Ushauri kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara kuhusu fedha zilizotolewa na Mgodi wa North Mara kwa ajili ya miradi ya Kijamii

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mkuu wa Mkoa wa Mara amezuia takriban Tshs.5 billioni zinazotolewa na mgodi wa North Mara kwa ajili ya miradi ya kijamii na hii imetokana na matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na mgodi wa North Mara. Binafsi nakubaliana na uamuzi wa Mkuu wa Mkoa.

Kama fedha zinatolewa na vifaa vya ujenzi vinanunuliwa kama sementi, nondo nk. na baadaye vifaa hivi havitumiki na hata kupelekea sementi kuganda mbona naona kama viongozi wa vijiji husika hawatimizi wajibu wao. Mkuu wa Mkoa anaendelea na kusema kuwa miradi karibu yote haina ubora kama inavyotakiwa.

Namshauri Mkuu wa Mkoa kufanya yafuatayo:-
  1. Kwanza kila kijiji kiibue mradi wake mfano ujenzi wa madarasa, kituo cha afya, zahanati,maji nk.
  2. Miradi ipitiwe na watalaam na kujua gharama ya kila mradi uliopendekezwa na kijiji husika.
  3. Tenda itangazwe kwa ajili ya ujenzi wa hii miradi na wale walioomba gharama zao zipitiwe na watalaam.
  4. Utekelezaji uanze kwa wale waliopewa kazi wakisimamiwa na watalaam kwa ajili ya ubora na pia ukaguzi ufanyike kwa kila hatua ya ujenzi.
  5. Mwisho wa mradi awepo mkaguzi atakayeteuliwa ma Mkuu wa Mkoa ili apitie miradi yote kwa ajili ya malipo ya mwisho.
  6. Mfuko huu usimamiwe na Kamati itakayoteuliwa na Mkuu wa Mkoa. Kutokana na hatua nilizozieleza hapo juu natumaini kuwa miradi itakayotekelezwa itakuwa na ubora na kutakuwa na thamani ya fedha.
Nawasilisha.
 
Kuna harufu ya upigaji hapo
 
Back
Top Bottom