Ushauri kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu migomo ya wafanyakazi Tanzania: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa Rais Jakaya Kikwete kuhusu migomo ya wafanyakazi Tanzania:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Aug 6, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kwako Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,Rais na Amiri Jeshi Mkuu wan chi yangu Tanzania. Kwa heshima na taadhima napenda kukuandikia kupitia mtandao huu wa JamiiForums nikiwa na imani kwamba ushauri huu utausoma wewe mwenyewe au wasaidizi wako wa Ikulu,Usalama wa Taifa au Waziri anayehusika na Utumishi.Nina imani kuwa kuna siku huwa unapitiapitia humu kwenye Jamiiforums na Facebook.

  Mimi nikiwa mfanyakazi wa Serikali nimesikitishwa sana na matukio mawili ya hivi karibuni yakihusiana na migomo ya Wafanyakazi wa sekta ya Afya na Elimu. Sekta ambazo naamini kuwa ni muhimu sana kwa mstakabali wa Taifa letu. Kwamba bila Madaktari basi afya za Watanzania ziko mashakani na bila ya Waalimu basi Elimu ya Watanzania hali kadhalika itakuwa mashakani. Migomo yote miwili imetangulizana na yote ilikuwa ni ya madai ya kuongezewa Mishahara na Posho kulingana na umuhimu wa sekta hizi mbili.Ni kweli kwamba mishahara ya Wafanyakazi wa nchi hii katika sekta karibu zote haikidhi mahitaji ya Wafanyakazi kwa muda mrefu sasa.

  Mheshimiwa Rais,serikali yako inayoongozwa na CCM imeshindwa kabisa kuboresha Maisha ya Watanzania wakiwemo Wafanyakazi japo kwa asilimia kidogo kama ulivyo ahidi wakti ukiingia madarakani mnamo mwaka 2005. Nasikitika kusema kwamba uliwadanganya Watanzania. Pengine yawezekana ulitumia lugha hii ya kuboresha Maisha ya Watanzania kama hila ya kuweza kujipatia kura nyingi za kukuingiza madarakani. Inasikitisha kuwa maisha bora yameshindikana kwa muda wote wa miaka 7 ambayo umekuwa madarakani pamoja na kuwa nchi hii imejaliwa utajiri wa Maliasili nyingi za madini lukuki ambazo badala ya kuwanufaisha Watanzania sasa zinawanufaisha Wageni wanaojulikana kama Wawekezaji pamoja na nchi zao!

  Ni dhahiri kuwa serikali yako imeshindwa kuleta Maisha bora kwa wafanyakazi kwa kuwaongezea mishahara na posho zingine kwa kisingizio cha Serikali Haina Pesa japo madai hayo siyo kweli. Nikiwa Mtanzania mzalendo napenda leo kukupatia Ushauri wa bure kabisa kuhusu kutatua migogoro hii ya Wafanyakazi inayojitokeza mara kwa mara kwa sababu ya mishahara na posho duni zinazotolewa kwa Wafanyakazi.Kwa vile serikali inasema na inakiri kuwa haina pesa ya kuwalipa Wafanyakazi wake ukweli ni kwamba nchi hii ina utajiri unaowanufaisha Mafisadi wachache na Wawekezaji Uchwara. Bila shaka una taarifa na Mabilioni au Matrilioni yaliyogunduliwa hivi karibuni kwenye Mabenki ya Uswisi. Hiyo ni pesa ya Watanzania inayopashwa kurudishwa Tanzania kama ilivyorudishwa Chenji(Rushwa ya Rada) ili iweze kuboresha Maisha ya Watanzania ikiwemo kuongeza Mishahara ya Madaktari na Waalimu.

  Ushauri wangu ni kwamba: Kama serikali imesema haina uwezo wa kulipa ongezeko la mishahara na posho kwa Wafanyakazi hususani Madaktari na Waalimu basi kuna haja kwa Serikali sasa kuangalia upya sheria ya KODI kwa mfanyakazi ijulikanayo kama P.A.Y.E. kwa maana ya kuipunguza ili kumpa unafuu mfanyakazi huyu anayepata mshahahara ambao nathubutu kuuita kuwa ni sawa na ujira kwa kwa kibarua wa kutwa. Tunajua serikali imeweza kusamehe Makampuni makubwa ya wawekezaji kutolipa kodi kwa miaka 5 maarufu kama TAX HOLIDAY. Je,serikali inashindwaje kuwapunguzia Wafanyakazi KODI? Naamini kabisa unafuu wa kodi ukitolewa utakuwa kama nyongeza ya mshahahara kwa Watumishi wote.

  Itakuwa ni jambo la kusikitisha na kushangaza kama Serikali itakuja na madai yaleyale ya kuwa haiwezi kuwapunguzia kodi Wafanyakazi maana itakosa mapato ya Mabilioni toka kwenye Kodi!. TRA wana kanuni zao za kukokotoa KODI ya mshahara na ukiangalia kwa undani kabisa utagundua kuwa Wafanyakazi ndiyo wanaoumizwa zaidi na mfumo huu wa PAYE kwa vile wao huwa hawana namna ya kukwepa makato haya. Tunajua kuna Wafanyabiashara wengi ambao huwa wanakwepa kulipa kodi ya mapato kwa kushirikiana na maafisa wa TRA kwa kuonyesha mapato kidogo au kuuza bidhaa bila risit na hivyo kuikosesha serikali mapato. Mfanyakazi hana namna ya kukwepa kodi maana yeye anakatwa moja kwa moja toka kwenye mshahara wake kabla hata hajaupokea.

  Sheria ya TRA imeweka viwango maalumu kwa Wafanyabiashara ili kuweza kulipa VAT. Kuna wafanyabiashara hawalipi VAT kwa vile mapato yao hayafikii kiwango Fulani cha mapato kwa mwaka. Lakini mfanyakazi yeye atafyekwa tu bila kujali mapato ya mfanyakazi huyu kwa mwaka. Sheria ya VAT inasema mfanyabiashara alipe 18% tu ya kila pato analoingiza kwa kila biashara anayofanya. Jambo la kushangaza ni pale PAYE inapokuwa kubwa kuliko hata VAT ya mfanyabiashara anayeweza kutengeneza mamilioni kwa mwaka achilia mbali kwa wiki au kwa mwezi. Huu hakika ni ukandamizaji na unyonyaji wa mfanyakazi maskini mwenye mshahara sawa na ujira wa kibarua wa kutwa. Hapa chini nimeambatanisha Jedwali linaloonyesha makato ya PAYE kwa mwezi na mapato mengine yoyote atakayopata mfanyakazi nje ya mshahara wake.Kwenye Bajeti ya waziri wa Fedha ya mwaka 2012/13 tumesikia ongezeko la kima cha chini cha Mfanyakazi toka Tshs.80,000/= kwenda Tshs. 135,000/=.
  Guide to Income Tax Act, 2004

  Rates for withholding tax on employment - Pay As You Earn (PAYE)
  Note: Income here refers to monthly income.
  Income includes the value of benefits in kind and allowances (which are not to cover certain employer expenses in doing your job) received during the month.
  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Total Monthly Income
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Rate Payable
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where total income does not exceed Shs. 80,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  NIL
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where total income exceeds Shs. 80,000 but does not exceed Shs. 180,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  18.5% of the amount in excess of Shs. 80,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where total income exceeds Shs. 180,000 but does not exceed Shs. 360,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Shs. 18,500 plus 20% of the amount in excess of Shs. 180,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where total income exceeds Shs. 360,000 but does not exceed Shs. 540,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Shs. 54,500 plus 25% of the amount in excess of Shs. 360,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where total income exceeds Shs. 540,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Shs. 99,500 plus 30% of the amount in excess of Shs. 540,000
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Makato ya PAYE kwa wafanyakazi wa Tanzania ni makubwa sana ukilinganisha na kile wanacholipwa. Hivyo kuna haja ya Waziri wa Fedha na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais( Menejiment ya Utumishi wa Umma) kukaa pamoja na kuangalia namna ya kuwapunguzia Wafanyakazi mzigo huu wa KODI kwa vile Serikali imeshindwa kuwaongezea Mishahara. Wazungu wanasema,''something is better than nothing" kwa maana kwamba kile kidogo watakachopata kutokana na kupunguziwa mzigo wa Kodi basi ni bora kuliko kutopata kabisa hata hiyo nyongeza.

  Kama Jedwali linavyoonyesha hapo juu,mfanyakazi wa Tanzania anakatwa makato yanayokaribia au kuzidi robo ya Mshahara wake yaani wastani wa 25% na zaidi.
  Nitaeleza: Tuchukulie mfanyakazi wa kawaida anayelipwa Mshahara wa kati ya Tshs. 360,000/= lakini hauzidi Tshs.540,000/=. Kwanza kabla ya yote anatakiwa awe ameshanyang'anywa Tshs. 54,000/= kabla ya kukatwa PAYE ya 25% kwa kila shilingi inayozidi Tshs.360,000/=. Tuseme nina lipwa Tshs. 539,000/= kwa mwezi. Hapa TRA watachukua Tshs.54,000/= kwanza na halafu Tshs. 539,000-360,000/=179,000 X 25/100=Tshs.45,000/= + 54,000/= total ni Tshs.99,000/= Ukichukua hii Tshs.99,000/= ukakokotoa kwa asilimia ya Mshahara halisi wa Tshs.539,000/=unakuta kwamba huyu Mfanyakazi kalipa 54,000/= ambayo ni 15% ya Tshs.360,000 jumlisha na 25% ya Tshs. 179,000/=. Kwa hiyo mshahara huu wa mfanyakazi unakatwa KODI mara mbili bila sababu.
  Tuchukue tena Mfanyakazi anayelipwa Tshs. 850,000/=kwa mfano. Huyu anatakiwa alipe kwanza Tshs.99,500/= ya Tshs.540,000/=na ndipo akatwe tena 30% ya Tshs.310,000/=sawa na Tshs.93,000/=. Ukijumlisha kodi zote 2 unapata Tshs.192,500/= ambayo averall percentage ni 22.64% zaidi ya VAT ambayo ni 18 % .

  Ukija kwenye ukokotoaji wa pato la mfanyakazi kwa mwaka unakuta kwamba anapata Tshs.850,000/= X 12 sawa na Tshs.10,200,000/= kwa mwaka lakini analipa 22.64%. Mfanyabiashara anayepata kiasi hiki cha Pesa kwa mwaka haruhusiwa kulipa Kodi ya VAT mpaka pato lake lifikie zaidi ya Tshs.20,000,000/=(20m Tshs.)kwa mwaka! Hapa chini naambatanisha Jedwali la Mlipa Kodi ambaye ni Mfanyabiashara.

  Individual businesses with turnover less than Tsh 20 million

  If your individual business has a turnover (total value of sales) of less than Tsh 20m, you have a choice. If you keep only very basic records which can show the TRA only which turnover band you are in, you must pay the fixed presumptive rates below. If you keep better records allowing you to demonstate accurately your turnover to the TRA, you may choose to be assessed according to the percentage of turnover presumptive rates below. If you keep good records of all your business transactions you may choose to submit a return and pay taxes on your net income (income minus expenses and deductions) calculated according to the income from business rules and pay tax on this net income according to the standard individual tax rates. It is in your best interest to keep as accurate records as possible, as paying tax on your net income is fairer than paying tax on your turnover.
  Presumptive income tax rates

  [TABLE="class: MsoNormalTable"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Annual Turnover
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Annual Tax payable where records are kept sufficient only to demonstrate turnover band
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Annual Tax payable where sufficient records are kept to demonstrate turnover accurately
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where turnover does not exceed Tsh 3,000,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tsh 35,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  1.1% of the turnover
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where turnover exceeds Tsh 3,000,000 but does not exceed Tsh 7,000,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tsh 95,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tsh 33,000 plus 1.3% of the turnover in excess of Tsh 3,000,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where turnover exceeds Tsh 7,000,000 but does not exceed Tsh 14,000,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tsh 291,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tsh 85,000 plus 2.5% of the turnover in excess of Tsh 7,000,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Where turnover exceeds Tsh 14,000,000 but does not exceed Tsh 20,000,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tsh 520,000
  [/TD]
  [TD="bgcolor: transparent"]
  Tsh 260,000 plus 3.3% of the turnover in excess of Tsh 14,000,000
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Mheshimiwa rais najua unajua kuwa kuna pesa nyingi sana katika nchi hii zinapotea kifisadi kupitia kwenye Ununuzi wa Mashangingi, Mishahara Hewa,Uwekezaji kwenye Migodi ya Madini, Mikataba ya Uwekezaji kwenye Kuzalisha Umeme,Viwanda ,Vitalu vya Uwindaji na Mahoteli. Tumesikia Matrilioni ya Tshs.yaliyoko kwenye Mabenki ya Uswisi na serikali yako bado imekaa kimya. Hapa Wafanyakazi ndipo wanapopata uchungu wanapojibiwa kuwa Serikali haina pesa!

  Mheshimiwa Rais, nahitimisha kwa kusema kwamba huu utaratibu ni unyonyaji kwa Wafanyakazi walalahoi wa Tanzania na kuneemesha wafanyabiashara wachache wanaopata mailinioni kwa mwaka na kulipa kodi kidogo.Kama kweli serikali yako ni sikivu kama ambavyo siku zote wewe mwenyewe na watu wako huwa mnadai basi naomba hili la KODI ya Wafanyakazi maarufu kama PAYE ulifanyie kazi ili wafanyakazi wapatiwe unafuu wa kodi ili kipato kwa mwezi kiongezeke walau kidogo maana Serikali haina pesa za kuongeza Mishahara ingawa kiukweli pesa zipo.

  Nawasilisha.
   
 2. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu ushauri mzuri
  but kwa JK inakuwa kama unapoteza mda wako na resource!
   
Loading...