Ushauri kwa Rais Samia: Malalamiko dhidi ya Polisi yanazidi, Muswada wa Mamlaka ya Kusimamia/Kuwachunguza Polisi unahitajika haraka

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Kwako Rais Samia. Suala la mgongano kati ya Hamza na Polisi sio jipya kutokea nchini, labda tofauti kubwa ni kwamba Hamza alichukua hatua ya kulipiza kisasi kwa kuwaua askari.

Kila siku malalamiko dhidi ya unyanyanyasasi au uonevu wa Polisi, na yanazidi kujitokeza, lakini inakuwa kama Serikali kwa makusudi inapuuza hali hii. Ni lini serikali itaona umuhimu wa kuwa na mamlaka itakayosimamia na kulichunguza jeshi la Polisi dhidi ya malalamiko ya rushwa, ukandamizaji wa wanasiasa wa upinzani, kubambikiwa kesi, kupigwa watuhumiwa, kuuwawa watu wakiwa kizuizini, matumizi ya nguvu isivyostahili, kunyimwa haki ya dhamana, kudhulumiwa nk?

Je, ni matukio mangapi ya namna ya Hamza tunataka yatokee nchini ndio tuelewe kwamba tunahitaji chombo ambacho kitakuwa na mamlaka ya kuwasimamia Polisi (Independent Police Oversight Authority) na kuchunguza malalamiko yanayotolewa dhidi ya vitendo vya ukandamizaji, unyanyasaji na uvunjifu wa haki za binadamu dhidi ya Watanzania?

Hili si la Raisi Samia tu, bali wabunge wote lazima mjipe changamoto ya kufikisha huu muswada Bungeni haraka iwezekanavyo.

Tusisahau kwamba, tofauti na Hamza, watu wengi wenye chuki dhidi ya Polisi kinachowazuia kufanya alichofanya Hamza ni kwamba hawana uwezo wa kupata silaha kama Hamza, lakini wangekuwa na uwezo huenda tungesikia yaliyo makubwa kuliko hata ya Hamza.

 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
  • In Kenya, the Independent Policing Oversight Authority (IPOA) was established through an Act of Parliament published in November 2011 to provide for civilian oversight over the work of the police in Kenya. IPOA mission is to conduct impartial and independent investigations, inspections, audits and monitoring of the National Police Service to prevent impunity and enhance professionalism in the interest of the public. The Authority receives complaints from members of the public on police misconduct and undertakes independent investigations, including deaths and serious injuries arising from police action
  • In South Africa the South Africa, the Independent Police Investigative Directorate Bill, was published in Government in 2010. The South African IPD Act stipulates that IPID shall investigate any death in police custody or as a result of police action; may investigate any misconduct or offense allegedly committed by a South African Police Service member
  • In UK Police Reform Act 2002 created the Independent Police Complaints Commission (IPCC), which was established in 2004. IPCC, a non-departmental public body funded by the Home Office, has national and regional offices. IPCC oversees the whole of the police complaints system. It can choose to manage or supervise a police investigation into a case and independently investigate the most serious cases
  • In Ghana, the Ghanaian Police Council is a constitutional body that advises the president on matters of policy relating to internal security, including the role of the police, budgeting, finance and administration, as well as recruitment.
  • In Australia, there are a number of agencies providing independent and impartial investigation and detection (with accompanying coercive powers), as well as prevention campaigns:
  • In British Columbia, Canada, the Office of the Police Complaint Commissioner provides civilian oversight of complaints regarding municipal police. The Office is completely independent from the police, government agencies and political parties.
  • In France, the Commission nationale de déontologie de la sécurité (CNDS) is the only independent institution overseeing the police. Complaints are filed indirectly: only the Prime Minister and individual members of parliament can refer a matter to CNDS,
  • In Lesotho, the Police Complaints Authority, established in 2003 but operational since 2005, is an independent oversight body that monitors questionable police conduct and addresses grievances against the police. It is empowered to investigate complaints about police misconduct and make recommendations for disciplinary action to the Commissioner of Police and for prosecution to the Director of Public Prosecutions.
  • In Malaysia, the Enforcement Agency Integrity Commission is a new independent oversight body targeting all law enforcement agencies (not only the police), which can receive and investigate complaints. Additionally, they visit detention facilities
  • In the Philippines, the People’s Law Enforcement Board receives complaints, conducts investigations and hearings, adjudicates on citizens’ complaints against Philippine National Police officers and members
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,559
2,000
Wafuasi wa Mbowe ndio wanachuki na Jeshi la Polisi eti kisa Mbowe kafunguliwa kesi ya Ugaidi!

Jeshi letu la Polisi chini ya Kamanda IGP Sirro ni IMARA kama chuma.

hakuna mhalifu yeyote atakaye salimika.

Songa Mbele polisi wetu kamwe msibabaishwe na hawa wahuni wachache, wavuruga amani,
Hamza alikuwa Gaidi kama anavyo tuhumiwa Mbowe na wezake.
Tunawaomba Jeshi letu lifuatilie nyenendo za viongozi wa chadema pamoja na baadhi ya wafuasi ambao wana dalili za kuwa na tabia za kigaidi.
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,560
2,000
Kama umezaliwa mwaka huu labda.

Watu wazima tunajua awamu ya nne polisi ilikuwa inanuka kiasi gani.

Kwa tabia za kipuuzi za watz kuna siku tutataka hicho chombo kiundiwe chombo kikuchunguza.
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Wafuasi wa Mbowe ndio wanachuki na Jeshi la Polisi eti kisa Mbowe kafunguliwa kesi ya Ugaidi!

Jeshi letu la Polisi chini ya Kamanda IGP Sirro ni IMARA kama chuma.

hakuna mhalifu yeyote atakaye salimika.

Songa Mbele polisi wetu kamwe msibabaishwe na hawa wahuni wachache, wavuruga amani,

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna sehemu inasema wafuasi wa Mbowe hawana haki ya kulalamika dhidi ya Polisi, na ndio maana tunahitaji hicho chombo.

Hamza hakuwa mfuasi wa Mbowe, lakini alikuwa na sababu ya kukitumia chombo kama hicho na kingekuwapo huenda kusingekuwa na haya mauaji
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Juzi hapa Polisi wamevunja Mkutano wa ndani wa juu kabisa wa NCCR-Mageuzi, wakidai ni kwa amri toka juu. Mbatia alimpigia simu Waziri wa Mambo ya Ndani kutaka kujua kulikoni, waziri wala hana habari wala hajataarifiwa juu ya zuio la mkutano huu wa juu wa NCCR.

Ni wazi tumefikia mahali Polisi wanajiona wao ndio mamlaka ya mwisho nchini, IGP ni mkubwa kuliko mawaziri hata Raisi. Sasa hii ni hatari sana. Tunahitaji chombo huru cha kuwasimamia Polisi
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,229
2,000
AUYZ3t.jpg
 

Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
5,117
2,000
Hata chizi hujiona mzima
Wafuasi wa Mbowe ndio wanachuki na Jeshi la Polisi eti kisa Mbowe kafunguliwa kesi ya Ugaidi!

Jeshi letu la Polisi chini ya Kamanda IGP Sirro ni IMARA kama chuma.

hakuna mhalifu yeyote atakaye salimika.

Songa Mbele polisi wetu kamwe msibabaishwe na hawa wahuni wachache, wavuruga amani,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Narudia tena, kuna umuhimu wa kuwa na chombo huru cha kuchunguza matukio kama ya Hamza. Huwezi kuwapa polisi wachunguze wakati kuna tuhuma kwamba walimdhurumu Hamza. Ndio maana tunapewa taarifa kama hii tuliyopewa juu ya Hamza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom