Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu
Vita dhidi ya Wauza Madawa ya Kulevya haijawahi na haitakuja kuwa ya kitoto sehemu yoyote duniani. Ni vita inayowahusu watu wenye jeuri ya pesa na roho mbaya. Kuna wakati Serikali za Mexico, Brazil na Pakistani zilitaka kupinduliwa sababu tu viongozi wake walitaka kuchukua hatua kudhiniti mitandao hiyo.
Haya mashambulizi tunahoyaona sasa dhidi ya Makonda kwa sasa ni kutokana na vita aliyoanzisha ambayo imepewa baraka na Rais Magufuli. Kitendo cha kukamatwa watumiaji kimewatia pressure wauzaji maana wanaona sasa mambo yanaenda kuharibika. Wanaamini pia kuwekwa ndani akina Joan, Petitman, Wema Sepetu na wengineo kutafumua mitandao yote ya madawa ya kulevya.
Wito wangu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na vyombo vya dola. Kurudi nyuma katika mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya ni kubariki kuangamiza vizazi vyetu. Msirudi nyuma. Mtashambuliwa sana. Mtatishwa sana. Mtakebehiwa sana. Miongozo itaombwa sana Bungeni. Hizo ndizo gharama za mapambano dhidi ya madawa ya kulevya kote duniani. Hao wanaokushambulia wanatumia Bunge kama kichaka. Hayo mashambulizi hawawezi kuyasema nje ya Bunge na wala hutaona wanaandika kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii. Wanajua kuwa wana kinga ya Bunge.
Kadri watakavyowasakama ndivyo wanavyowapa nguvu ya kuwashughulikia mabosi wao. Endeleeni hivyo hivyo. Najua kwamba mlifanya uchunguzi wa kina kabla hamjaanza hii kamata kamata. Ushahidi mnao wa kutosha. Hawa akina Msukuma ambao wana hamu ya kuona Bunge linahalalisha matumizi ya Bangi wasiwakatishe tamaa. Endeleeni kupambana. Mungu yu pamoja nanyi na kwa hakika wadhalimu siku zao zinahesabika.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi wamefanikiwa kumkamata. Waziri wa Sanaa Nape Nnauye wameshamkamata. IGP Ernest Mangu wamegonga kisiki. Walitaka operesheni dhidi ya wauza unga isimamishwe eti inadhalilisha watu mashuhuri, akina Wema Sepetu. Watanzania, wapi tunaelekea? Kwa nini Madawa ya kulevya tunayaanudu kuliko Mungu?
Hivi katikati ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya mtu anainuka na kutaka Makonda asimamishwe kazi? Are we serious? Mchawi aliyeturoga amekufa?