Ushauri kwa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB)

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kwanza nitoe shukrani zangu za dhati kwa Bodi hii ya usajili ya Wakandarasi. Wanafanya kazi nzuri sana ya kuwasimamia Wakandarasi wote nchini katika masuala ya elimu, semina mbalimbali ili kuwapa wakandarasi uelewa katika sekta ya ujenzi.

Wakandarasi wamepangwa katika madaraja mbalimbali kuanzia daraja la 1-7 na uwezo/thamani ya kazi kwa kila daraja ambayo kila daraja kwa mujibu wa sheria anatakiwa kutekeleza.

Thamani ya kazi kwa madaraja haya yalipangwa muda mrefu na hivyo kutokana na maendleo,mabadiliko ya bei ya vifaa vya ujezi na kushuka kwa thamani ya fedha inatakiwa sasa thamani ya kazi inayotakiwa kutekelezwa kwa kila daraja ufikiriwe upya.

Nitoe mfano wa kandarasi la daraja la 7. Thamani ya utekelezaji wa kazi yake si zaidi ya Tshs 200m. Kwa sasa thamani hii inashauriwa iongezwe na kufikia angalau Tshs.300m ukichukulia kuwa mabadiliko makubwa ya bei ya vifaa, kushuka kwa thamani ya fedha yetu.

Kwa hitimisho ninaiomba CRB ipitie thamani ya kazi inayotakiwa kutekelezwa na kila daraja na iweze kuja na suluhisho kwa faida ya Wakandarasi wote.
 
Back
Top Bottom