mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 887
- 705
Mikataba mibovu katika sekta ya nishati,madini,manunuzi,na ujenzi wa miundombinu kitita ni chanzo kikuu cha umaskini uliokithiri katika taifa letu.Umaskini husika umetokana kwa kiasi kikubwa na ulaghai,rushwa kubwa,Ufisadi,Ubinafsi,matumizi mabaya ya madaraka,ujasiliamali wa kisiasa na ubovu wa katiba na udhaifu wa sheria zetu.
Maridhiano ya kitaifa kupitia tume maalumu yangelazimisha wote walioifisidi nchi,ilaghai nchi,ifitini nchi,Walioingia mikataba ya ulaghai,Mikataba mibovu,waliotengeneza mikataba ya kimangungo..ikiwemo ya uchimbaji madini,gesi,uvunaji misitu,Usafirishaji..
Tume ya maridhiano itawalazimisha wote wanaoguswa na kusababisha hasara kubwa kwa nchi kwa namna moja au nyingine na kuwataka waungame,watubu, kukiri madudu walioyafanya na kurejesha mali zote walizojirimbikizia kupitia mihamala yenye kuliangamiza taifa.Watapaswa kukiri siri zenye uovu ndani zenye chemuchemu isababishao umaskini,mateso,unyonyaji na uharamia wa rasilimali za taifa Tanzania...