Ushauri kwa continental decoder HD fanyeni hivi mteke soko

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Kwa sasa hivi decoder yenu ndo decoder mtu anamudu kununua kwa bei ya chini.
Ila mnaweza mkafanikiwa sana ila mzingatie mambo yafuatayo muweze kuliteka soko hapa bongo;-
Anzisheni customer care wa mtandaoni kama walivyo wenzenu startimes, Kiukweli nyie page yenu ya fb ni kama imebuma wateja wanapata tabu hawana kimbilio page yenu hamjaapdate kwa miaka mingi hakuna hata customer care halafu mnadhani mtateka soko sahau
2.Mkipigiwa simu muache majibu ya dharau unakuta customer care anapokea halafu anajibu km utadhani yeye ni mke wa diallo haya muyaache.
3.Vifurushi vyenu havieleweki; Kuna kifurushi kimoja tu kwa mwezi yaani 12000 vingine ni vya wiki na siku
Mnashindwaje kuweka vifurushi vya 4000, 5000, 6000, 7000, 8000 na 10000?
Yaani mavifurushi vyenu ni vya hovyo mno jirekebisheni mkiweza hapa mtateka soko kama startimes walivyo na cha nyota.
Ubunifu wa channel uwepo: Muache kurudia vipindi halafu hizo channel hazina hata studio ni cd tu mnaweka mnazirudia kwa miaka 3 hizo star movie, star bunge, star sinema, star tollywood, star kid, star culture n,k maana ni nyingi ziboresheni kama startime walivyo na channel star swahili bollywood ambazo ni nzuri
Boresheni vifurushi maana ukinunua kifurushi channel wanakufungulia baada ya wiki huu ni upuuzi badilikeni kuwen fasta km startimes
Boreshen mitambo na muache kuhama hama satelite mara kubadili frequency muwe na msimamo samahani zenu zilituchosha
Ni hayo tu
 
Ni kweli mkuu hawa jamaa wanaboa kweli star movie kila siku yale yale tu dah, najuta kununua king'amuzi chao aisee.
 
Back
Top Bottom