Ushauri kwa Mh.Lowassa

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Namshauri Mh.Lowassa katika kufanikisha harakati zake za kujisafisha aandae kongamano katika kanisa lake na kutangaza kutubu waziwazi na kuahidi kurudisha mali yote aliyopata isivyo halali kwa masikini na kuwarudishia mara nne mali kwa watu aliowadhulumu na awombe radhi wote aliowadhalilisha na aahidi kubadilisha tabia yake.Hongera kwa kushinda kwa kuwanunua wamasai.
 
Mkuu unaongoza kwa kutoa ushauri humu jamvini. nimeona pia ule wa Dr Slaa
 
Mkuu unaongoza kwa kutoa ushauri humu jamvini. nimeona pia ule wa Dr Slaa

Ushauri wangu unajikita kwenye ukweli ili watu wasijisafishe kwa kujidanganya.Kama wanataka kujisafisha wawe wazi.
 
Watanzania wengi ni mafisadi kuanzia kifikra, kupokea vijisenti kwenye kampeni na hata kuomba rushwa kwa nguvu. Hii ni kuanzia ngazi ya chini hadi juu, kwa hiyo toa kwanza Boriti kwenye jicho lako ndio uone Kibanzi kwenye jicho la mwenzio. Je yupo awezaye kuwa wa kwanza kumpiga mwingine JIWE? Sote tukatubu tuombe Mungu kutuondolea hilo pepo kweye nchi yetu tuanze ufuasi mzuri upya.
 
Nahisi kwamba watoa hoja wana chuki zao binafsi nakushukuru nakwetu kwa ushauri wako
naomba kila mtu aisafishe nyumba yake kabla ya kumnyooshea kidole mwenzake. je lowasa ndiye anayetafuna halmashauri zetu nchini je wewe unayemtuhumu una usafi kiasi gani?
tukikubali kujisafisha, basi tz ijayo itakuwa nzuri na mahali pema pa kuishi. kumbuka kila mtu akipata nafasi basi anajilimbikizia mali. acha hizo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom