Ushauri kwa ccm: No way forward,,, jipangeni kutokea bench | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa ccm: No way forward,,, jipangeni kutokea bench

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tuko, Oct 7, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Naandika post hii bila chembe ya ushabiki wa chama chochote cha siasa (ingawa mimi ni mshabiki wa CHADEMA). Lengo langu kubwa ni kutoa maoni yangu juu ya chama hiki kikubwa; CCM, ambacho kwa namna moja au nyingine, kinatuhusu (hadi sasa kinatutawala).

  CCM imetawala nchi hii kwa miongo kadhaa sasa, na bila kuwa biased, wamefanya mengi kwa kweli. japo kwa uwezo wao. Napenda kuitazama CCM kama chama kilichojikusanyia wanachama viongozi, wenye sifa na uwezo mkubwa wa kuongoza. Hili linajidhihirisha kutokana na ukweli kuwa kama ukiangalia kati ya wanajamii ambao kwa namna moja au nyingine wameonekana kuwa na sifa bora za uongozi katika maeneo yasiyokuwa ya kisiasa, (katika dimensions za siasa), kama kwenye dini, mashuleni, katika taasisi za umma na binafsi, hata katika koo na familia, wengi wao, ama bado wapo, au wamewahi kuwa ndani ya CCM, nikiwazungumzia wale waliopenda kujiingiza katika siasa.

  Lakini kama ilivyo kwa taasisi yeyote yenye uongozi, chama cha siasa kina muundo wa pyramid, kwa maana kuwa hata muwe millioni nyingi, lazima kunakuwa na mmoja au wachache, wanaokuwa mbele kama viongozi. CCM nayo iko hivyo.

  Katika hali ambayo tunaiona hivi sasa, CCM imepoteza mvuto na umaarufu wake kwa Watanzania. Sina takwimu za kisayansi, hivyo simlazimishi yeyote kukubali hili, lakini, with fair mind, Mtanzania yeyote anayefuatilia siasa za Tanzania, atakubaliana nami kuwa CCM imepoteza mvuto (naamini hata mwenyekiti wa CCM taifa, ndani ya akili yake anaamini hivyo). Najua CCM kwa kufahamu hilo wanafanya kila linalowezekana kujirudisha katika mstari, na hapo ndipo mimi natoa ushauri wangu.

  Mwaka 1995, hali ya kupoteza mvuto iliyokaribia hii ya sasa ilijitokeza (kwa ushahidi wa matikeo ya kura za uchaguzi mkuu). Tukitumia kura hizo hizo (tukiamini matokeo yalikuwa halisi), tunaona CCM iliimarika mwaka 2000 na zaidi 2005. Sababu zinaweza kuwa katika angles tofauti, lakini kubwa, umahiri wa aliyekuwa mwenyekiti na rais; Mkapa (kwa mbinu za aina yeyote, negative or positive) ulichangia kwa kiasi kikubwa. Mwaka 2010, zaidi ya miaka minne baada ya kuingia mwenyekiti mwingine, tunaona umaarufu wa CCM umeporomoka.

  Binafsi, naamini bado CCM inao uwezo, tena mkubwa wa kurudisha umaarufu wake, tena kwa muda mfupi kama wakijipanga. Lakini, sioni namna yeyote ya uwezekano huo kuwepo, huku CCM ikiwa madarakani. CCM, kama ilivyo kwa chama chochote cha siasa kina wanachama wa aina mbili; wanachama wanaotetea maslahi ya chama kwa faida na maslahi ya nchi, na wanachama wanaotetea maslahi ya chama, kwa faida na maslahi yao au watu binafsi.

  Kwa bahati mbaya, kundi la maslahi binafsi, limefanikiwa kukua, na mbaya zaidi, limefumika kundi la maslahi ya nchi. Kama kuna kitu kinachowatenganisha CCM leo na watanzania, ni neno, ni msemo, ni dhana FISADI. Kwa bahati mbaya sana, sio wanachama wote, au viongozi wote, wana sifa ya UFISADI ndani ya CCM. Hii ina maana kuwa kama kutakuwa na uwezekano wa kuchambua kati ya mafisadi na si-mafisadi, bado CCM inabeba viongozi wengi sana wenye sifa nzuri, na tunaowahitaji sana katika uongozi wa nchi yetu.

  Changamoto waliyo nayo CCM kwa sasa, ni kuwaaminisha watanzania kuwa wao sio mafisadi. Naweza kuthbutu, kuapa kuwa, hakuna namna nyingine ya kufanikisha hilo, zaidi ya kuondoka chamani, wanachama wake, waliokuwa 'labeled' MAFISADI. Ni ukweli na uhalisi kuwa, hakuna namna yeyote hawa 'MAFISADI' wanweza kuondoka chamani, lazima waondolewe, na hapa ndipo pagumu. Hapa ndipo CCM, wanapolazimika kufanya uamuzi mmoja mgumu; kuachia madaraka kwanza, wakakaa bench, wakajipanga upya. Mtu unaweza kujishawishi kuwa, kama ndivyo, basi, tubaki madarakani, hadi pale tutakapoondolewa na wananchi, then tutajipanga. Ukweli ni kuwa, that will be too late to repair.

  Kwa kuwa CCM wanaoshikilia uongozi katika chama, na katika serikali, wengi wao wapo katika lile kundi la maslahi binafsi, wana-CCM na Watanzania kwa ujumla wasahau kuwa haw jamaa watakuwa tayari kuachia ngazi kirahisi, NO WAY. Watatumia mbinu zozote zile kubaki madarakani, na hapo ndipo watakapoichakaza CCM beyond repair kwani wao maslahi yao, sio CCM, bali ni wao binafsi.

  Hebu imagine, kama ninavyoimagine mimi (sio lazima iwe kweli) kuwa, kwa mbinu zozote zile CCM wabakie madarakani mwaka huu, hiki chama kitakuwaje miaka mitano ijayo?!!!!! Hata kama kitaondoka wakati huo (kama CCM haiondoki mwaka huu, lazima itaondoka 2015 - Naamini hivyo), unadhani kitakuwa katika shape gani?

  Napenda kuwaasa wanachama wa CCM wenye mapenzi mema na chama chao kwa manufaa ya nchi hii, wakubali kujipanga sasa. Hakuna nafasi ndani ya vikao vya chama, itakayowaruhusu kuwaondoa viongozi wenu wababishaji. Nafasi mliyo nayo ni hii ya kuwatumia wanachi wa Tanzania. CCM ikiondoka madarani leo, ndo itajulikana nani alikuwepo, kwa maslahi ya watanzania, na nani alikuwepo kwa maslahi binafsi. Hawa MAFISADI wanafahamu kabisa kuwa wameshachafuka, na kuwa thamani ya uanasiasa wao inabaki tu kwa sababu bado wapo madarakani, na wanaendelea kujifaidisha.

  Nina uhakika leo CCM ikitoka madarakani leo, wapo wengi sana kati yao watakaostaafu siasa. Wanaoona kuwa, katika kizazi hiki, hawasafishiki tena mbele ya Watanzania. Hakuna Namna nyingine ya hawa kuondoka, zaidi ya CCM kuondoka madarakani.

  Kwa hiyo, wanaCCM mlio na uchungu na chama chenu, na nchi yenu, kubalini kurudi benchi, mkajipange, mkachambuane, mrudi katika chati. Mna bahati ya kuwa na raslimali nyingi za mali na watu wenye uwezo wa kuongoza, lakini gari yenu inahitilafu mbaya, inaelekea kubaya, na dreva wenu na wapambe wake hawataki kugeuza, kwani bado wanafaidika na nauli za abiria. Kubalini sasa kuliharibu moja kwa moja gari, abiria wapande kwenye gari nyingine,na nyie mpate nafasi ya kurepea gari yenu.

  Kama wewe ni mwana-CCM na unakipenda chama chako, na unataka kukijenga, fanya yafuatayo

  i. usikipigie kura mwaka huu
  ii. Shawishi watu wasikipigie kura
  iii. Usikubali kushiriki mbinu zozote za kubadili matokeo ili kikipa CCM ushindi

  Kama mtakubali CCM iendelee na uongozi mwaka huu, for sure, inaelekea kupotea katika ramani ya siasa Tanzania. Mlio ndani yake ambao mna nia nzuri na nchi hii, mtapotea pia kwani by then, hamtaweza kukusanyana tena. Mtasambaa na kuishia kutangatanga katika vyama vingine, au kuanzisha vyama vidhaifu, kwani umoja wenu hautakuwepo tena.

  The string that UNITED you is broken and Things are FALLING apart. Kumbukeni wahenga wanasema, "KUANGUKA KWA MTI MKUU, WATOTO WA NDEGE HUTAWANYIKA"...
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Sikio la kufa halisikii dawa, na la kuvunda, halisikii ubani!!
   
 3. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Poor CCM... Wanatia huruma!
   
 4. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Well said. Ni uchambuzi yakinifu na uliojaa ukweli mtupu.
   
 5. c

  crusingtz Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TUKO........u gave more than a diagnosis, u prescribed the terminally ill with the curable drug. MY ADVICE TO THE PATIENT- take the Doctors order and get plenty of rest. You will be more use to the Team when your well!
   
 6. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,477
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  malaria sugu unasemaje?pengo na kadogoo tunaomba tathmini
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuu well said nimekuelewa, sana nakubaliana na wewe 100%
   
Loading...