Ushauri kwa Ndalichako kuhusu Wakurugenzi na Maafisa Elimu

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,127
2,796
Awali ya yote nawapongeza watendaji niliowataja hapojuu kwa mchgango wao mkubwa sana katika ujenzi wa taifa.Nimeona nitoe mawazo yangu tena juu ya mustakabali wa kiwango cha elimu kwa kuzingatia suala mojatu la mafanikio na kutokufanikiwa katika kada ya elimu

Sio siri hata kidogo kwamba zipo changamoto nyingi za kiuteendaji,kimfumo na mazoea ambavyo huikabili kada hii achilia mbali changamoto za miundombinu,maslahi ya walimu na ubora wa elimu inayotolewa kutokidhi mahitaji ya wasoaji na mahitaji ya wakati tulionao kuanzi ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu.Wasomi kwa asilimia kubwa hawaandaliwi kujitegemea bali kadri mtu anavyosoma anazidi kuwa mzigo kwa taifa/tegemezi(kutegemea ajira serikalini)

Nirudi kwenye msingi wa hoja yangu ambapo ninataka kuzungumzia matokeo mabovu hususan shule za sekondari,ninazungumza kwa uzoefu uliopo ambapo kila mtu ambaye ni mdau wa elimu analielewa janga hili.Ninasisitiza kwamba ingawaje zipo changamoto lukuki lakini wakuu wa shule wahusike na kuwajibishwa kwa matokeo hayo.Ninasema hivyo kwa sababu haiwezekani mfano wanafunzi waliopo halmashauri moja tena shule zote za mjini maarufu kama shule za kata halafu,walimu wapo wakutosha(yaani mijini) na hatimaye shule fulani ikawa na wanafunzi waliofaulu halafu shule nyingine kwa miaka mfululizo inatoa sifuritu.Wakuu wa shule(baadhi) wapo wanasubiria kusimamia na kwenda kusahihisha mitihani,kuhudhuria vikao na dili za madawati
Ninauliza wakurugenzi, maafisa elimu na waziri husika je hii hasara hamuioni?

Uzoefu unaonyesha kwamba baadhi ya wakuu wa shule ni wazembe,wanafanyakazi kwa mazoea,niwatoro kazini,niwababe(hawashauriki/nimiungu watu),niwabadhirifu hivyo kupelekea matokeo hasi tofauti na malengo ya elimu hivyo shule hizo zimekua kama vijiwetu vya kuzalisha vijana wengi wasiokua na manufaa kwa elimu waliyo ipata na tafsiri yake nihasara kubwa kuanzia ngazi ya familia za wanafunzi hao mpaka taifa kwa upotevu wa rasilimali muda,fedha.Tena baadhi ya wakuu wa shule huchagua aina ya walimu wanaowataka kupelekewa kwenye shule zao.Wakuu wengi wa shule wanataka walimu wa kike kwasababu hawahoji na wale wanaohoji hufanyiwa fitina nakuhamishwa.Ushahidi mzuri ni shule nyingi katikati ya halmashauri za miji,wilaya na majiji ambapo walimu wakike ndiowengi na wanaume kutupwa pembezoni.Tatizo hilo hutokana na ukweli kwamba upo ukaribu/urafiki wa watendaji na wakuu wa shule usiokua na afya kwa taifa bali maslahi binafsi

USHAURI KWA VIONGOZI
*Wakuu wa shule wasikae vituoni zaidi ya miaka mitano

*Shule zenye wakuu washule wanaotoa sifuri wakati wenzao wa mazingira hayohayo wakifaulisha,wakuu hao washushwe vyeo na wafundishe katika shule hizohizo wasiondolewe

*Maafisa elimu kwa kiasi kikubwa wanazembea(kutojishughulisha na matokeo hasi ya wanafunzi)badala yake wanakaatu ofisini hawawajibiki kwa kuwaondoa wakuu wa shule wasio wajibika ipasavyo,wakurugenzi wawawajibishe maafisa elimu kwani kazi yao ni kuhakikisha malengo ya elimu yanatimia na sio kukaatu ofisini.Unamkuta afisa elimu hajawahi kutembelea shule kwa zaidi ya miaka miwili hii ni kensa kwa afya ya elimu

*Shule nyingi hazina bodi za shule hivyo mapato na matumizi,nidhamu mbovu kwa wanafunzi haviangaliwi na maafisa elimu wapotu

Ninasisitiza kwamba kwa matokeo mabovu ya wanafunzi mbali na changamoto zilizopo wakuu wa shule wanahusika pia

Ninashukuru nimetimiza wajibu kwa taifa langu
 
Nimeusoma uzi wako na kuuelewa kwa kiasi nilichojaaliwa na mwenyezi Mungu.
Nami kama mwananchi wa kawaida na mdau wa elimu nimewiwa kuchangia japo kidogo.

Ntajaribu kupitia hoja chache kati ya ulizozizungumzia.

Nikianza na hoja wakuu wa shule kuwa wapigaji, hilo lipo na nadhani ni karibu kila idara. Elimu, Afya, Polisi,...
Hilo suala ka kiasi kikubwa linatokana na tabia ya mtu ya kukosa uadilifu na uzalendo. Kuna mtu hata ofisini kukiwa na sh 10,000/=ataiba walau 1000 ili tu akidhi kiu yake . Lakini kwa upande mwingine, wa tz tuna stereotyping kwamba kila mkuu wa idara ni mpigaji, hata kama siyo. Inawezekana mtu alisimuliwa tu lakini akaamini. Kwa hiyo kuna mtu anatoka chuo kuja kuajiriwa kwa mara ya kwanza anajua mkuu wake wa kituo ni mpigaji, hata kama hajui anapiga nini hasa!

Kuhusu suala la wakuu wa shule kwenda kusimamia na kusahihisha mitihani, hilo sina uhakika sana hasa ikizingatiwa hujataja specifically kama ni mitihani ya taifa ama la. Kama ni mitihani ya taifa mkuu wa shule haruhusiwi kwenda kusahihisha, na hilo ni kati ya sharti mojawapo la NECTA. Kusimamia ni lazima asimamie kwenye kituo chake cha kazi kama msimamizi mkuu msaidizi. Lakini kumekuwa na malalamiko kwa walimu wengi na ya muda mrefu kuhusu baadhi ya walimu kuteuliwa kusimamia mitihani mara nyingi kuliko wengine. Hilo linahitaji ufafanuzi ulio nje ya uwezo wangu, nadhani TISS kupitia ofisi ya DSO wanakusika.

Walimu wa kike kupatikana wengi ktk shule za mijini, sababu yake kubwa ni kwamba walimu hao wanawafuata waume zao wanaokuwa wanafanya kazi huko. Hata hivyo siku hizi inasemekana kuna ndoa za kichina! Pia baadhi ya ma afisa elimu wasio waaminifu (baadhi nawafahamu) huwapanga walimu wa kike ktk vitu vya mjini kwa sababu maalum ikiwemo ya easy access (kifupi ni mboga zao)!

Kuhusu kutofaulisha kwa baadhi ya shule, kwa ufahamu wangu hili ni jambo very comlicated sana. Kwanza inatokana na attitude ya mwanafunzi. Kuna wanafunzi wanaenda sekondary bila kujitambua na bila malengo ya kufaulu. Hawa kwa kiasi kikubwa wanatokana na mfumo wa mitihani ya darasa la saba ambayo 100% ni Objective! Kuna mwanafunzi mwenye bahati anaweza kupata maswali yote ya mtihani mzima as long as ameweza ku shade correctly (betting?). Mwanafunzi kama huyu hata ungemleta Yesu Kristo au Mtume Muhamad (S.W) hawezi kuelewa. Lakini sababu nyingine inaweza kuwa ya ki genetic. Maana tunaambiwa kwamba mtoto ana inherit 40% ya intelligence kutoka kwa wazazi.(I stand to be corrected). 60% iliyobaki inatokana na mazingira, nutrition, diseases, interaction,.......! Hapa kuna tatizo kubwa. Watanzania tulio wengi hasa wa vijijini tunakula mlo mmoja kwa siku. Hata ukipatikana huo mmoja ni wa kufanya mwili na roho visitengane tu lakini siyo nutritious! Kuna mtoto anaishi kwenye nyumba ambayo ni sawa na nje, analala sehemu chafu, yenye wadudu, anawea kuwa hana shuka la kujifunika and so on ( wenzangu wataongezea). Kwa hiyo hapa hatuwezi kupata watoto waliojengeka vizuri kisaikolojia. Hata hivyo kuna baadhi ya walimu wanaitumia hii kama excuse ya kutowajibika ipasavyo.

Kwenye whether elimu yetu inatuandaa kujitegemea? Hapa pia napagusa huku mikono ikitetemeka kwa woga! Kwa sababu ni mara nyingi sana tunashuhudia ktk nchi zilizoendelea watu wakiwa barabarani wakiandamana kudai ajira. Sasa swali la kujiuliza ni je, hawa nao pia walipewa elimu ya makaratasi tu kwa maana ya vyeti? Kama siyo kwa nini wameshindwa kujiajiri mpaka wanaandamana? Kama ndiyo, kumbe sasa na sisi tuko sahihi maana na wenzetu wako hivyo hivyo? Kama mfumo wa elimu yetu ni mbovu hivyo unafaa kuangaliwa upya, ni mbovu ukilinganishwa na upi? Hapa nategemea wataalamu wa mifumo ya elimu na Uchumi watatusaidia.

Jambo la mwisho ni kuhusu nidhamu ya wanafunzi. Kwamba ni mbovu kwa kuwa wakuu wa shule na Bodi zao hawawajibiki. Hapa pia kunahitajika mjadala mpana. Nadhani walimu wote taaluma yaokwa kiasi kikubwa imejikita ktk malezi ya mtoto. Hivyo huu ni wajibu wa kila mwalimu shuleni kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na nidhamu nzuri. Mwalimu anayesubiri mkuu wa shule ku control nidhamu ya shule inabidi ajitafakari upya. Lakini pia malezi kwa kiasi kikubwa yanayegemeana na jamii inayowazunguka. Siyo siri kwamba jamii ya sasa ya kitanzania hailei watoto bali inafuga! Kwa hiyo tusitegemee shule tu ndiyo zitengeneze nidhamu za wanafunzi wakati ni chombo kidogo sana. (School is a miniature of a society). Pia hizi shule nyingi za kutwa za jamii a.k.a shule za kata halikuwa jambo lenye afya kimalezi. Kuna mwanafalsafa mmoja Jean Rousou (sina uhakika na spelling za sir name) aliwahi kusema kwamba: " If you want to educate a person separate him/her from the evil society". Sasa mtoto anakwenda na kutoka shuleni anakatiza mitaa iliyojaa madanguro, mateja, viroba , bangi,...... halafu utegemee awe na malezi bora, kivipi. Falsafa hii ndiyo wanayoitumia seminary kuziweka shule zao mbali na jamii (porini?).

Nimalizie kwa kusema kwamba suala la elimu na malezi kwa Tanzania ni kama kwa sasa halina mwenyewe kila anayejisikia anafanya analotaka. Hata mfumo wa uongozi haujakaa uzuri. Afisa Elimu anateuliwa na Katibu Mkuu wa wizara halafu anasimamiwa na DED aliyeteuliwa na mtu wa wizara nyingine. Hapa chain of command haijakaa vizuri. Kwamba mtu kateuliwa na Katibu mkuu wa wizara ya Utumishi ila madiwani wanaweza kumkataa na kumfukuza kazi,kweli?
Naomba niwasilishe.
 
Mkuu Mathematique nakupongeza sana kwa majibu ambayo yamekua chanya kwangu,nimechelewa kukujibu kwakua nilikua nimebanwa na mambo ya hapa na pale lakini naamini hata ukikawia bora ufike

Kuhusu suala la mitihani wapo wakuu wa shule za o-level wanaenda kusimamia mitihani ya kidato cha sita ila sio tatizo kubwa sana la kuhusianisha na matokeo mabovu kwenye shule zao

Juu ya nidhamu ya wanafunzi ukweli nikwamba zipo shule ambazo wakuu wa shule wamesusiwa wanafunzi na walimu wengine kwa kutokubaliana na ushauri wa kuwaondoa wanafunzi ambao ni madereva bodaboda,wateja wa viroba na mihadarati mingine.Wakuu hao wanatiliwa shaka kwamba wanakula hele kisha wanadai bodi za shule zilikaa na kujali juu ya maendeleo ya shule,hii ni kwasababu haiwezekani suala la kisheria la bodi ya shule kukaa kujadili maendeleo ya shule lakini bodi hazikai.Mkuu Mathematique nakuthibitishia kwamba kuna shule zina zaidi ya miaka mitatu na zaidi hawajawahi kukaa na bodi za shule,maafisa elimu hawafuatilii mambo hayo na hela zinapigwa na wakuu wa shule.

Pia wakuu wa mikoa nadhani ndio wanayo mamlaka ya kupitisha majina ya wajumbe wa bodi baada yakupelekewa majina na wakuu wa shule nao wanaangalia nani anafaa zaidi na wakisharudisha majina hayo kwa wakuu wa shule hawafuatilii tena.Huwa hawafuatilii wakiamini kwamba maafisa elimu wanafuatilia kumbe hawakusanyi taarifa muhimu kama hizo

Kuhusu matokeo ya wanafunzi kuhusianishwa na kurithi uwezo wa kiakili kwa wazazi na mababu zao,kama kuna ukweli ni kidogo mno kwani mbona shule jirani ambapo wanafunzi waliotoka lasaba shule moja,alama sawa lakini wanafeli kidato cha nne shule A n shule B wanafeli?Hapo nadiriki kusema watoto wanaangalia mitazamo,misimamo na muelekeo wa wakuu wa shule juu ya tabia,mienendo yao na matokeo ya mabovu

NINASEMA WAKUU WA SHULE WANACHANGIA SANA KUPOROMOSHA MORALI YA WANAFUNZI NA WALIMU KWAKUA WANAONA WAO PIA NIWATAWALA ETI NA WANAWADHIBITI WALIO CHINI YAO. WAKUU AMBAO WAMECHOKA KUSIMAMIA MAJUKUMU YAO WANASINZIATU OFISINI WAONDOKE WASIMAMIE WENGINE WENYE MITAZAMO CHANYA NA WANAOUMIA WANAFUNZI WAKIFELI
 
Miongoni kwa kansa ambayo Magufuli nilitegemea aanze kuipeleka OCEAN ROAD HOSPITAL ni Ma ofisa Elimu na Wakuu wa SHULE. Hawa ni tatizo awabadilishe ikiwezekana aweke vijana ambao wana ubunifu zaidi.

Kuna SHULE Fulani hapa Tarime mjini ni ya Hostel kuna watu wamejimirikisha kama mradi wao wa upatu. Kila wanapojisikia wanapandisha ada, ni ya serikali lakini inakuwa kama serikali imesafiri.
 
Hata wakibadilishwa wote nchi nzima serikali haipotezi hela yoyote maana wanabakitu hapohapo au wanahamia shule jirani.
Mh.Raisi anahangaika na madawati kwani hajui wakuu wa shule wamepiga dili?Hivi kuna shule mwanafunzi wa sekondari ameruhusiwa kusoma bila kulipa hela ya dawati?Hebu baadhi ya hao mchwa waondolewe ili elimu iboreshwe
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom