Ushauri kwa Jeshi la Zimamoto: Litoe elimu kuhusu majanga ya moto na namna ya kuchukua tahadhari

Toto Zembe

Member
Jul 15, 2019
74
99
Jeshi la zima moto kwanza nawapongeza kwa kazi nzuri ya kutekeleza majukumu yenu, lakini kuna sehemu mnakwama,.Sehemu hiyo ni katika utoaji wa elimu kuhusu majanga ya moto na jinsi gani ya kuchukua tahadhali pale janga linapo tokea

Jaribuni kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na hata ikiwezekana kuanzisha akaunti maalum ya YouTube,ili kuwafikia watu wengi bila kusahau kuanzisha hata vidawati vya kutoa elimu.

Wito wangu ni huo asanten sana.
 
Bila Shaka askari wa jeshi la zima moto ni wachache sana nchini ukizingatia na mahitajio ya nchi hawa kidhi mahitaji.

Serikali ongezeni idadi ya askari wa jeshi hili ili kukidhi mahitaji.
 
Elimu zianzie hadi ngazi ya shule za msingi. Japo ipo lakini nafikiri haitiliwi mkazo. Au njaa zinaamia hadi kichwani.
 
Chif mtu yoyote mwenye uwezo wa kutoa hiyo elimu na atoe kwa kadri mtu utakavyo weza,,,,
Lkn kutegemea jeshi la zimamoto tutachelewa,,hawatengewi mrungula wa kutosha hawa jamaa,,
 
Bila Shaka askari wa jeshi la zima moto ni wachache sana nchini ukizingatia na mahitajio ya nchi hawa kidhi mahitaji.

Serikali ongezeni idadi ya askari wa jeshi hili ili kukidhi mahitaji.
Na zana za kazi zisambazwe kila almshauri ya mji. Siyo moto unatokea wilayani nje ya mji alafu tutegeme zimamoto watoke town wauwahi, hydrants ziwepo maeneo yote hiyo iende sambamba na kutoa elimu kuhusu namna ya kuzuia majanga ya moto
 
Kwani wewe ujui moto unazimwa na nini Au hujui kama moto unaunguza .Wasichezee pesa za umma kwa upuuzi huu Maana ajali hizi zimeshatokea na wametoa elimu sana .Wacha kucheza na betri la kwenye gari la kubeba mafuta watu hapana sikia.
 
Ikiwezekana wapite kwenye mashule ya sekondari wafanye 'drill' na wanafunzi. Nimewahi kuwaona wakitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa viwanda na taasisi fulanifulani lakini nadhani haitoshi.

Eneo lingine muhimu kwenye uokoaji ni huduma ya kwanza, wengi hata waliopita shule wameisoma tu kwenye makaratasi, inapotokea ajari kila mtu ana panic na kukimbia huku wakilialia, wengine hubakia wameduwaa pembeni matumbo yakiwatetemeka wasijue cha kufanya, wale wachache wanaosaidia wanafanya kwa kujiongeza tu.
 
ikiwezekana wapite kwenye mashule ya sekondari wafanye 'drill' na wanafunzi. Nimewahi kuwaona wakitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa viwanda na taasisi fulanifulani lakini nadhani haitoshi.
eneo lingine muhimu kwenye uokoaji ni huduma ya kwanza, wengi hata waliopita shule wameisoma tu kwenye makaratasi, inapotokea ajari kila mtu ana panic na kukimbia huku wakilialia, wengine hubakia wameduwaa pembeni matumbo yakiwatetemeka wasijue cha kufanya, wale wachache wanaosaidia wanafanya kwa kujiongeza tu.
Hivi Tz kuna jeshi la zima moto au zima chadema majanga yakitokea wakijulishwa wanasema gari halina maji, wakati wakiambiwa chadema wana mkutano dakika sifuri na zima moto nao wanakuwepo na gari lao tena lipo full maji wako tayari kuwamwagia maji wanachadema ila sio janga la moto 😎😎😎😎😎😂😂😂😂
 
Jeshi la zima moto,kwanza nawapongeza kwa kazi nzuri ya kutekeleza majukum yenu,lakini kuna sehemu mna kwama,sehemu hiyo ni katika utoaji wa elimu kuhusu majanga ya moto na jinsi gani ya kuchukua tahadhali pale janga linapo tokea,jalibuni kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na hata ikiwezekana kuanzisha account maalum ya Utube,ili kuwafikia watu wengi bila kusahau kuanzisha hata vidawati vya kutoa elimu.

Wito wangu ni huo asanten sana.
Tatizo wabongo wabishi
Tamaa uwizi umetuzidi
Elimu mmpewe Mara ngapi

Ova
 
Jeshi la zima moto,kwanza nawapongeza kwa kazi nzuri ya kutekeleza majukum yenu,lakini kuna sehemu mna kwama,sehemu hiyo ni katika utoaji wa elimu kuhusu majanga ya moto na jinsi gani ya kuchukua tahadhali pale janga linapo tokea,jalibuni kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na hata ikiwezekana kuanzisha account maalum ya Utube,ili kuwafikia watu wengi bila kusahau kuanzisha hata vidawati vya kutoa elimu.

Wito wangu ni huo asanten sana.
Nadhani elimu itolewe mashuleni, kuanzia shule za msingi ili mtoto akue akijua
 
Back
Top Bottom