Ushauri kwa kamati ya CHADEMA itakayokutana na Rais Jakaya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa kamati ya CHADEMA itakayokutana na Rais Jakaya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumishi Wetu, Nov 24, 2011.

 1. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Waheshimiwa wana JF naomba kutoa mawazo na maoni kwa kamati itakayo kutana na Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Nina imani sote tutachangia ili kwa wale wakubwa wa CDM watakaokutana na Rais wetu wapate mawazo mapya na kujipanga kwa uzuri zaidi kuyawakilisha kwa mkulu wa boma letu la TZ:-

  1. Kwanza inahitajika busara na hekima kuu waliyo jaliwa hawa viongozi wetu ili waweze kuteka mtililiko wa kikao ili kiweze kuwa na matunda mazuri kwa nchi yetu.

  2. Kwanza wajue kabisa kama wanavyo elewa kuwa wanawakilisha Watanzania na hapo ndipo ulipo mustakabari wa taifa letu, kupona au kuingia kwenye misukosuko.

  3. Nawaomba watumie lugha isiyo na jaziba, yenye wingi wa ushawishi ili mkulu wa boma letu aelewe kuwa yeye anatawala kwa muda mfupi tu uliobaki miaka minne tu. Hivyo ni bora akaona ni busara kuwapa Watanzania katiba iliyo bora ambayo inadumu vizazi hata vizazi. Atoke kwenye box la chama awaze kama raia wa kawaida mwenye nia ya kuleta mabadiliko, nchi ipone!! Na yeye atabaki kwenye vitabu vya kumbu kumbu vya mashujaa wa nchi hii!!!!!!!!

  4. Kinyume cha hapo Watanzania hawatakubali kudanganywa na hila za kupewa katiba fake ambayo haina nguvu kama hii iliyopo isiyo na uwezo wa kudhibiti na kulinda rasirimali zetu; Isiyoweza kukemea watu wanaojichukulia madaraka na kuingia mikataba fake ya kufilisi nchi yetu.

  5. Mfahamishe kuwa akiwa kichwa ngumu katiba kwa namna yoyote na kwa kipindi chochote kile itapatikana na yeye atahukumiwa na historia kwa kufanya usanii kwenye maswala muhimu ya ukombozi wa taifa letu.

  Hadi hapo nawasilisha,naomba mawazo yenu waheshimiwa!

   
 2. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni imani yetu kwamba watafikia muafaka.
  Kwenye ile kamati sioni kama kuna mwenye jazba pale. Na kimsingi jazba ni matokeo ya kupuzwa kwa hoja za msingi.
  Naamini wata come out na kitu kinachoeleweka. Hawa ni watu wazima, wataelewana tu.
   
 3. KAZIMOTO

  KAZIMOTO JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  utaifa kwanza watafanikiwa
   
 4. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wote kwa pamoja walenge kwenye utaifa kwanza kuliepushia taifa letu baraa na machafuko!!!!!!!!!!
   
 5. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pia waelewe kuwa watanzania hawana haraka sana na katiba mpya. Issue siyo bora katiba mpya bali ni katiba mpya bora. Watanzania hawachoka hata kama itachukua miaka zaidi ya mitano kupata hiyo Katiba mpya bora.

  Tunaweza kwenda kwenye uchaguzi wa 2015 na katiba hii iliyopo kama baada ya hapo Tanzania itapata katiba mpya bora.
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wakikusikia wenyewe! subiri waje, mimi nasepa.
   
 7. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Maneno yako swadakta Mkuu HISIA KALI, kweli Watanzania hatuhitaji bora katiba bali tunahitaji katiba bora, itakayo kuwa mkombozi wawanyonge na mkombozi wa rasilimali zetu zinazo porwa usiku na nchana!!!!!!!!!!

   
 8. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wacha woga kijana kwa mtindo huu ukombozi utachukua muda mrefu kupatikana;stand up for your rights!!!!!!!!!!

   
 9. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kunahitajika kuchanga karata vizuri na kumuonyesha Mkulu kwamba hakuna njia ya mkato watu ni waelewa sio Watanzania wa enzi za Nyerere, hiki ni kizazi kingine kinahitaji mabadiliko!

  Katiba ndio italeta mabadiliko tunayo hitaji kulinda na kufaidi mali zetu wenyewe!!!!!!!!Bila mashinikizo ya mafisadi!!!!!!!!
   
 10. N

  Nakwetu Member

  #10
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona ni midume mitupu? Katiba ya midume sio?
   
 11. N

  Nakwetu Member

  #11
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngoja nimshtue Ananilea Nkya aunde kamati ya wakina mama na wadada kwenda kuongea na Rais maana tumeachwa na Chadema
   
 12. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii si tume ya kukusanya maoni ya wananchi ambayo ni lazima ihusishe watu wa namna tofauti ndugu, hii ni kamati ndogo kwa madhumuni maalumu. Kama ni hivyo utakavyo bado utaulizia walemavu, wazee, nk.
   
 13. m

  maluguthengosha Member

  #13
  Nov 24, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huwez jua wanaweza kulianzisha huko kwenye pango la wanyanganyi kna mama mnaweza umia.nafikir kuna kitu kikubwa hapo wanafanya
   
 14. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CHADEMA wakitaka kumfurahisha Rais waseme kwamba katiba mpya haitayaangalia mambo yaliyotendeka nyuma ila yale yatakayofuata baada ya uzinduzi wake. Nasema hivi kwa vile viongozi wengi na hasa walio na waliokuwa madarakani wanaogopa kuadhibiwa na katiba mpya kwa makosa yao (kama yatajidhihirisha).
   
 15. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2011
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa manufaa ya Watz tuna imani kamati itawasilisha maoni na mawazo yetu wote. Best wishes!
   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Baada ya hatua hii lazima na kina mama watahusishwa usijali, jahazia hili ni letu wote bila ubaguzi!!!!!!!!!!
   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hasa yeye Mkulu wamuhaidi immunity after his tenure, nadhani hapo wataweza kueleweka maana madudu ni mengi kwa term hii Hmaster!!!!!!!
   
Loading...