Ushauri kwa Mwigulu: Chukua wenye shahada tu kwenye ajira mpya za polisi

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Siku chache zilizopita nilimsikia mwigulu akiongea bungeni kuwa Jeshi la Polisi lina mpango wa kuajiri vijana zaidi ya elfu nne ili kuongeza nguvu katika kukabiliana na uhalifu.

Imefika hatua sasa majeshi yetu kujaa wasomi badala ya kujazana darasa la saba. Napendekeza katika ajira hizi mpya vigezo vya mtu kuchaguliwa kujiunga na mafunzo kiwango kidogo cha elimu iwe degree na kuendelea.

Natuamini kuwa maoni haya yatafanyiwa kazi na Mwigulu pamoja na wizara kwa ujumla.
 
Siku chache zilizopita nilimsikia mwigulu akiongea bungeni kuwa jeshi LA Polisi Lina mpango Wa kuajiri vinaja zaidi ya elfu nne ili kuongeza nguvu katika kukabiliana na uharifu.

Imefika hatua sasa majeshi yetu kujaa wasomi badala ya kujazana darasa LA saba. napendekeza katika Ajira hizi mpya vigezo vya mtu kuchaguliwa kujiunga na mafunzo kiwango kidogo cha elimu iwe degree na kuendelea.

Natuamini kuwa maoni Hays yatafanyiwa kazi na Mwigulu pamoja na wizara kwa ujumla
hili ni jeshi, kuna haja ya kupima umbo la mtu na kuangalia ujasiri wake, sidhani kama elimu pekee inaweza kuwa kigezo bora.
unaweza kuta hata majeshini kama JWTZ makomandoo wakawa ni watu wenye elimu ya kawaida saaaaana.
kwa maoni yangu tuchukuliwe na sisi wenye division zero kwa kigezo cha physical appearence
 
Mkuu jeshini elimu sio kigezo hata kidogo cha kujiunga na jeshi bali nidhamu,uzalendo na Ujasiri ndio misingi pekee au sifa pekee za kuwa askari.2012 nilienda kujiunga JwTz nikiwa na degree yangu nikajua elimu ndio sifa kubwa,Ila nilipofika huko niliwakuta Military police (MP) ndio wakufunzi inasemekana elimu zao ni darasa la Saba tuu ila ni wazalendo na watiifu vibaya mno.
 
Ili na wew uliyesota miaka mitano baada ya ku graduate bila ajira upate ajiriwe???
Bahati za wenzio usilalie mlango wazi,, NJAA MBAYA AISEE, NA MWAKA HUU UTAIBA NAKWAMBIA..!!

Nakutania usije nimeza na Njaa njaa zako..!!!

Mimi sina mpango na hizo kazi Mkuu, maana hata umri wangu hauniruhusu ila ni ushautpri tu maana sasa hivi kinachotumika no teknolojia siyo nguvu. huyo darasa LA saba km Mimi anawezaje kutumia hiyo teknolojia
 
Jeshi LA Polisi lina askari ambao ni form four ni wana fani mbalimbali kama madereva, mafundi na kadhalika yaani Kuna watu wenye elimu ndogo ambao ni wakupokea oda ambao wanastaafu wakifikisha miaka 45 .
Haiwezekani kuajiri wenye degree tu watakosekana watu wa kutumwatumwa kwani wenye degree wote watakuwa maofisa soon
 
elimu sio kigezo chenye maana zaid.. ni vemawakatazama weled wa mtu kuoambana na ualifu,umbo na ukakamavu wake kwa ujumla.... by the way hao wenye degree wengi wao mboga saba watatuzingua tu matokeo yake polis wawili wanapigwa na raia mmoja si aibu hiyo?
 
Siku chache zilizopita nilimsikia mwigulu akiongea bungeni kuwa jeshi LA Polisi Lina mpango Wa kuajiri vinaja zaidi ya elfu nne ili kuongeza nguvu katika kukabiliana na uharifu.

Imefika hatua sasa majeshi yetu kujaa wasomi badala ya kujazana darasa LA saba. napendekeza katika Ajira hizi mpya vigezo vya mtu kuchaguliwa kujiunga na mafunzo kiwango kidogo cha elimu iwe degree na kuendelea.

Natuamini kuwa maoni Hays yatafanyiwa kazi na Mwigulu pamoja na wizara kwa ujumla
Nafasi zilizotoka kwa Polisi ni 2,543 tu kwa mwaka huu,uhamiaji 600,Magereza 500..zimamoto na uokoaji 600 na NIDA 40 na maofisa 26 wa ngazi za juu

Jeshi na usomi ni vitu viwili tofauti,ipo elimu ya Polisi akiwa kazini..Hao wasomi ni wasumbufu sana wakiwa kazini,kazi hawataki kufanya,wanachagua kazi...akiambia abebe bunduki aende Bank akalinde hataki,anasema yaani mimi na Master degree yangu nibebe bunduki nikalinde kweli?!Polisi mshahara hawana faida wala uzalendo,wako after money!!hawana sumu kabisa za jeshi..

Pitieni JKT kwanza mukafunzwe uzalendo ndipo mujiunge kwenye majeshi..
 
Wakati mnapanga kuajili wasomi utakuta majambazi wanaolihenyesha jeshi letu pengine hakuna jambazi hata mmoja mwenyeshahada kwa kuwa kupigana vita na degree ni vitu viwili tofauti.
 
Matatizo haya wananchi wanayolalamikia kufanyiwa na police Hii inatokana na ufahamu mdogo wa police lakini wanapewa mamlaka makubwa na kukabiziwa silaha za moto bila kujua haki za msingi za hao wanaowalinda
 
Siku chache zilizopita nilimsikia mwigulu akiongea bungeni kuwa jeshi LA Polisi Lina mpango Wa kuajiri vinaja zaidi ya elfu nne ili kuongeza nguvu katika kukabiliana na uharifu.

Imefika hatua sasa majeshi yetu kujaa wasomi badala ya kujazana darasa LA saba. napendekeza katika Ajira hizi mpya vigezo vya mtu kuchaguliwa kujiunga na mafunzo kiwango kidogo cha elimu iwe degree na kuendelea.

Natuamini kuwa maoni Hays yatafanyiwa kazi na Mwigulu pamoja na wizara kwa ujumla
Nakubaliana na wewe 100%.Kama wapo wenye degree na wako tayari kufanya kazi, kwa nini tuchukue Std VII levers,Form IV au hata Form VI wakati tumetumia fedha nyingi kuwa-develop. I think it's a good idea.
 
Mimi sina mpango na hizo kazi Mkuu, maana hata umri wangu hauniruhusu ila ni ushautpri tu maana sasa hivi kinachotumika no teknolojia siyo nguvu. huyo darasa LA saba km Mimi anawezaje kutumia hiyo teknolojia
Wewe ni Polisi?
Uliwahi kuwa Polisi?
Unajua jinsi jeshi la Polisi linavyofanya Kazi?
Unaujua Muundo wa Jeshi la Polisi?
Ni Idara au Taasisi gani iliyowahi kuajiri watu wenye kiwango kimoja cha elimu ikafanikiwa?
Ni teknolojia gani inayotumika na jeshi la Polisi ambayo Diploma, form VI na form IV hawaiwezi?
Nieleze angalau nchi moja duniani ambayo Polisi wake wote wana digrii.
 
Nafasi zilizotoka kwa Polisi ni 2,543 tu kwa mwaka huu,uhamiaji 600,Magereza 500..zimamoto na uokoaji 600 na NIDA 40 na maofisa 26 wa ngazi za juu

Jeshi na usomi ni vitu viwili tofauti,ipo elimu ya Polisi akiwa kazini..Hao wasomi ni wasumbufu sana wakiwa kazini,kazi hawataki kufanya,wanachagua kazi...akiambia abebe bunduki aende Bank akalinde hataki,anasema yaani mimi na Master degree yangu nibebe bunduki nikalinde kweli?!Polisi mshahara hawana faida wala uzalendo,wako after money!!hawana sumu kabisa za jeshi..

Pitieni JKT kwanza mukafunzwe uzalendo ndipo mujiunge kwenye majeshi..
Ungenieleza ulipo ningekuagizia kinywaji mkuu, huyu hawajui polisi maslahi.
 
Wakati mnapanga kuajili wasomi utakuta majambazi wanaolihenyesha jeshi letu pengine hakuna jambazi hata mmoja mwenyeshahada kwa kuwa kupigana vita na degree ni vitu viwili tofauti.
Hapana mkuu sikubaliana na wewe. Huhitaji kusoma sana kujua kwamba kusoma kuna kuongezea reasoning ability and hence uwezo kushuhulikia changamoto.Utakuwa mtu wa ajabu sana kupinga ukweli huu wa wazi.Kwa hiyo wazo la kuajiri vijana wetu wenye degree ambao hawana ajira kwa sasa ni muafaka kabisa.
 
Back
Top Bottom