Tume ya Uchaguzi inayo orodha iliyopendekezwa na CHADEMA tangu 2010. Dr Slaa atuambie kama anao uwezo wa kuibadili sasa.
Majimboni nako kungekuwa na utaratibu kama huu au unaofanana na huu kungeokolewa pesa nyingi za walipakodi wa NCHI hii. Kwa mfano kule Arumeru Mashariki sasa ambako Mbunge wao amefariki, Tume ingemtangaza yule aliyemfuatia kwa kura nyingi kama anazo sifa bado. Akina Kafulila na Hamad waliovuliwa UANACHAMA nao nafasi zao zingechukuliwa na wagombea waliofuata kwa kura nyingi. Pengine hata kutimuana kungepungua sana.Wildard,
asante kwa swali.
1. Majina yalipelekwa kwa Mujibu wa Sheria ya Uchaguzi mwezi mmoja kabla ya uchaguzi, yaani 30.09. 2010. Kwa mujibu wa sheria inapotokea nafasi wazi Tume ikiisha kujulishwa na Spika, inatangaza jina la mtu anayefuata kwenye listi hiyo.
2. Kama mtakumbuka Chadema iliwasilisha majina hayo baada ya kuaandaliwa na Kamati ndogo ya Kamati Kuu kwa misingi ya vigezo maalum vilivyoidhinishwa na Kamati Kuu.
3. Tume inaweza kumwandikia Katibu Mkuu kumjulisha kuwa kwenye Listi yao anayefuata ni fulani na kutaka Katibu Mkuu athibitishe kama mhusika huyo bado anayosifa ya kuwa mbunge au la, mathalan kama bado ni mfuasi wa chama au amehama chama, au chama kwa sababu zingine kimemvua uanachama. Baada ya ya kupata uthibitisho huo huo Tume itaeendelea na Taratibu za kumtangaza mrithi wa kiti husika.. Iwapo anayefuata kwenye listi atakuwa amepoteza sifa, jina lake litafutwa kwenye listi listi na Tume na atatangazwa anayefuata. Huu ndio utaratibu wa kuwapata wabunge wa viti maalum katika kipindi chote hadi uchaguzi ujao.
Kwa vile pacha wa marehemu alikuwa akimsaidia marehemu katika kazi nyingi za kibunge na kisiasa,na tumeona marehemu alikuwa na mvuto mkubwa kwenye maisha ya kijamii na kisiasa- pacha wa marehemu ambaye amefanyakazi kama mfuasi wa marehemu arithi mikoba