Ushauri kwa Baraza la Mitihani NECTA:-Semina elekezi kwa wataalamu wa Maabara iendane na ufuatiliaji wa ubora wa maabara zilizopo mashuleni

RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,294
2,000
Hongereni kwa kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha gurudumu la elimu ya nchi yetu linasonga Daima na kuleta tija kwenye ueledi wa fani mbali mbali.

Nimepata taarifa ya semina elekezi kwa wataalamu wa maabara inaendelea hadi sasa!Niwaombe msiishie tu kwenye semina pekee bali muandae tume ya sayansi ya kufuatilia ubora wa hizo maabara zilizopo mashuleni kama zinakidhi viwango na vigezo vya vitendo halisi vya kisayansi kufanyika

Hii itasaidia nyie kutambua mapungufu yaliyomo na kutoa maelekezo kwa serikali kutatua changamoto zitakazo jitokeza

Kuna baadhi ya shule hazina maabara kabisa,nyingine zina maabara moja tena ambazo ni kuukuu,tena bubu kabisa na hazikidhi viwango vya semina elekezi mnazotoa.

Nyingine hazina hata umeme wa solar hivyo ni vigumu kwa waalamu kufanya vitendo vya kisayansi ipasavyo.

Naamini NECTA ni taasisi pekee inayoaminika na sikivu itafanyia kazi mapendekezo hayo kutoka kwa wadau wa sayansi na elimu nchini!!
 

RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,294
2,000
Ndio kuna shule baadhi vigezo vya maabara havikidhi viwango ni jukumu lenu kutoa taarifa kwa mamlaka husika!changamoto zifanyiwe kazi!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom