Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Kwako Prof Muhongo,
Sina shaka kuwa utakubaliana nami kwamba ukiangalia gharama na "effort" kwa ujumla zilizotumika kutekeleza mradi wa gesi wa Songo Songo, ambazo kwa ujumla nadhani zilipita zaidi ya dola Milioni 700, leo hii tukiongelea kuwa matokeo ya mradi huo ni uzalishaji wa Megawati za Umeme 198, huenda dunia nzima ikatucheka. Yaani kule kuhamisha watu kwenye eneo la kupitisha bomba la gesi, kuwalipa fidia, na effort zote zilizohusu huo mradi ilikuwa kwa ajili ya Megawati 198 tu? Hivi kweli huu mradi kwa upande wa serikali uta-break even kabla ya hiyo gesi kwisha, ambapo makadirio yalikuwa miaka 25? Kimsingi, nguvu iliyoingizwa na serikali kwenye mradi wa Songo Songo ilipaswa iwe kwa ajili ya production isiyopungua Megawati 500.
Mradi huu unanikumbusha sana ule utani wanaofanyiwa ndugu zangu Wapare, kwamba Mpare anaweza kuwa ana kesi ya kuku na jirani yake, akaamua kumhonga hakimu mbuzi!
Na sasa tuko kwenye mchakato mwingine wa gesi toka Mtwara. Je, kwa mara nyingine tutaona nguvu nyingi ikitumika kuzalisha Megawati 100?
Prof. Muhongo ukiwa pale Afrika Kusini, nadhani uliona kwamba aina ya miradi yao ya power generation, mtambo wao mmoja tu wa kuzalisha umeme, unatoa umeme unaoweza kutoa umeme kwa Tanzania nzima! Yaani ingewezekana kabisa kituo cha Ubungo kuzalisha umeme kwa Tanzania nzima na kuzima vyote vingine nchini (japo kiusalama hili sio jambo jema). Na hii miradi yao sio ya technolojia ya ajabu - ni thermal generation ya kawaida tu kutumia makaa ya mawe, ila wanakuwa na busara ya ku-invest katika power generation katika scale kubwa, wakielewa pia mambo ya economies of scale. Itatuwia gharama kubwa kuwa na viji plant vidogo vidogo kama vya Songas kama ishirini hivi iili kuzalisha umeme wa kutosheleza demand ya Tanzania na hata kuuza nje.
Ushauri wangu kwako Mheshimiwa Prof. Muhongo ni kwamba let's start thinking big kwenye project za power generation. Tufikie wakati hapa nchini Tanzania, tunapopanga miradi ya kuzalisha umeme ya Tanesco, tuwe tunasema isiwe chini ya Megawati 300. Hadi leo hii tuna matatizo ya upatikanaji wa umeme kwa kuwa tumekuwa so mediocre katika kupanga project za power generation. Tumefanya mambo kiswahili swahili sana - kwa namna ya kuanzisha biashara za juice. Hii miradi ya Megawati 100 na ushee tuwaachie watu kama REA ndio wahangaike nayo, lakini iwe ni aibu kwetu kuweka so much effort ili kupata Megawati 100 sijui, kama tulivyofanya kwa Songo Songo.