KaziIendelee
JF-Expert Member
- Oct 30, 2013
- 327
- 229
Awali ya yote nampongeza sana Mhe. Rais wetu, mpendwa wetu Mama SAMIA SULUHU HASSANI kwa kazi nzuri anayoifanya na wasaidizi wake. Pia nampongeza sana aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi mstaafu kwa kazi kubwa aliyoifanya na nampongeza sana Mkuu mpya mteule wa majeshi ya ulinzi kwa uteuzi wake.
Baada ya utangulizi wangu huo, naomba nijikite katika kushauri kwa Serikali, Mkuu mpya wa majeshi na wasaidizi wake kuhusu namna ipi bora ya uendeshaji wa shule za sekondari za majeshi.
1. Nashauri waalimu wote ambao sio askari wanaofanya kazi katika shule hizo waajiriwe na serikali ili kulipunguzia jeshi gharama za uendeshaji na ikifanyika hivyo hata ada zinaweza kushuka na ikawa msaada kwa watoto wengi wa kitanzania kupata taaluma na kulelewa kinidhamu kuwa wazalendo wa Taifa letu.
2. Non teaching staff kama wapishi waendelee kulipwa na jeshi kulingana na makubaliano yao.
3. Pia kuwepo na mchanganyiko katika nafasi za kiutawala kwa maana ya raia na askari ili kuleteta chemistry nzuri ya kiutendaji kuepuka uendeshaji wa taasisi ya kitaalumu kwa imla.
Huo ndiyo ushauri wangu.
Kazi Iendelee.