Mkumbwa Jr
JF-Expert Member
- Mar 23, 2016
- 2,624
- 3,652
Awali ya yote nawapongeza watendaji niliowataja hapojuu kwa mchgango wao mkubwa sana katika ujenzi wa taifa.Nimeona nitoe mawazo yangu tena juu ya mustakabali wa kiwango cha elimu kwa kuzingatia suala mojatu la mafanikio na kutokufanikiwa katika kada ya elimu
Sio siri hata kidogo kwamba zipo changamoto nyingi za kiuteendaji,kimfumo na mazoea ambavyo huikabili kada hii achilia mbali changamoto za miundombinu,maslahi ya walimu na ubora wa elimu inayotolewa kutokidhi mahitaji ya wasoaji na mahitaji ya wakati tulionao kuanzi ngazi ya msingi hadi vyuo vikuu.Wasomi kwa asilimia kubwa hawaandaliwi kujitegemea bali kadri mtu anavyosoma anazidi kuwa mzigo kwa taifa/tegemezi(kutegemea ajira serikalini)
Nirudi kwenye msingi wa hoja yangu ambapo ninataka kuzungumzia matokeo mabovu hususan shule za sekondari,ninazungumza kwa uzoefu uliopo ambapo kila mtu ambaye ni mdau wa elimu analielewa janga hili.Ninasisitiza kwamba ingawaje zipo changamoto lukuki lakini wakuu wa shule wahusike na kuwajibishwa kwa matokeo hayo.Ninasema hivyo kwa sababu haiwezekani mfano wanafunzi waliopo halmashauri moja tena shule zote za mjini maarufu kama shule za kata halafu,walimu wapo wakutosha(yaani mijini) na hatimaye shule fulani ikawa na wanafunzi waliofaulu halafu shule nyingine kwa miaka mfululizo inatoa sifuritu.Wakuu wa shule(baadhi) wapo wanasubiria kusimamia na kwenda kusahihisha mitihani,kuhudhuria vikao na dili za madawati
Ninauliza wakurugenzi, maafisa elimu na waziri husika je hii hasara hamuioni?
Uzoefu unaonyesha kwamba baadhi ya wakuu wa shule ni wazembe,wanafanyakazi kwa mazoea,niwatoro kazini,niwababe(hawashauriki/nimiungu watu),niwabadhirifu hivyo kupelekea matokeo hasi tofauti na malengo ya elimu hivyo shule hizo zimekua kama vijiwetu vya kuzalisha vijana wengi wasiokua na manufaa kwa elimu waliyo ipata na tafsiri yake nihasara kubwa kuanzia ngazi ya familia za wanafunzi hao mpaka taifa kwa upotevu wa rasilimali muda,fedha.Tena baadhi ya wakuu wa shule huchagua aina ya walimu wanaowataka kupelekewa kwenye shule zao.Wakuu wengi wa shule wanataka walimu wa kike kwasababu hawahoji na wale wanaohoji hufanyiwa fitina nakuhamishwa.Ushahidi mzuri ni shule nyingi katikati ya halmashauri za miji,wilaya na majiji ambapo walimu wakike ndiowengi na wanaume kutupwa pembezoni.Tatizo hilo hutokana na ukweli kwamba upo ukaribu/urafiki wa watendaji na wakuu wa shule usiokua na afya kwa taifa bali maslahi binafsi
USHAURI KWA VIONGOZI
*Wakuu wa shule wasikae vituoni zaidi ya miaka mitano
*Shule zenye wakuu washule wanaotoa sifuri wakati wenzao wa mazingira hayohayo wakifaulisha,wakuu hao washushwe vyeo na wafundishe katika shule hizohizo wasiondolewe
*Maafisa elimu kwa kiasi kikubwa wanazembea(kutojishughulisha na matokeo hasi ya wanafunzi)badala yake wanakaatu ofisini hawawajibiki kwa kuwaondoa wakuu wa shule wasio wajibika ipasavyo,wakurugenzi wawawajibishe maafisa elimu kwani kazi yao ni kuhakikisha malengo ya elimu yanatimia na sio kukaatu ofisini.Unamkuta afisa elimu hajawahi kutembelea shule kwa zaidi ya miaka miwili hii ni kensa kwa afya ya elimu
*Shule nyingi hazina bodi za shule hivyo mapato na matumizi,nidhamu mbovu kwa wanafunzi haviangaliwi na maafisa elimu wapotu
Ninasisitiza kwamba kwa matokeo mabovu ya wanafunzi mbali na changamoto zilizopo wakuu wa shule wanahusika pia
Ninashukuru nimetimiza wajibu kwa taifa langu