Ushauri kwa huyu rafiki

Perry

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
10,043
2,000
Rafiki yangu ana galfrd wake ambae wamedumu nae kwa takribani mwaka sasa,jamaa alikua na mipango mizuri sana kumhusu huyu dada lakni imetokea jamaa kabadilika ghafla baada ya yule mdada kumwambia kwamba eti ana ugonjwa wa ''athma'',mshikaji anadai eti huo ugonjwa ni wa kurith so anaogopa wanae wasije wakarith maradhi.kuna ukweli kwenye hlo swala wakuu?
 
Ni ukweli kuwa athma au pumu ni ugonjwa ambao mtu anaweza kurithi. Hivyo mshauri huyo jamaa yako kama kweli anampenda athma si tatizo kihivyo, halafu si wana mwaka hao jamaa zako katika mahusiano sasa ina maana kipindi chote alikuwa hajaliona hilo mpaka leo hii. Mimi naona point ni kuwa huyo jamaa yako amemchoka huyo demu, na linapokuja suala la kumshauri mtu aliyemchoka demu wake huwa pana shida sana.
 
....duh,ni kweli athma huwa inarithiwa ila jamaa,mhhh alikuwa anamtafutia sababu na kweli ameipata
 
Ni kweli asthma inarithiwa ila sio ugonjwa wa kufanya amuache gf wake.
Kuna watu wana ugonjwa na bado wanaishi vizuri tu.
OTIS.
 
jamaa hajampenda huyo dada
ila pia
ni vyema wamewekana wazi huenda mungu hakupanga wawe pamoja
huyo dada aachane nae kwanza mwaka mmoja hawawezi wakawa wamezama kiasi hicho especialy kwa mdada
 
Huyo Jamaa nae sio,anawzia watoto kupata pumu kabla hujawapata je kama hazai? mwambie kama kesha pata mwengine aende asije akachelewa
na huyo dada avute subra Mungu atampa mwenye khier na yeye sababu ndoa zinaandikwa binguni ...
 
huyo jamaa yako anamtosa mdada wa watu kiaina............... inawezekana watoto wake wasirithi
 
Huyo rafiki yako anatafuta upenyo wa kutokea tuu maana kashamchoka mwenzake na wala sio hicho kigezo
Ina maana muda wote aliokaa nae alikuwa hajajua kuwa mwenzake ana huo ugonjwa
 
Huyo rafiki yako anatafuta upenyo wa kutokea tuu maana kashamchoka mwenzake na wala sio hicho kigezo
Ina maana muda wote aliokaa nae alikuwa hajajua kuwa mwenzake ana huo ugonjwa

Mkuu unaishi Hungumalwa kweli?Tutafutane...
 
nadhani huyo jamaa anatakiwa aende na mdada wakapate ushauri jinsi gani ya kuzuia hilo tatizo
 
Mapenzi ya dhati hayakuwepo hapo..... Kimsingi hata km wangeoana ending isingekuwa nzuri..... Bora wameachana mapema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom