Elections 2010 Ushauri kwa Oriwo; Namna ya kufanya utafiti wenye viwango...

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Napenda kumsafisha bwana Oriwo; mkurugenzi wa synovate. Majibu yao ni ya kweli kuwa 61% ya watanzania watampigia kura Kikwete. Hata hivo majibu yao sio halisi... wamepigwa changa la macho.

Nimenahatika kufanya tafiti kadhaa maeneo ya vijijini na mijini, najua jinsi matokeo yanavyoathiriwa. Ukifika huko, kwanza wewe ni mgeni, watu hawakufahamu nawe huwafahamu. Ili uweze kuwafikia watu kama umeshafanya sample selection labda kwa kutumia daftari la wakazi, ni lazima uombe msaada wa mwenyeji. Mara nyingi, anayefaa zaidi kutoa msaada ni mwenyekiti wa mtaa, au kiongozi yeyote wa serikali ya mtaa.

Unaondoka na mwenyeji wako unaanza kuzungukia walengwa wako. Amini usiamini, hata utumie mbinu gani, ni wananchi wachache sana wanaweza kuelewa kuwa unachofanya, hakihusiani na serikali. Ni katika mazingira hayo ambapo wachache sana ndiyo wanaothubutu kutoa maoni dhidi ya serikali au dhidi ya raisi aliyeko madarakani. Wananchi wale wanaamini kuwa kwa vyovyote, yale atakayoyasema, lazima utaenda kumwambia yule kiongozi wale wa mtaa, na kwa wengi wanaogopa kuwa huo ndio mwanzo wa matatizo kwao.

Katika utafiti ambapo tulikuwa tanatafuta amoni ya wananchi juu ya ubora wa hudumua fulani kati ya inayotolewa na serikali, na inayotolewa na watu binafsi, tuligundua kuwa watu wengi walikuwa wanasema serikali ndio bora. Kwa kuhakikisha kuwa majibu hayo ni halisi, sio ya uwoga tuliamua kubadili mbinu.

Tulidesign mabox fulani ambayo tulikuwa tunayavaa kwa kutunduka mgongoni. Yalikuwa na chemba mbili. Ilikuwa tumapita mitaani tukiwa na mbegu za mti fulani unaitwa 'mkusu' na tukikutana na mtu tunamuelezea kwa kifupi utafiti wetu, na tunampa mbegu moja tunamwambie aweke kwenye chemba ya serikali kama anadhani huduma ya serikali ndiyo bora, au chemba ya binafsi kama vinginevyo, katika box lile alilovaa mgongoni mtafiti. Tulifanya hivi tukimpa mtoa maoni nafasi ya kuweka ile mbegu bila kutazamwa na mtu mwingine. Amini usiamini, majibu kwa method hii yalikuwa SIGNIFICANTLY DIFFERENT na yale ya kutumia method ya kwanza.
 
duuhhh hii kali, ila ndio research techiniques, REDET na SYNOVET wanacopy na kupaste yaliyoandikwa kwenye vitabu.
 
Back
Top Bottom