Ushauri kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Salamu Rais wangu, naomba ujumbe huu ukufikie kwa njia yoyote. Naandika ujumbe huu nikiamini kabisa kuwa amani ya Tanzania bado ni nzuri sana, lakini pia naiona amani hii ikiwa katika kitisho kikubwa cha kuvurugika iwapo tu busara, utu na uzalendo hautatumika haraka iwezekanavyo.

Mhe Rais naandika haya nikiamini kabisa kuwa wewe ndiwe mwenye nafasi kubwa ya kuamua kuwa amani yetu iendelee kuwepo au vinginevyo kutokana na mabadiliko makubwa ya kisiasa yanayoendelea nchini. Rais wangu si siri tena kuwa Watanzania walio wengi wanahitaji mabadiliko makubwa ya uongozi wa nchi hii, na si siri pia viongozi wengi wa chama chako kilichomadarakani hawataki CCM itoke madarakani na wako tayari kutumia mbinu zozote kuliko kuachia madaraka hofu ikiwa na mazoea ya kutawala na maisha yao pindi chama kingine kitakapochua madaraka, haya ndio yanayonitisha.

Nimesema hapo mwanzo kuwa wewe ndio mwenye uwezo wa kuifanya Tanzania iendelee kuwa ya amani ukiamua au kuitumbukiza kwenye mgogoro kama nchi nyingine zenye mgogoro. Nakushauri kwa dhati kabisa na kutoka ndani ya moyo wangu kuwa ni vizuri leo ukadhamiria na kusema kwa dhati kuwa Tanzania kwanza Chama baadaye.

Amua kuweka misingi ya haki hasa katika masuala ya uchaguzi ili kuepusha vurugu katika uchaguzi 2015, dalili mbaya ziameanza kujionyesha katika chaguzi ndogo zinazoendele. Nakushauri Rais wangu achana na wale washauri wanaolenga maslai yao ya baadae. Usikubali kwa kuwa kwanza wakati mambo yatakuwa yameharibika utalaumiwa wewe na si wao, na hata kama hujali kulaumiwa pia ujue kuna maisha baada ya maisha ya hapa Duniani, roho za watu zitakazopotea zitakuwa zinalia mbele ya Mungu sasa pima.

Sasa fanya yafuatayo:
(a) Mchakato wa tume na uchaguzi huru ni lazima ili kuendeleza amani yetu kwa kuwa hata CCM wakishindwa wewe huna chakupoteza ushapiga miaka 10 na unastaafu na kuicha Tanzania na amani tele
(b) Jenga mazingira mazuri na wapinzani ili kusiwe na kulipizana kisasi wakati CCM itakapo kuwa mpinzani
(c) Waandae CCM kisakolojia kuwa kwa kuwaambia hawana hati miliki ya kuitawala Tanzania na wategee siku moja kuwa Chama cha Upinzani.

Mungu akubariki Rais wangu uione hatari kwa mapana yake.
 
Back
Top Bottom