Ushauri kwa kina kaka: Unapoanza mahusiano mapya epuka wanawake wa aina hii

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,220
USHAURI TU KWA KINAKAKA (TAKE IT OR LEAVE IT)
UNAPOANZA UHUSIANO MPYA EPUKA WANAWAKE WA AINA HII

1.MSICHANA WAKO WA ZAMANI
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

2.DADA WA RAFIKI YAKO KIPENZI
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

3.WANAWAKE WENYE MAMBO MENGI
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

4.WANAWAKE WANAOPENDA HELA KUPITILIZA (WACHUNAJI)
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.

5.MSICHANA WA ZAMANI WA RAFIKI YAKO
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea msichana wake toka zamani.
 
Tatizo kila ulilo liongea hasa no 1,2 na 5 yanamazingira tofauti katika utokeaji unaoweza kuwa na matokeo hasi au chanya.
 
Sometimes mabest hushauriana mapema juu ya kukabithiana makoloni ya zamani kabla hata ya demu kutongozwa ila wanawake wana huruma utashangaa anamkubalia huku akijua fika alikuwa rafiki wa ex wake soo amazing
 
Marafiki wa mwanamke wako pia kaa nao mbali
Inaonekana una wivu mkali sana shosti.
Ila kweli, mazoea mazoea mwisho wa siku unamkuta boy wako yuko na friend wako bar, ukiuliza eti ni ushemeji tu....mjini hakuna cha ushemeji.
Abiria chunga mzigo wako
 
Inaonekana una wivu mkali sana shosti.
Ila kweli, mazoea mazoea mwisho wa siku unamkuta boy wako yuko na friend wako bar, ukiuliza eti ni ushemeji tu....mjini hakuna cha ushemeji.
Abiria chunga mzigo wako
Mashost hawana maana hawakawii kutaka kuonja mhogo wangu
 
Back
Top Bottom