Ushauri kwa NCCR-MAGEUZI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa NCCR-MAGEUZI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ulukolokwitanga, Nov 12, 2010.

 1. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  NCCR Mageuzi ni chama kilichofanya vizuri sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Ingawa wabunge wake wote wanatoka mkoa mmoja na mlistahili kupata mbunge mmoja nje ya mkoa wa Kigoma lakini manyng'au ya CCm yakapora ushindi wenu kwa uchakachuaji lakini ni mafanikio makubwa sana. Chama kimepata wabunge vijana na wenye uwezo mzuri wa kujenga hoja, pengine kuliko hata mwenyekiti wa chama ambaye hoja zake ni zile zile kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Ushauri wangu kwenu ni kuwa mnayo nafasi nzuri zaidi ya kukiimarisha chama wakati huu kuliko wakati wowote ule, msijiingize katika mkenge wa kufanya alliance na chama cha CUF kuunda minority opposition bungeni kwakuwa msimamo wa cuf miaka yote huwa haieleweki na kwa sasa wana ndoa na ccm. Ni bora kama chama mkawa na msimamo wa peke yenu bungeni ambao ni wa upinzani utakaokitambulisha chama chenu kama chama dume cha upinzani, msikubali kufunikwa katika mwamvuli wa chama chochote. Hii itavutia watu wengi kukiunga mkono chama chenu na kuwaweka katika nafasi nzuri ya kupanuka kama ilivyokuwa zamani.
   
Loading...