kujitokeza, lakini inakuwa kama Serikali kwa makusudi inapuuza hali hii. Ni lini serikali itaona umuhimu wa kuwa na mamlaka itakayosimamia na kulichunguza jeshi la Polisi dhidi ya malalamiko ya rushwa, ukandamizaji wa wanasiasa wa upinzani, kubambikiwa kesi, kupigwa watuhumiwa, kuuwawa watu wakiwa kizuizini, matumizi ya nguvu isivyostahili, kunyimwa haki ya dhamana, kudhulumiwa nk?
Je, ni matukio mangapi ya namna ya Hamza tunataka yatokee nchini ndio tuelewe kwamba tunahitaji chombo ambacho kitakuwa na mamlaka ya kuwasimamia Polisi (Independent Police Oversight Authority) na kuchunguza malalamiko yanayotolewa dhidi ya vitendo vya ukandamizaji, unyanyasaji na uvunjifu wa haki za binadamu dhidi ya Watanzania?
Hili si la Raisi Samia tu, bali wabunge wote lazima mjipe changamoto ya kufikisha huu muswada Bungeni haraka iwezekanavyo.
Tusisahau kwamba, tofauti na Hamza, watu wengi wenye chuki dhidi ya Polisi kinachowazuia kufanya alichofanya Hamza ni kwamba hawana uwezo wa kupata silaha kama Hamza, lakini wangekuwa na uwezo huenda tungesikia yaliyo makubwa kuliko hata ya Hamza.