Ushauri kwa CHADEMA

Eddo Sambai

JF-Expert Member
Aug 1, 2013
2,344
1,771
Kabla ya yote napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu mweza wa yote kwa kutujalia kuiona siku ya leo, Pili wanajamii Forums wote watakaosoma post hii na kuiboresha zaidi bila kuwasahau wale watakaoikosoa.

Mimi binafsi napenda kushauri uongozi wote wa Chama Cha Demokrasia ( CHADEMA ) kuwa kipindi hiki ndio muda muafaka kwa Chadema kujijenga na kujiakikishia kujiakikishia kuchukua dola 2015. Kama inavyofaamika kuwa ni bora kuwa na jeshi la watu 2 kuliko jeshi la waasi na wasaliti 1,000.

Pia napenda kuipongeza kamati kuu ya Chadema kwa maamuzi waliyo yachukuwa juu ya wasaliti wa Chama. Pia nawashauri wazidi kuchukuwa atua zaidi za kinizamu juu ya wasaliti hao na itakuwa ni jambo la afya kwa chama kama hao wasaliti watafukuzwa kabisa uanachama wao.

Hio itakuwa ni jambo litakalowafanya viongozi wengine wasije kuingia kwenye tamaa za ajabuajabu na pia itawafanya watanzania wengi kuamini/kujua kuwa Chadema ni chama sahii na hakina mdhaa ata kidogo.

Zaidi ya yote ni kwamba wasaliti hao walikwisha sambaza sumu ya Usaliti ndani ya chama na hivyo njia pekee ya kutoa sumu hiyo ni kuwafukuza uanachama na hapo ndipo tutaona sumu iliyosambazwa ikitoka na kuwafuata wasaliti na hapo tutapata wanachadema halisi na sio mchanganyiko wa pumba na mchele.

Mwisho napenda kukushukuru sana wewe uliyesoma mawazo yangu na nitashukuru sana kama nitapata mchango wa mawazo yako.

TAHADHARI:
Mjadala juu ya ZZK VS chadema ulisha fungwa, hivyo tujikite juu ya nini Chadema wanapaswa kukifanya hasa kipindi hiki.
 
Asante Mkuu ya Kaya kwa mawazo yako.
Mimi nitapingana na wewe kidoko katika hatua ya pili unayotaka ichukuliwe na Chadema. Ni kweli kabisa kila mtu anafahamu kuwa chadema ni chama cha watu wote ( wenye dini na wasuio na dini, madhehebu yote, makabila yote, masikini na matajiri, ) na kweakweli wasaliti ni watu wanaotoka katika jamii nilizoorezesha kabla. hivyo mimi naona adhabu ZZK aliyopewa inamstaili na inamtosha.
 
ninachojua hawatamfukuza kwa sababu atapewa adhabu ya kutokugombea mpaka uchaguzi upite. siunajua lazima wahafidhina washinde.
we all know the conflicts we see is due to power.
 
Profesa Baregu aitahadharisha CHADEMA kuhusu kumtimua Zitto
Post Fri Nov 29, 2013 9:36 am

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.

"Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama," Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.

Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.

Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.

"Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani."
Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.

Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.

"Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho," alisema na kuongeza:

"Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana."

Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.

"Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi.

Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake."
 
KATIBU TANGA AHOJI, ALAANI ZITTO KUVULIWA UONGOZI

Baadhi ya viongozi wa Chadema mkoa wa Tanga, wamehoji maamuzi ya kumvua madaraka Zitto na wenzake.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Tanga, Harid Rashid, alisema jana kuwa hakubaliani na maamuzi hayo.

Rashid ambaye aliongozana na mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Hussein Baruti na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Tanga, Mohamed Aufi, alisema kuwavua nyadhifa viongozi hao ni uonevu kwa kuwa hawaoni kosa walilolifanya.

Alisema kuwa Kamati Kuu ilikuwa na njia nyingi za kulipatia ufumbuzi jambo hilo badala ya kuwavua uongozi.

Alisema kuwa wameamua kuwa wazi kuhusiana na tukio hilo kutokana na ukweli kuwa Zitto ni mtu muhimu katika uongozi wa chama.
 
CHADEMA DAYOSISI YA KASKAZINI hamuwezi kuhodhi chama na kufanya watu wote misukule. DEMOKRASIA KWANZA!
 
NGUMI ZAPIGWA MBEYA

Kundi la vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Zitto jijini Mbeya wanadaiwa kurushiana makonde na viongozi wa Chadema katika ofisi ya chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini kwa madai ya kutofautiana msimamo kuhusiana na uamuzi wa Kamati Kuu.

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, David Mwambigija maarufu kwa jina la ‘Mzee wa Upako', alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo juzi mchana.
Mwambigija alisema kuwa chanzo cha vurugu hizo ni vijana zaidi ya 18 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Zitto kuanza kufanya vikao vya siri mjini Mbeya kwa nia ya KUPINGA MAAMUZI YA KAMATI KUU.

Alisema uongozi wa chama ngazi ya wilaya ulipopata taarifa hizo alizodai kuwa ni za kiintelijensia na kuwa yeye (Mwambigija) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya chama hicho wilaya, aliamua kuaandikia barua ya kuwaita ofisini kwa lengo la kuwahoji.

Alisema vijana hao walipofika ofisini kwake huku wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa tayari wameketi kwa ajili ya kuwahoji, waliingia ndani ya ofisi na kulazimisha wahojiwe kwa pamoja badala ya kuhojiwa mmoja mmoja.

Alisema walipotakiwa watoke nje ili kila mmoja ahojiwe kwa wakati wake, waligona na kukataa kutoka ofisini na ndipo yeye kama Mwenyekiti alipoamuru kikosi cha ulinzi wa chama hicho maarufu kwa jina la Red Bridged kuwatoa nje kwa nguvu na ndipo vurugu hizo zilipoanza.

"Ni kweli kumetokea vurugu kubwa ofisini kwetu wakati kikao cha kamati ya utendaji kikihitaji kuwahoji vijana wanaoendesha vikao vya siri kutaka kukihujumu chama kutokana na uamuzi wa Kamati Kuu kumvua Zitto madaraka, tumepata taarifa hizi kwa njia zetu za kiintelijensia kuwa vijana hawa wapo kwenye kundi la Zitto," alisema Mwambigija.

Hata hivyo, Mwambigija alipotakiwa na gazeti hili kuonyesha uthibitisho juu ya tuhuma dhidi ya vijana hao, alisema kuwa ushahidi bado ni siri kwa vile wametumia njia zao za kiintelijensia kubaini mtandao wa vijana hao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala ambaye ni mmoja wa vijana walioitwa kuhojiwa na kamati ya utendaji alikanusha madai hayo na kusema kuwa vurugu hizo hazikuwa na uhusiano hata kidogo na sakata la Zitto kuvuliwa madaraka.

Alisema chanzo cha vurugu hizo ni Kamati hiyo kumuita na kutaka kumuhoji kinyume cha katiba ya Chadema yeye (Kasambala) ambaye ni kiongozi wa mkoa, hivyo hawezi kuhojiwa wala kuwajibishwa na kamati hiyo ambayo ni ngazi ya wilaya.

Alisema kuwa Katiba ya Chadema inaeleza wazi kuwa kingozi wa mkoa mamlaka yake ya nidhamu ni Kamati Kuu ya Chadema Taifa, hivyo kitendo cha ngazi ya wilaya kumuita na kutaka kumuhoji ni ukiukwaji wa Katiba.

"Mimi baada ya kupata barua ya kuitwa na Kamati hiyo ikinieleza kuwa nina tuhuma ambazo hazikuandikwa kwenye barua waliyoniletea, nilikwenda ofisini ili nipewe tuhuma zangu kwa maandishi kama ambavyo Katiba inaelekeza, lakini nikashangaa eti wanataka wanihoji, nikakataa walipotaka kunishinikiza vijana wakawajia juu wakipinga nisidhalilishwe na ndipo vurugu zile zilipoanza," alisema Kasambala.
 
kushauri chadema ni kumshauri shetani ambaye amezoea kuishi kwa kufanya maovu haiwezekani arudi kuungana na mungu hata kidogo chadema kinalaana ya mungu walishafanya dhambi kwa mungu na duniania kwa wanadamu.
 
Kabla ya yote napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu mweza wa yote kwa kutujalia kuiona siku ya leo, Pili wanajamii Forums wote watakaosoma post hii na kuiboresha zaidi bila kuwasahau wale watakaoikosoa.

Mimi binafsi napenda kushauri uongozi wote wa Chama Cha Demokrasia ( CHADEMA ) kuwa kipindi hiki ndio muda muafaka kwa Chadema kujijenga na kujiakikishia kujiakikishia kuchukua dola 2015. Kama inavyofaamika kuwa ni bora kuwa na jeshi la watu 2 kuliko jeshi la waasi na wasaliti 1,000.

Pia napenda kuipongeza kamati kuu ya Chadema kwa maamuzi waliyo yachukuwa juu ya wasaliti wa Chama. Pia nawashauri wazidi kuchukuwa atua zaidi za kinizamu juu ya wasaliti hao na itakuwa ni jambo la afya kwa chama kama hao wasaliti watafukuzwa kabisa uanachama wao.

Hio itakuwa ni jambo litakalowafanya viongozi wengine wasije kuingia kwenye tamaa za ajabuajabu na pia itawafanya watanzania wengi kuamini/kujua kuwa Chadema ni chama sahii na hakina mdhaa ata kidogo.

Zaidi ya yote ni kwamba wasaliti hao walikwisha sambaza sumu ya Usaliti ndani ya chama na hivyo njia pekee ya kutoa sumu hiyo ni kuwafukuza uanachama na hapo ndipo tutaona sumu iliyosambazwa ikitoka na kuwafuata wasaliti na hapo tutapata wanachadema halisi na sio mchanganyiko wa pumba na mchele.

Mwisho napenda kukushukuru sana wewe uliyesoma mawazo yangu na nitashukuru sana kama nitapata mchango wa mawazo yako.

TAHADHARI:
Mjadala juu ya ZZK VS chadema ulisha fungwa, hivyo tujikite juu ya nini Chadema wanapaswa kukifanya hasa kipindi hiki.

Viroba ukichanganya na WANZUKI unapata pumba kama zako hapa
 
kushauri chadema ni kumshauri shetani ambaye amezoea kuishi kwa kufanya maovu haiwezekani arudi kuungana na mungu hata kidogo chadema kinalaana ya mungu walishafanya dhambi kwa mungu na duniania kwa wanadamu.

damu ya mussa tesha inawatesa, laana ya kutaka kumlisha denis msaki sumu inawatafuna na laana ya kutaka kumlisha zitto sumu aliyokuwa nayo ben mida ieght ambayo ilidondoka bar. chagadema ni janga la kitaifa
 
Zitto asababisha ngumi kurushwa

Na Waandishi wetu

28th November 2013

Vijana wachapana wakidhibitiana

Uamuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kuwavua nafasi za uongozi vigogo wake watatu akiwamo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, umepokelewa vibaya na wafuasi wao ambao wameamua kupigana ngumi.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alivuliwa nyadhifa zake sambamba na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Mkumbo Kitila na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Kamati Kuu ya chama hicho ilichukua hatua hiyo Ijumaa iliyopita, baada ya kubaini waraka wa usaliti waliouandaa ukiibua tuhuma mbalimbali dhidi ya chama na viongozi wake ngazi ya taifa.
 
Back
Top Bottom