Ushauri kwa CHADEMA: Karata ya mwisho mliyobaki nayo ni katiba mpya

fenisher

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
287
500
Kutokana na hali ya kisiasa ilivyo sasa na chama chenu kupungua kasi kutokana na sababu mbalimbali zinazosababisha wananchi kukosa imani na nyinyi mmojammoja. Napenda kutoa pendekezo ambalo linaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine.

[HASHTAG]#KATIBA[/HASHTAG]
Hii ni karata ya mwisho ambayo mmebakiwa nayo katika kurudisha imani kwa wananchi, mwananchi wa sasa hata umweleze akapige kura kwa sasa hawezi kukuelewa ndio maana katika uchaguzi madiwani watu walikua wachache.

Kama hamtoanza kudai katiba mpya basi 2020 hakuna atakayeenda kupiga kura na hivyo swala la mabadiliko katika nchi litabaki kua historia. Kama hadi leo hamjaanza kudai katiba mpya ambayo pia ingesaidia kudai tume huru basi mnaruhusu CCM kuongoza milele.

Kama mnashindwa kupigania kitu kitachokuwezesha kupata haki yenu basi hapo hakutakua na haja ya kupigania haki hiyo. Na kama mkishindwa kupigania katiba mpya basi mngeshauri vyama vya upinzani kufutwa na kuepusha chuki na makundi baina ya wananchi wenyewe. Kama ikipatikana katiba mpya hapo mtaona wananchi watakua wengi katika uchaguzi wa 2020 bila ya hivyo harakati mnazoendeleza zitakua kama kuimbia maiti ili ifurahi.

NB; Mi si mfuasi wa chama chochote na wewe kama ni CHADEMA unaweza ongezea ushauri katika kusaidia kukua kwa chama chako na kama wewe ni CCM pia unaeza toa ushauri kwa kuwa upinzani ukiwa na nguvu ndio chama chako kitaleta maendeleo zaidi ili kuwapoteza upinzani. WEKA UCHAMA PEMBENI NA SIMAMA KAMA MWANANCHI alafu toa ushauri wako.

Nawasilisha.

Fenisher
 

Naminipo

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
506
1,000
Kutokana na hali ya kisiasa ilivyo sasa na chama chenu kupungua kasi kutokana na sababu mbalmbali zinazosababisha wananchi kukosa imani na nyinyi mojamoja. Napenda kutoa pendekezo ambalo linaweza kusaidia kwa namna moja ama nyingine....

[HASHTAG]#KATIBA[/HASHTAG]
Hii ni karata ya mwisho ambayo mmebakiwa nayo katika kurudisha imani kwa wananchi, mwananchi wa sasa hata umweleze akapige kura kwa sasa hawezi kukuelewa ndio maana katika uchaguzi madiwani watu walikua wachache. Kama hamtoanza kudai katiba mpya basi 2020 hakuna atakayeenda kupiga kura na hivyo swala la mabadiliko katika nchi litabaki kua historia. Kama hadi leo hamjaanza kudai katiba mpya ambayo pia ingesaidia kudai tume huru basi mnaruhusu ccm kuongoza milele. Kama mnashindwa kupigania kitu kitachokuwezesha kupata haki yenu basi hapo hakutakua na haja ya kupigania haki hiyo. Na kama mkishindwa kupigania katiba mpya basi mngeshauri vyama vya upinzani kufutwa na kuepusha chuki na makundi baina ya wananchi wenyewe. Kama ikipatikana katiba mpya hapo mtaona wananchi watakua wengi katika uchaguzi wa 2020 bila ya hivyo harakati mnazoendeleza zitakua kama kuimbia maiti ili ifurahi.

NB; Mi si mfuasi wa chama chochote na wewe kama ni cdm unaeza ongezea ushauri katika kusaidia kukua kwa chama chako na kama wew ni ccm pia unaeza toa ushauri kwa kuwa upinzani ukiwa na nguvu ndio chama chako kitaleta maendeleo zaidi ili kuwapoteza upinzani. WEKA UCHAMA PEMBENI NA SIMAMA KAMA MWANANCHI afu toa ushauri wako.

Nawasilisha..
Fenisher.....
Siamini kama kunaweza tokea katiba mpya ya wananchi kwa mazingira ya sasa ya kisiasa na uelewa wa wananchi tulio wengi. Labda tu kama vingefutwa vyote, katik kipindi cha mpito iundwe katiba ya wananchi. Hili ni gumu pia hivyo tuvumilie tu, hakuna namna kama ipo niambiwe!
 

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Mar 30, 2014
9,449
2,000
JK aliwaambia..ameanzisha mchakato, mkiuchezea shauriyenu...yeye atakuwa amepumzika Msoga wakati nyie mko bize mnalialia
 

kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,559
2,000
Chadema hawatoaminika tena haswa baada ya kuahirisha Ukuta na kuleta katafunua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom