Ushauri kwa CCM kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025

SHILLINGS

Senior Member
Oct 24, 2013
144
1,000
Ushauri kwa Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025:

1. IGP Simon Sirro aendelee kuimarisha jeshi la polisi na kuhakikisha anaendelea kutetea Chama Cha Mapinduzi,

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iendelee na utaratibu wa kukata majina ya wagombea wa vyama vya upinzani kwa kukosa sifa ya kusoma na kuandika,

3. Watendaji wote wa vijiji na kata waitwe ikulu na kupewa maagizo maalum ya kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda uchaguzi,

4. Jaji Mtungi aanze mchakato wa haraka wa kukifuta Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kabla ya uchaguzi wa mwaka 2024/2025,

5. Mahakama zihakikishe kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anakaa jela hadi kufika mwaka 2026,

6. Tume ya Taifa ya iteue TBC kuwa Chombo pekee cha kurusha matangazo ya matokeo yote ya uchaguzi wa rais. Iwe marufuku kwa chombo kingine chochote kutangaza matokeo,

7. Serikali ifungie mitandao yote ya kijamii wakati wa uchaguzi na iwe marufuku kubandika matokeo ya uchaguzi nje ya vituo vya kupigia kura,

8. Wasimamizi wa uchaguzi ihakikishe kwamba hakuna wakala yoyote wa Chama cha upinzani anatoka na nakala ya matokeo kwenye chumba cha kupigia kura.

9. Wasimamizi wa uchaguzi wahakikishe kwamba mawakala wote wa vyama vya upinzani wanaingia kwenye vyumba vya kupigia kura saa 6 mchana siku ya kupiga kura,

10. Tume ya taifa itangaze mgombea wa Chama cha Mapinduzi kimeshinda kwa kuwa kwa mujibu wa katiba ya JMT hakuna mahakama yoyote inapaswa kuhoji matokeo ya Urais baada ya kutangazwa

Nakala: Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
 
Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,837
2,000
Kwanza hakuna haja ya kufanya uchaguzi ambao matokeo yake yanajulika kuwa waliopo madarakani ndio wenye maamuzi ya nani ashinde. Sasa kama wameweza kulazimisha mpaka wabunge wa cdm unategemea nini?
 
G4N

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
843
1,000
Wajitangaze tu mkuu, hakuna haja ya uchaguzi kwa tume iliyopo.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,999
2,000
Hivi kuna chama makini kweli kitashiriki uchaguzi wowote nchii hii baada ya uchafuzi uliofanyika 2020.
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
14,403
2,000
Ushauri kwa Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025:

1. IGP Simon Sirro aendelee kuimarisha jeshi la polisi na kuhakikisha anaendelea kutetea Chama Cha Mapinduzi,

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iendelee na utaratibu wa kukata majina ya wagombea wa vyama vya upinzani kwa kukosa sifa ya kusoma na kuandika,

3. Watendaji wote wa vijiji na kata waitwe ikulu na kupewa maagizo maalum ya kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda uchaguzi,

4. Jaji Mtungi aanze mchakato wa haraka wa kukifuta Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kabla ya uchaguzi wa mwaka 2024/2025,

5. Mahakama zihakikishe kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anakaa jela hadi kufika mwaka 2026,

6. Tume ya Taifa ya iteue TBC kuwa Chombo pekee cha kurusha matangazo ya matokeo yote ya uchaguzi wa rais. Iwe marufuku kwa chombo kingine chochote kutangaza matokeo,

7. Serikali ifungie mitandao yote ya kijamii wakati wa uchaguzi na iwe marufuku kubandika matokeo ya uchaguzi nje ya vituo vya kupigia kura,

8. Wasimamizi wa uchaguzi ihakikishe kwamba hakuna wakala yoyote wa Chama cha upinzani anatoka na nakala ya matokeo kwenye chumba cha kupigia kura.

9. Wasimamizi wa uchaguzi wahakikishe kwamba mawakala wote wa vyama vya upinzani wanaingia kwenye vyumba vya kupigia kura saa 6 mchana siku ya kupiga kura,

10. Tume ya taifa itangaze mgombea wa Chama cha Mapinduzi kimeshinda kwa kuwa kwa mujibu wa katiba ya JMT hakuna mahakama yoyote inapaswa kuhoji matokeo ya Urais baada ya kutangazwa

Nakala: Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi
in short unapendeza nchi itoke kwenye democracy iende kwenye communism? wel nina habari mbaya kwako.. its doesnt work enzi hiz.. mama hatohangaika kusoma uchafu
 
Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
9,488

Umeshindwa kumuelewa kweli? Ameisanifu ccm hapo na alies wake Kama @tanpol na nec
 
Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
9,488
2,000
Chedema wasishiriki kwenye huu ujinga kabisa bila katiba na tume huru
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom