Ushauri kwa Mamlaka ya maji safi na maji taka Mwanza (MWAUWASA)

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Kwanza ninawapongeza kwa huduma nzuri ya maji wanayoitoa lakini pamoja na pongezi hizo ninawashauri kwama ifuatavyo:-

Hapa Mwanza pindi umeme unapokatika pia na maji hukatika na hivyo kutupa taabu sana wakati umeme ukiwa haupo. Ninawashauri MWAUWASA wajenge matenki makubwa maeneo ya miinuko ili umeme unapokatika basi wananchi waweze kupata maji kutoka wenye matenki haya kwa njia ya gravity na hii pia itasaidia sana kuwapunguzia gharama ya umeme pindi haya matenki yakijaa wanaweza kuzima mashine zao na wananchi kupata maji kwa njia ya gravity.

Ninapoandika sasa hivi umeme umekatika na hakuna maji.
 
Huko mwanza ntapataje kiwanja kilichopimwa na serikali kisichokuwa na migogoro
 
Kuna tatizo la bomba kuu maeneo ya chanzo cha maji limepasuka tangia jana, na mafundi wapo wanalishughulikia ilo swala,worry not.
 
Naomba Mwenye contacts za operations Manager au MD wa Mwauwasa ndugu Sanga anipatie tafadhali. Huduma za upatikanaji Maji haziridhishi kabisa Mwaka huu ukilinganisha na miaka mitatu iliyopita.
 
Back
Top Bottom