Alwaz
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 6,835
- 10,381
Binafsi sikukupigia wewe kura yangu ingawaje niliwapigia kura wagombea wa chama chako ngazi nyengine.
Kampeni zako na za wapinzani wako ndizo zilizoniongoza kufanya hivyo.
Najua machungu uliyonayo ni makubwa sana.Leo sina nia mbaya na wewe na nataraji mashabiki wako hawatonielewa vibaya.Ndio maana nakuletea salamu kutoka ndani ya moyo wangu.
Sababu inayonifanya nifikishe salamu zangu za dhati kwako ni kwa vile mimi ni mpenzi wa haki na nimegundua kuwa katika huu uchaguzi na nyengine kote hakuna haki.Napendelea mshindi lazima atokane na ukweli wa kura na matokeo ya kampeni pekee na si vyenginevyo.
Kwa mwaka huu yawezekana kura ulizopata sio aslimia kama ilivyotangazwa kutokana na sababu zozote zile.Hata hivyo uwe na uhakika kwamba hata haki kikamilifu ingetendeka basi uwezekano wa wewe kwamba ungekuwa mshindi ni mdogo.
Kubwa ambalo napenda ulielewe ni kuwa hizi chaguzi zina mikono kutoka mbali.Mshindi huamuliwa miongoni mwa wagombea kulingana na maslahi ya hiyo mikono.Yawezekana kutokana na uchanga wako katika siasa hukuyajua haya.
Kwa juhudi yako pekee na wafuasi wako haiwezekani kubadili hii hali.Hivyo baada ya huu uchaguzi unachokisema kiwe ni kwa kupima sana.
Nakushauri uwe mvumilivu na jifunze mengi kutoka kwa mgombea mwenzako;Seif Shariff Hamad.Ikiwezekana safiri ukutane naye.