Ushauri Kwa BAVICHA na CHADEMA; Someni Historia ya Nchi hii, mnajidhalilisha kwa wenye akili

Chadema wameshikwa pabaya sana mwakauu, nakumbuka Sabaya alipokamatwa tu walikunywa bia na kuchoma ile nyama yetu kwa fujo, leo kibano kimekuja kwao kinakuwa cha uchungu.
Kwani chadema hawana imani na mahakama kuwa itatenda haki kwa Mbowe, tulieni mahakama ifanye kazi yake.
Kuanzia majuzi nasika ohoo eti serikali itapata aibu hivyo wafute hii kesi, kweli!! Yaani leo Bavicha wanaofia serikali ya CCM kupata aibu basi ni ajabu
Ingekuwa inatenda haki mahabusu wasingejaa
 
Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla

Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama

Napenda kuwashauri hivi;

Embu jitahidini kusoma na kujua angalau kidogo historia ya nchi hii na nadhani itawasaidia kidogo

Wanajeshi wa kesi ya Mbowe si watu wa kwanza nchini kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama vya Tanzania baada ya kufanya Jinai.

Mwaka 1981, Wanajeshi kadhaa akiwemo Komando Tamimu, Kapteni Kadego,Kapteni Maganga, Luteni Zacharia Hanspope, Kapteni Maghee na wenzako walifanya mpango wa kutaka kuiangusha Serikali ya Awamu ya kwanza.

Kwenye mipango iyo Walishirikiana na Wanajeshi wenzao akiwemo Luteni Ndejembi( Ambaye alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma- Ni baba Mzazi wa Naibu Waziri Ndejembi, Mbunge wa Chamwino)

Wakati wanapanga mipango yao Ndejembi na wenzake waliwaripoti kwa Mkuu wa Usalama Jeshini . Enzi izo alikuwa Luteni Kanali Davis Mwamunyange ( Ambaye Kwa sasa ni CDF Mstaafu )

Baada ya mipango iyo kusanuliwa Vikosi vya ulinzi na Usalama ( JWTZ, TISS na Polisi) walifanya operesheni maalumu iliyowezesha wanajeshi hao wote kukamatwa na kuuwawa kwa Komando Tamimu ambaye aliuliwa akijaribu kutoroka. Wanajeshi hawa ukisoma kesi hii walipitia msoto wa uhakika ikiwemo torture ili kupata kiundani mipango yao

Kesi ilienda Mahakamani na watuhumiwa wote walihukumiwa vifungo gerezani! Kesi iyo iliendeshwa na Wakili wa Serikali matata aliyejulikana kama Sekule ambaye alikuwa DPP na baadae akaja kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kwa maelezo haya napenda leo kuwahusia Bavicha na Chadema, acheni kuanzisha vi thread vyenu uchwara ambayo vinaonesha hamjui historia ya hii nchi. Kama mnadhani mnaleta uchonganishi basi jueni mnakosea sana. Vyombo vya dola vya Tanzania vinafanya kazi kwa utaratibu maalum na ndo mana nchi iko salama miaka yote hii tangu Uhuru

Poleni sana Bavicha na Chadema!

Mbowe haponi!

Kumbe ulikuwa umesema haya:

"Wanajeshi hawa ukisoma kesi hii walipitia msoto wa uhakika ikiwemo torture ili kupata kiundani mipango yao"

Si ungejitolea mkuu kutoa ushahidi upande wa utetezi kuwa washitakiwa kwa standard za polisi wetu, watakuwa wamepitia msoto wa uhakika ikiwamo torture?

Kumbe wewe hujui kuwa upande wa mashtaka unakanusha hilo kata kata?

Unajua jaji anauhitaji ukweli wa nini haswa kilijiri ambao ndiyo ulio msingi wa pingamizi lililopo mikononi mwake sasa hivi?

😂😂😂!!

Hiiiiii bagosha.
 
Kama unakubali kuigwa ya Guantanamo kwa nini unapinga ushoga?
Torture haiigwi ni human nature, before mzungu afike Africa torture ilikuwepo kwenye chiefdoms, jiulize kwanini Shaka Zulu alikimbiwa uje na majibu…huo ushoga wenu its against nature. …
 
Nyie mnaonufaika na utawala dhalimu lazima muutetee tu bila kujali watu wanateseka na kufa ili mradi matumbo yenu yajae.

Hawa Vijana wanaoshabikia ccm wanasumbua sana mtaani kutwa kuomba vihela, kazi hawafanyi kutwa kuvaa Minguo ya kijani na kuwapamba wabunge wao na madiwani....Ohhhhh sijui wateleta maji, ooohhh mara barabara kwani kusingekuwepo ccm barabara maji na n.k visingekuwepo? Kwan hela za maendeleo wanatoa mifukoni mwao?
vijana fanyeni kazi achaneni na kijani kutwa kushinda kwenye viofisi vya kijani na njano.....shikeni jembe mkalime....mnatuangusha sana.
 
Mambo yao waachie wenyewe...

Wanauhuru wa kuongea, kutoa maoni au kuonesha misimamo Yao...
 
Ujumbe gani sasa uliotoa hapo au unahisi nani halifahamu hilo swala la kina Hanspope?? Na je Hio inshu ya kina Hanspope na ya Mbowe vina relation mkuu?? Au na wewe ulisimuliwa halaf umekuja na ki-thread ukoko chako hapa.

Hivi huyu mwamba amebadili gia lini maana kumbukumbu zangu za kipindi cha uchaguzi mwaka jana yeye ndo alikuwa anajaza threads hapa kumponda Magu na kumtetea Lissu? Huyu jamaa kama sio Kigogo mwenyewe sijuhi!!Sio kwa hii U-turn.
 
Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla

Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama

Napenda kuwashauri hivi;

Embu jitahidini kusoma na kujua angalau kidogo historia ya nchi hii na nadhani itawasaidia kidogo

Wanajeshi wa kesi ya Mbowe si watu wa kwanza nchini kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama vya Tanzania baada ya kufanya Jinai.

Mwaka 1981, Wanajeshi kadhaa akiwemo Komando Tamimu, Kapteni Kadego,Kapteni Maganga, Luteni Zacharia Hanspope, Kapteni Maghee na wenzako walifanya mpango wa kutaka kuiangusha Serikali ya Awamu ya kwanza.

Kwenye mipango iyo Walishirikiana na Wanajeshi wenzao akiwemo Luteni Ndejembi( Ambaye alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma- Ni baba Mzazi wa Naibu Waziri Ndejembi, Mbunge wa Chamwino)

Wakati wanapanga mipango yao Ndejembi na wenzake waliwaripoti kwa Mkuu wa Usalama Jeshini . Enzi izo alikuwa Luteni Kanali Davis Mwamunyange ( Ambaye Kwa sasa ni CDF Mstaafu )

Baada ya mipango iyo kusanuliwa Vikosi vya ulinzi na Usalama ( JWTZ, TISS na Polisi) walifanya operesheni maalumu iliyowezesha wanajeshi hao wote kukamatwa na kuuwawa kwa Komando Tamimu ambaye aliuliwa akijaribu kutoroka. Wanajeshi hawa ukisoma kesi hii walipitia msoto wa uhakika ikiwemo torture ili kupata kiundani mipango yao

Kesi ilienda Mahakamani na watuhumiwa wote walihukumiwa vifungo gerezani! Kesi iyo iliendeshwa na Wakili wa Serikali matata aliyejulikana kama Sekule ambaye alikuwa DPP na baadae akaja kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kwa maelezo haya napenda leo kuwahusia Bavicha na Chadema, acheni kuanzisha vi thread vyenu uchwara ambayo vinaonesha hamjui historia ya hii nchi. Kama mnadhani mnaleta uchonganishi basi jueni mnakosea sana. Vyombo vya dola vya Tanzania vinafanya kazi kwa utaratibu maalum na ndo mana nchi iko salama miaka yote hii tangu Uhuru

Poleni sana Bavicha na Chadema!

Mbowe haponi!
Mbowe haponi hata kura yangu haikupona mliikomba, wanaccm ndio raia daraja la kwanza nchi hii. Wewe ungejua historia ya nchi hii ungejua mwingereza hakuwaua wala kuwafunga waliopigania uhuru, aliondoka bila kuacha kesi yoyote ya ugaidi.
Mwisho, BAVICHA na CHADEMA wanahusikaje kwenye kesi zaidi ya wewe kujionesha ni mpenda kubambikia watu kesi. Hilo la Mbowe si gaidi ni la wapenda haki wote kasoro wewe mwanaccm na baadhi ya wanaccm. Ujue leo Jumamosi wapo wanaccm watakaomtembelea Mbowe jela kwa kuwa wanaamini hakuna ugaidi wa shilingi laki sita na kununuliana nyama choma.
 
Mtoa mada tupo kwenye utawala wa sheria na si zama za dictator nyelele.hao kina kingai na mahita baada ya kesi kumalizia lazima tuwatafute wakiwa hai au wamefariki ili walipe gharama za matendo yao.haiwezekani wanajeshi wateswe Kisha watesaji waendelee kunywa mvinyo kwenye sturi ndefu,watesaji wataishi maisha mithili ya digdigi.
 
Habarini Bavicha na Chadema kwa Ujumla

Leo napenda kuwashauri jambo la kuwasaidia kutokana na trend yenu ya kuanzisha vi thread humu kuongelea kesi ya Mbowe na kuleta nadharia zenu kuhusu watu waliokuwa Wanajeshi ambao wamedhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama

Napenda kuwashauri hivi;

Embu jitahidini kusoma na kujua angalau kidogo historia ya nchi hii na nadhani itawasaidia kidogo

Wanajeshi wa kesi ya Mbowe si watu wa kwanza nchini kudhibitiwa na vyombo vya ulinzi na Usalama vya Tanzania baada ya kufanya Jinai.

Mwaka 1981, Wanajeshi kadhaa akiwemo Komando Tamimu, Kapteni Kadego,Kapteni Maganga, Luteni Zacharia Hanspope, Kapteni Maghee na wenzako walifanya mpango wa kutaka kuiangusha Serikali ya Awamu ya kwanza.

Kwenye mipango iyo Walishirikiana na Wanajeshi wenzao akiwemo Luteni Ndejembi( Ambaye alikuja kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma- Ni baba Mzazi wa Naibu Waziri Ndejembi, Mbunge wa Chamwino)

Wakati wanapanga mipango yao Ndejembi na wenzake waliwaripoti kwa Mkuu wa Usalama Jeshini . Enzi izo alikuwa Luteni Kanali Davis Mwamunyange ( Ambaye Kwa sasa ni CDF Mstaafu )

Baada ya mipango iyo kusanuliwa Vikosi vya ulinzi na Usalama ( JWTZ, TISS na Polisi) walifanya operesheni maalumu iliyowezesha wanajeshi hao wote kukamatwa na kuuwawa kwa Komando Tamimu ambaye aliuliwa akijaribu kutoroka. Wanajeshi hawa ukisoma kesi hii walipitia msoto wa uhakika ikiwemo torture ili kupata kiundani mipango yao

Kesi ilienda Mahakamani na watuhumiwa wote walihukumiwa vifungo gerezani! Kesi iyo iliendeshwa na Wakili wa Serikali matata aliyejulikana kama Sekule ambaye alikuwa DPP na baadae akaja kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Kwa maelezo haya napenda leo kuwahusia Bavicha na Chadema, acheni kuanzisha vi thread vyenu uchwara ambayo vinaonesha hamjui historia ya hii nchi. Kama mnadhani mnaleta uchonganishi basi jueni mnakosea sana. Vyombo vya dola vya Tanzania vinafanya kazi kwa utaratibu maalum na ndo mana nchi iko salama miaka yote hii tangu Uhuru

Poleni sana Bavicha na Chadema!

Mbowe haponi!

Kwamba Mbowe haponi?

Kama kupata Maelezo ya Adamoo, sheria ilikiukwa, Yatatupwa

Habari ndiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom