USHAURI: Kwa maslahi ya nchi, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ufanyike kwa ngazi ya Ubunge na Madiwani tu

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
WanaJf, Kwa haya yanayoendelea nchini (uchapaji kazi wa Rais magufuli) na hasa kukubalika sana kwa wanachi wa kawaida na hata wa kipato cha kati na juu (Machinga, wakulima, Mamantilie, Wafanyabishara n.k) ambao asilimia 90 ndio wapiga kura katika nchi yetu, JE SI UUNGWANA NA MATUMIZI BORA ya nafasi kwa vyama vya upinzani kuokoa bajeti ya uchaguzi wa Rais ili fedha zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.

Rais Magufuli apite bila kupingwa, lakini kwa Madiwani na wabunge tuchuane kwenye kampeni na boksi la kura?

Kwa Mtizamo wangu na kwa niaba ya Mtizamo wako ni wazi JPM atashinda kwa Kimbunga 2020.

Wenu, Mjukuu
 
Zamani JF ilikua na mada nzuri kutoka kwa wakongwe kama wewe ata na mimi. Yaani una hamka tu nakuandika kua uchaguzi kwa ngazi ya rais usifanyike kwakua wananchi wanamkubali. Mimi nilidhani ungekuja na data kabisa alafu ungetuambia ni ibara ipi au sheria ipi ya uchaguzi ina ruhusu ilo.
TUACHE KUIONENEA JF
 
Watanzania sio wajinga hata wamwache Dikteta Jiwe apite bila kupingwa.Lazima apata upinzani kwanza, ndani ya CCM na baadaye kama hao maCCM wasiojitambua watampitisha kuwa mgombea wao. Baadaye dhidi ya vyama vya upinzani

Huo wasiwasi ni wa nini kama kweli anapendwa sana, kafanya mengi mazuri ndani ya miaka minne tu? Kwa nini huo "uzuri wote" aliofanya usimbebe kwenye sanduka la kura ili aendelee kihalali?

Kama mazuri yake yanayotangazwa hadi kuchosha wananchi wanayaona ni mazuri na ndiyo kipaumbele chao, kwa nini awe na kigugimizi mtake njia ya mkato?

Ujenzi wa barabara, madaraja, hospital za wilaya na mikoa, vituo vya afya na zahanati, ununuzi wa ndege kadhaa, ujenzi wa Stieglers Gorge kuzalisha umeme wa kutosha. Najiuliza kwa nini vitu hivi visimbebe?

Tusisahau upande wa pili unaomtia hofu. Watu wasiojulikana, maiti za kwenye viroba ufukweni, risasi alizopigwa Tundu Lissu mchana kweupe, Kuingilia biashara ya mazao kama korosho kulikowafanya wana Kusini wakose mapato, Kufinya uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa watu kujieleza na kukosoa. Hivi viti vimempa madoa makubwa. Bado kuna trillion kadhaa zisizo na maelezo hata CAG hajui lolote, kuzuia shughuli halali za vyama vya upinzani ambavyo vipo kikatiba na kisheria. LAKINI kubwa kulko yote, ni utawala wake wa mabvu usiozingatia katiba wala sheria za nchi.

Kwa upungufu wote huo, hata ajenge Stieglers Gorge kumi, anunue ndege 100, ajenge barabara kila kata, ajenge hospital kila tarafa, bado wati watamkataa. Heri maskini huru kuliko mtumwa tajiri.
 
Naam kwa kuwa Magufuli atashinda kwa kishindo
Kuweka Uchaguzi ni kupoteza pesa tu

Hizo pesa zingeenda kujenga hospital

Nchi zote za kidictator huwa hazipendi uchaguzi, na wafaidika wa hao madictator ndio huupigia debe utawala huo uendelee kukaa madarakani bila uchaguzi.
 
Ni maoni yako lakini ni kwa maslahi yako binafsi na watu wachache na sio kwa maslahi ya taifa
 
WanaJf, Kwa haya yanayoendelea nchini (uchapaji kazi wa Rais magufuli) na hasa kukubalika sana kwa wanachi wa kawaida na hata wa kipato cha kati na juu (Machinga, wakulima, Mamantilie, Wafanyabishara n.k) ambao asilimia 90 ndio wapiga kura katika nchi yetu, JE SI UUNGWANA NA MATUMIZI BORA ya nafasi kwa vyama vya upinzani kuokoa bajeti ya uchaguzi wa Rais ili fedha zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.

Rais Magufuli apite bila kupingwa, lakini kwa Madiwani na wabunge tuchuane kwenye kampeni na boksi la kura?

Kwa Mtizamo wangu na kwa niaba ya Mtizamo wako ni wazi JPM atashinda kwa Kimbunga 2020.

Wenu, Mjukuu

Ushauri wako peleka kwa mumeo
 
Awamu hii watu wamekuwa waoga Sana hata kufiri tu imekuwa shida tunao waamini hatuwataki na tunao wataka hatuwaamini
 
Kazi ya mtakatifu ni kushindana na shetani, ukimuona mtakatifu anaogopa kushindana na shetani ujue utakatifu wake ni wamashaka.
 
Ni maoni yako lakini ni kwa maslahi yako binafsi na watu wachache na sio kwa maslahi ya taifa
Je unajisikiaje tutumie mabilioni kushindania nafasi ambayo mshindi tayari ameshapatikana kwa yale anayoyafanya na watu kumuunga mkono?Maslahi Binafsi ni kufuja fedha za Umma wakati tunaweza kuziokoa
 
Itakuwa ni wendawazimu kusubiri aachie kiti. Ana kila dalili ya kuwa Museveni au Kagame wa Tanzania.
Mh Rais anasubiri Muda wake ufike apumzike, HOFU yenu ni nipi???

Ameshasisitiza yeye atafanya kazi katika kipindi chake na atapisha, TATIZO mnadeal na kesi ndogondogo
 
Zamani JF ilikua na mada nzuri kutoka kwa wakongwe kama wewe ata na mimi. Yaani una hamka tu nakuandika kua uchaguzi kwa ngazi ya rais usifanyike kwakua wananchi wanamkubali. Mimi nilidhani ungekuja na data kabisa alafu ungetuambia ni ibara ipi au sheria ipi ya uchaguzi ina ruhusu ilo.
TUACHE KUIONENEA JF
Bishweko BADO MADINI yapo moja wapo ni hili la kuokoa fedha za Umma.
 
Katiba imeandika uchaguzi miaka 5 kwa rais, wabunge na madiwani. Kwa unadhauri tuvunje katiba ?
 
WanaJf, Kwa haya yanayoendelea nchini (uchapaji kazi wa Rais magufuli) na hasa kukubalika sana kwa wanachi wa kawaida na hata wa kipato cha kati na juu (Machinga, wakulima, Mamantilie, Wafanyabishara n.k) ambao asilimia 90 ndio wapiga kura katika nchi yetu, JE SI UUNGWANA NA MATUMIZI BORA ya nafasi kwa vyama vya upinzani kuokoa bajeti ya uchaguzi wa Rais ili fedha zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo.

Rais Magufuli apite bila kupingwa, lakini kwa Madiwani na wabunge tuchuane kwenye kampeni na boksi la kura?

Kwa Mtizamo wangu na kwa niaba ya Mtizamo wako ni wazi JPM atashinda kwa Kimbunga 2020.

Wenu, Mjukuu
Nishauri tu mkuu uhamie SHENZISTAN ambako watu hawaheshimu katiba ya nchi.
 
Mh Rais anasubiri Muda wake ufike apumzike, HOFU yenu ni nipi???

Ameshasisitiza yeye atafanya kazi katika kipindi chake na atapisha, TATIZO mnadeal na kesi ndogondogo
Kesi ndogo ndogo zipi?
Kagame aliwahi tamka tena kwa jazba, muda wangu ukiisha naondoka. Yupo mpaka kesho kutwa!
Dalili za mvua ni mawingu
 
Back
Top Bottom