USHAURI KWA ONLINE SHOPPING SITES

Chagga King

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
1,835
1,050
Nawashauri hawa wanaotoa huduma ya kutangaza bidhaa kwenye mitandao (online shopping sites) Mfano JUMIA (formerly Kaymu) hata ZoomTz.

Kumekuwa Na wimbi la watu wanaotumia hizo fursa vibaya, ntaeleza hapa
1. Kupost bidhaa bila kuweka bei, katika kitu kinachokera Ni pale mtu unapoingia kwenye hizi site unakuta vitu karibia vyote havina bei Na kwenye price tag unakuta umeambiwa "contact seller"
Sasa let say Kuna variety za bidhaa moja ambazo zinabei tofauti so unataka ujue kila bei Ili upate bei utakayoweza kuimudu, huwezi piga simu Na kuuliza "eti Samsung J5 Ni shillingi ngapi, Na J4 je, Mara vipi Tecno boom J8?," automatically utamboa muuzaji lakini ndo consumer behaviour yenyewe, so hii kitu inakunyima uhuru WA Ku negotiate.

Lakini pia hizi namba walizoweka wakati mwingine hazipatikani, Na huwezi piga usiku, au unampigia mtu anakwambia nipo nje ya ofisi.

2. Tangazo la bidhaa halioneshi mahala bidhaa ilipo (location), namba ya simu Na bei, hii inatokea Mara nyingi unakuta tangazo halina moja ya vitu nilivyovitaja au vyote, hili nalo Ni tatizo.

3. Kutokuwa makini katika kupost biashara yenyewe, unakuta mtu anapost bidhaa ila bei unakuta kakosea, wakati mwingine badala ya kuweka TZS anaweka US$, let say anauza bakuli unakuta price Ni USD5000, haha
Pia bei unakuta badala ya kuandika 1000 mtu anaandika 10000, Kuna IST nilikuta inauzwa milioni 127.

3. Picha zinazowekwa zimefifia Sana, au unakuta zimegeuzwa juu chini. Hii inaleta usumbufu

Kiukweli mapungufu Ni mengi, nimetaja machache, maana natumia simu kuandika. Kama Una Kero yako iweke hapa Ili wahusika waifanyie kazi.

Ushauri wangu sasa kwa wamiliki wa site yenyewe (web hosting) kuwa
1. Waweke criterias ambazo Ni mandatory, Mfano Price, Location etc ambazo bila kuzijaza hizo hutoweza Ku post bidhaa yako,
2. Halafu watu wenye matangazo mengi mngewatengea visehemu vyao, (pop-down tabs/menus) maana unakuta mtu amepost duka zima sasa, sasa kila mtu akipost hivyo online shopper anaboreka.

3. Muwe mnazipitia kuhakiki Kama zimekidhi vigezo, maana sidhani Kama huwa mnazihakiki.

Nawashauri hivi kwa sababu mnanufaika kwa huduma mnayotoa, sasa jitahidini kufanya ionekane smart.

Jumia, Kupatana, Zoom, n.k.
 
Back
Top Bottom