Kabla ya ushauri wangu kwa chama langu pendwa. Napenda kukipongeza sana chama hiki makini na madhubuti katika nchi yetu. Ni chama ambacho kimeifanya nchi yetu kujivunia uhuru na mapinduzi kwa kumpa heshima mtu mweusi ndani na nje ya Tanzania.
Nchi yetu ni imara sana na itaendelea kuwa imara zaidi pamoja na kujitokeza baadhi ya watu wasiopenda kujithamini na kupenda kujidharau hata pale panapokuwa na mafanikio ndani ya nchi yao. Watu wa namna hii ni wa kudharau na kupuuza kwani binadamu hatufanani na ndio maana huwa kuna vichaa na timamu.
Natoa ushauri kwa chama changu pendwa chini ya jemedari wetu John Pombe Magufuli (BULLDOZER) kwamba; Ni vyema mheshimiwa M/kiti wetu anapokuwa anatoa tathmini ya utendaji kazi wa chama kwa wajumbe wa mkutano mkuu taifa hasa pale anapozungumzia mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya chama kwa kuainisha mafanikio ni vyema iwe kwa pande zote mbili za muungano (Bara na Visiwani) badala ya kujikita sana upande wa bara.
Hii itasaidia kuondoa malalamiko ya kuonyesha chama kinatimiza ilani yake upande mmoja wa muungano badala ya nchi nzima.
Nawakaribisha wana CCM na wasio wana CCM kuchangia mawazo kuboresha na si vingenevyo.