Ushauri kwa CCM na serikali yake

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Ni ushauri wa bure kwa wanaccm,CCM na serikali yake.

Nianze kwa kusema tu kuwa,muda wa miaka 50 kutawala nchi inatosha kabisa.Sasa ni muda muafaka wa kukipa chama kingine kinachoonekana kuungwa mkono na walio wengi.kwa maana ccm haipo tena mioyoni mwa watanzania.

Haya maendeleo mnaojisifia/au mnataka kusifiwa mmeleta wakati ni wajibu wenu kufanya hivyo, yanatosha.Kwanza kujisifia kuwa mmeleta maendeleo ni dharau kwa wananchi,kwa sababu:

1.Ni wajibu wenu mfanye hivyo kwa hiari au kwa lazima kwani mnatumia kodi za wananchi from which they expect indirect returns.
2.Haiwezekani nchi kuwa kila aina ya rasilimali kama madini,misitu,ardhi yenye rutuba na maji ya kutosha,lakini tuna tatizo la njaa,madawati,umaskini,maji n.k.

3.Kilimo kimewashinda kila AWAMU mnakuja na sera mpya km KILIMO CHA KUFA NA KUPONA,KILIMO NI UTI WA MGONGO, MKURABITA,MKUKUTA NA SASA KILIMO KWANZA.ukiangalia malengo ya sera hizi yanafanana,nadiriki kusema kuwa hii imekuwa sera ya kuombea kura kwa wananchi.Hakuna jipya linalofanyika,imekuwa sera ya kuombea kura.CCM haina nia ya dhati kuondoa umaskini nchini.

4.Ukilinganisha nchi ambazo tukikuwa nazo sawa/ nyuma yetu kimaendeleo zamani,zenyewe ziko juu kuliko sisi mfano nchi ya Rwanda. Na maisha ya kwetu yanazidi kuwa magumu sijui hayo maendeleo ni kwa ajili ya mafisadi? Mbona wananchi hatuyaoni?
Watu wamewakosoa,wamewashauri wamewaonya, lakini mmeweka pamba masikioni huku mkiijiita serikali SIKIVU kama siyo UNAFIKI na DHARAU ni nini?

Tatizo kubwa la ccm na serikali yake haishauriki,kichwa ngumu. Wakati mtu anayekukosoa/ au kukushauri anakutakia mema.
Mfano,katika kampuni una wafanya kazi,lakini kuna tatizo ambalo wafanyakazi wanaliona lakini hawataki kuliripoti katika management,hilo tatizo likiwa sugu ni nini hatima ya kampuni? Bila shaka mwisho wa kampuni ni kuanguka/kuporomoka.

Sasa,Ccm msilaumu mtu,hii ni ukichwa ngumu wenu kutosikiliza shida na kero,ushauri na maoni ya wananchi.Matokeo yake mnalaumu vyama vya upinzani,wananchi kuunga mkono vyama vya upinzani siyo kuwa ni wajinga bali wako RATIONAL.

Wananchi wanajua kipi kibaya,kipi kizuri,wapi wamekosea,wapi kushauri.Lakini,wenzangu Ccm mmekuwa hamshauriki ndiyo chanzo cha wananchi kuwasaliti.

Mtatafuta mchawi,mtafanya kila aina ya baya kwa upinzani,mtazusha kila jambo baya kwa upinzani,lakini wananchi hawatawaunga mkono kamwe SINCE THEY ARE RATIONAL IN DECISION MAKING.

Wananchi wanajifunza kutokana na EXPERIENCE,mwaka 2010 kuna tuhuma nyingi zilizushwa juu ya ndoa ya Dr..Slaa,leo hii lipo wapi? Hapa wananchi wanahoji au ilikuwa ni uzushi wa CCM? Mbona hatujalisikia tena baada ya uchaguzi?

Wananchi wanajua mbinu zenu za kizushi,ndiyo maana kila baya mnalolitupia kwa wapinzani,wapinzani wanaibuka washindi. Huu ndiyo mwisho wenu.Mkifanya wananchi wanayotaka hakika mtashinda otherwise subirini kuondoka kwa AIBU ya kuzomewa kama mbwa mwizi.

USHAURI TU.
 
Ndugu huu ushauri ni mzuri sana ila nasikitika sidhani kama kuna wakukuelewa hapo sasa hivi wako busy na kufocus 2015 watatokaje, uzuri nikwamba ngonjera zao zote wananchi wameshazielewa wanawasubiria na hawataamini kitakachotokea.
 
Ushauri mzuri saana huu Mkuu na umejaa ukweli tupu.Lakini kama ulivyokwisha sema hapo awali,wametia pamba masikioni.
 
Huu ushauri unafaa kwa watu waliopigika!
Je, watanzania wamepigika?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
unawapigia mbuzi gitaa,MACCM wanachojua kung.oa kucha watu,kunyoa meno na kutoboa macho
 
Back
Top Bottom