Ushauri kwa CHADEMA na CD zilizochuja!


H

haki na usawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
476
Likes
7
Points
35
H

haki na usawa

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
476 7 35
Hiv chadema kuna nin? Mbona mengi yanazungumzwa na mengi hayana majibu ya kuwambia umma uliyo nyuma yenu?
Mfano:1 Mwasema CD ya ukabila, dini,ukanda na upendeleo imechuja je kweli imechuja? Maana lisemwalo lipo kama halipo linakuja na hili mwatakiwa mlitizame kwa umakini maana ni mwanzo wa chama kuvurugika! Pia kusema imechuja kama kuna ukweli mwajidanganya maana ukweli na uongo haukai pamoja! Cha msingi chukueni hatua kuonesha kuwa ni chama kinachozingatia misingi ya taifa na si kikabila!
Mfano:2 Uongozi wa Mwenyekiti Inaonesha mweyekiti anafanya kazi zingine zisizo zake maana inaonesha kuwa katika manunuzi anaamua tu bila kushirikisha watu na ananunua anachoona kinafaa kwa na kwa kuboresha chama ila ca msingi waweza kuwa unania nzuri ila bila taratibu ni uongo ambao wanaokuzunguka hawana uhakika ni namna gani utakuwa mkweli ndo maana katika tasisi kuna bodi ya ununuzi. Cha msingi ni kuchukua hatua ya kuboresha na si kila kinachosemwa na waliondolewa hakiwafai kwa uhai wa chama chenu na ndoto za demokrasia!
Mfano:3 Madeni baada ya Uchaguzi Kama mwenyekiti anaamua ni nini kifanyike pekee yake na mwisho hakuna mwanachama anayejua gharama halisi ya kile kinachodaiwa na hakuna mamlaka za cha chama juu ya uridhiaji wa matumizi ya hizo pesa basi ndoto kuwa na demokrasia. Maana wnachama hawajui wanadaiwa nini na nani na kwanin? Maana vikao vya chama ndo vinaridhia matumizi ya pesa yake kwa kuzingatia uwezo wake maana uendelezaj wa sera hii ni ukiukwaji wa ushikishwaji wa maamuzi katika chama mfano rejea kauli ya Chacha Wangwe, Dr. Kitila na sasa haijulikani ni nani ataongea tena baada ya uchaguzi wa awamu ya tano? Ni vizuri matumizi yakaridhiwa na wengi ili kuondoa lawama na zisizo na msingi maana kama mna lengo la kuboresha basi zingatieni ushauri wa wakosoaji!
Mfano:3 Posho ya ubunge Kama kweli chama mlikaa na mkaamua kuwa kwenu posho ni haramu kuchua tekelezeni imani yenu kama mtakuwa hamuamini hata kwa kile mlichoandika nyie bado ni ndoto kutekeleza matakwa ya umma ulo nyuma yenu! Kama hamkulazimishwa kukataa posho, hamkulazimishwa kuandika katika katiba yenu basi mna changamoto maana kama katiba yenu hamuiheshimu je mtaja hesimu ya nchi? Kama mliona kuna dosari ni bora mkarekebisha ili walo nyuma yenu wajue kweli mnasimamia mnachokisema! Bila kufanya hivyo ni kujidanganya kuwa nyie wasimamizi wazuri kwa yale manayaongea jukwaani!
Mfano 4 Maamuzi ya CC Mengi yanazungumzwa juu ya maamuzi kuanzia kwa kina Kabour, Chacha na sasa Zito na Kitila maana ukweli utabaki kuwa ukweli na uongo utabaki kuwa uongo! Kama kamati ilikurupuka katika maamuzi ni bora mkawa wazi maana kama mtaendelea kwa staili hii ya ukurupukaji basi ikija tokea mkachukua nchi mtaiingiza nchi katika mgogoro mkubwa huenda na majirani zake au nchi itayokuwa na mtazamo tofauti na wa chama chenu. Na hili lazima muwe wazi maana si kwa kuwa wanafiki/wasamaria wema wengi wanawaunga mkono kwa maamuzi yenu juu ya kuthibiti nidhamu za wanachama wenu lakini kama mlikurupuka bado ukweli uko kwenu maana aibu yenu na fahari yenu pia kama kweli mlizingatia au la kwa vipengele vinavyoainishwa na walioitwa wasaliti!
Mfano: 5 Maamuzi ya nidhamu Mengi yanaongelewa juu ya nidhamu kuchukuliwa kwa baadhi kwa uharaka na wengine wakiachwa bila kushughulikwa na kama mwafanya hivi ni makosa maana kwa sasa watu ni waelewa juu ya ubaya na uzuri wa kitu alichoongea mwanachama juu ya chama chake au kiongozi wa chama chake au juu ya mtu yeyote anayehusika kwa tatizo analotuhumiwa. Kama kauli za viongozi,wabunge,wanachama na wengine hazifumbuliwa kwa haki basi ni kujidanganya maana ukiwa muwazi kuwa muwazi na ukiamua unafiki basi fanya kazi ya unafiki kweli mfano muswada ni mzuri wa marekebisho ya katiba wanafiki walishangilia japo nyoyoni mwao wanajua ni uongo lakini kweli ikajitenga na uongo ukathihiri maana mkuu aliusain kwa mbwembwe mbele ya vyombo vya habari lakin ukweli wa hoja ukafanya urudishwe kufanyiwa marekebisho. Kwa hiyo nanyi kuwa wakweli wa nidhamu msiwe na upendeleo ambao hata mtoto mdogo ataujua maana kizazi hiki si miaka hiyo maana ukweli na uongo unajitenga mfano wa hapo juu kwenu huwei kusema kuwa ugawaji wa madaraka ni wa haki ila nasema ya dhahiri yako vifuani mwenu!
Mfano: 6 Wasaliti kila mwenye mtizamo hasi na chama Kila mwenye mtazamo tofauti na chama basi aitwe msaliti au anatumiwa na chama tawala. Kama kasumba hii ikiendelea basi mtamalizana wenyewe kwa wenyewe maana hakuna binadamu anayetosheka kwa pesa au madaraka maana tamaa imo ndani ya mioyo ya binadamu. Cha msingi angalieni je tofauti zenu zina faida au zina matatizo kama zina faida basi fanyieni kazi ili kuboresha chama chenu bila hivyo mtatengeneza makundi ambayo mengi yatakuwa na matazamo tofauti na mengine yataanza kwa kusaka ulaji bila kuboresha chama.
Mfano: 7 Waraka ulowatoa akina Zito na Kitila Inaonekana waraka uliotolewa ni feki na je kama chama kinafanya maamuzi magumu na kisha kupeleka hoja feki kwa wananchi je mtaelewekaje mbele ya macho ya wananchi. Kama ilitokea bahati mbaya basi semeni maana kulumbana waraka sahihi wengine si sahihi mnaacha watu njia panda na watabaki kujiuliza juu ya maamuzi yenu. Cha msingi zingatieni ukweli maana mkiumbuka kuwa ni waongo hamtaaminika tena kwa vile haya ni maamuzi ni magumu na yanahitaji ukweli na uadilifu ili jamii inayofuatilia iamini mnachoemanisha.
Mfano: 8 Kikosi cha usalama/Siri za chama Mengi yamezungumzwa juu ya kikosi hiki kikinasibishwa kwa mwenyekiti wa chama. Kama ni kwa ajili ya chama basi teueni watu kwa sifa zao na pia iwe ni kweli kwa ajili ya chama ila si kwa kulinda maslahi ya waliopo madarakani maana kama itakuwa hauna muda mrefu mtaumizana wenyewe kwa wenyewe. Bora kikosi kiwe cha chama badala ya kuwa cha mwenyekiti na kuondoa wapinzani wake/wanaotofautiana nao kimtazamo maana kufanya hivyo utawala ho huwa haudumu kwasababu siku wakikosana basi siri zote nje na mabaya yote nje na hilo linakuwa faida kwa chama kingine huku nyie mkibaki kujisafisha.
Mfano: 9 Uteuzi wa viti maalum Na hili limezungumzwa na hadi CC inaonekana ililikemea na kama ni kweli kuna upendeleo basi kuna changamoto maana kama ikithibitika kuwa kuna upendeleo huo basi mtadharaulika katika jamii. Si vibaya kupata mtu wako ila si vizuri wateule wote/wengi wawe wanakuhusu. Na hili lilimuumiza sana Lisu maana alipobanwa juu ya dada alikosa jibu baada ya usema chama tawala kina upendeleo. Cha msingi kuwa na vigezo ili aliyetimiza apate na si kuchukuana kindugu,kikabila na kikanda.
Mfano: 10 Matumizi ya pesa Inaonekana matumizi ya pesa kuptia chama hayafai kuulizwa na ikitokea muulizaji kahoji basi huitwa msaliti rejea kauli ya Chacha na sasa baada ya kina Zito. Kama masuala ya pesa yakawa ni kosa mtu kuhoji na hata kujua zinaendaje bas ni matatizo. Kama mtu yeyote akiuliza mapato na matumizi ni mbaya ndani ya chama kuna mchwa na huo mchwa unajilinda kwa maamuzi ya wanaouliza! Ukweli haujifichi na ipo siku madudu/matumizi mabaya ya ruzuku yataja julikana je wanaotetea uozo wataweka wapi sura zao? Kama mlikula basi acheni na tumieni kuimarisha chama ili mpate kula zaidi maana ndo ruzuku itangezeka. Kukimbila kuzuia watu uhoji ni vibaya maana hakuna mkamilfu katika dunia na hakuna asiye na tamaa ya kutengenesha maisha yake na ya familia yake.
Mwisho ni ushauri tu ulotolewa na si kujibizana kwa matusi na kejeli.Tambua kuwa kifo ni haki pia jua hakuna atakaye kufa kwa ajili ya mwenzake ili aendelee kuishi la msingi ni kufanya mema ukumbukwe milele daima!
 
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
2,861
Likes
1,466
Points
280
spencer

spencer

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
2,861 1,466 280
Unashauri umeombwa ushauri?
Wewe ni MwanaCCM Magamba yamekushinda, subiri uone kazi ya CDM.

Tushawashtukia, na sasa hamna jingine.
Kwani CCM ina wenyeti wangapi miaka 50 ya UHURU siyo wanne.
Mnararama nini,subirini tuwanyooshe vibaraka wenu:frusty:
 
M

m4cjb

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2012
Messages
6,900
Likes
356
Points
180
Age
34
M

m4cjb

JF-Expert Member
Joined Jul 23, 2012
6,900 356 180
Huyu mbulura katumwa kupima kina cha maji? kawaambie wasaliti na waliowatuma kuwa siku zao zinahesabika CDM!
 
K

kigoda

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Messages
1,782
Likes
8
Points
135
K

kigoda

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2012
1,782 8 135
Mda mwingine ukivimbiwa ni bora ukalale.
 
FYATU

FYATU

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2011
Messages
5,267
Likes
3,453
Points
280
FYATU

FYATU

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2011
5,267 3,453 280
Hapo kwenye kuhoji matumizi ndio kwenye mtiti.

Inashangaza mtu anayejinadi kuifahamu sheria vilivyo kama Tundu Lisu anakuwa kibaraka wa watu na kupewa rushwa ya kiti maalum kwa dada yake....na siku akipata UJASIRI wa kuhoji matumizi au mienendo ya wakubwa zake ndipo atakapoonekana hafai.

Ukitaka kusavaivu kwenye huu mradi a.k.a Saccos unatakiwa uwe kama kina Mnyika, Mdee, Msigwa, Lema.....ukiwa nje bweka kadri unavyoweza...lakini ukirudi ndani ni kuchezesha mkia tu kwa bwana wakubwa.
 

Forum statistics

Threads 1,250,303
Members 481,303
Posts 29,727,544