Ushauri kwa Balozi Mulamula: Mkitaka Tanzania ifaidike na Diaspora suala la uraia pacha haliepukiki

Kwa vipi uamue kuwa na double face?
Kwa nini usichague nchi moja tu na kuchukua uraia wake??
Jambo lipi linakuzuia kuchagua sehemu moja ya kuishi mpaka ulazimike kuishi na pasi mbili za kusafiria? Unajaribu kuficha au kupata nini cha ziada??
Kwenye makala umesema wengi wa wanaopinga uraia pacha hawajahi kuishi nie ya nchi. Hili nalo siyo kweli na hata kama lina ukweli bado halizuii kuibuka kwa maswali yanayohoji motive ya kutaka uraia pacha!!
Kama ni diaspora kuchangia nchini kwao mbona watahudi wanaweza bila kuwa na uraia pacha???
Tuache propaganda uchwara za kusingizia diaspora wakipata uraia pacha wataweza kuisaidia nchi hilo halina ukweli!
Eeee ndugu wacha kusema maneno bila kuwa na uhakika na unachokisema, utasemaje kuwa wayahudi hawana uraia pacha ilhali inajulikana fika kuwa wapo tele hususan matajiri wakubwa wa kiyahudi waishio nchi kama france, uk na usa wana uraia pacha? Israel inawafurahia kabisa kabisa wananchi wao kuwa na uraia pacha na wako kirahisi kuwapa uraia wale mayahudi ambao wamezaliwa nje ya nchi na ambao wanataka uraia wa kiyahudi. Kama utakumbuka hivi karibuni israeli wamempa uraia yule tajiri anaemiliki chelsea kirahisi kabisa, ili kumwezesha kuingia na kutoka katika nchi za europe na pia kuweza kuinvest nchini isarael.

Ama hayo masuali yako ya mwanzo, sina haja ya kukujibu, ila tu ikiwa hamtaki kutowa uraia wa pacha sawa, lakini wacheni kukaa kila siku kutowa wito kwa walio nje waje kusaidia Tanzania. Wao wameshatoa sharti lao ni kuwa muwaruhusu kuwa na uraia pacha, kama hamtaki basi! Wao wataendelea kuwasaidia familia zao nyumbani na nyie endeleeni kuwaruhusu wachina na wageni wengine kuja tanzania kuekeza na kuwanyanyasa ndugu zetu!
 
Na una ushahidi machafuko yametokea kwa sababu ya uraia pacha, huko Uganda, Rwanda, Kenya, Botswana, Angola, Ghana, nk, kwenye uraia pacha?
The way back Tanzania used to be tested and steadily withheld the turbulence, this time around the nest will be swept and torn into pieces disintegrating in the wilderness helplessly........
 
Na una ushahidi machafuko yametokea kwa sababu ya uraia pacha, huko Uganda, Rwanda, Kenya, Botswana, Angola, Ghana, nk, kwenye uraia pacha?
Wasababishaji ndio hao na pakiharibika wanatimkia ughaibuni bila kukwazwa na masharti. Ushahidi umeotoa mwenyewe kwa njia ya ramani inyoonesha mataifa ambayo yameruhusu uraia pacha, yaliyoruhusu nusu-nusu kwa baadhi ya mambo na yale ambayo bado kabisa. Ukiyachambua kundi la kwanza huko ndiko machafuko yaliko na waanzilishi ama wanaishi ughaibuni au kama kwenye nchi husika pakiharibika wanakwea pipa kwenda kujificha nje ya nchi.
 
Una theory za ajabu sana.
 
Tuache propaganda uchwara za kusingizia diaspora wakipata uraia pacha wataweza kuisaidia nchi hilo halina ukweli!
Na aliekuambia uraia pacha ni kwa ajili ya Diaspora rudi ukamwambie akufundishe zaidi maana ya uraia pacha. Utakapoelewa njoo uchangie hii thread
 
Na huo muswada utakapopelekwa BUngeni, wabunge wa CCM ndio wapiga kura. Sasa Wabunge wa CCM wanajua hawana ruhusa kupinga muswada wa serikali. Wanajua hawakushinda ubunge bali walifanywa kuwa wabunge ili kuja Bungeni kupitisha mambo ya serikali.
👍
Hapo umenena vyema mkuu
 
Kwa mwendo wa dunia ya sasa nadhani ni wakati sahihi sasa wa serikali yetu kuruhusu mwananchi kuwa na uraia wa nchi nyingine zaidi kutegemeana na unasaba alionao mhusika

Jambo hili litasaidia wengi ambao wapo kimya na kwa namna moja au nyingine kulisaidia taifa katika nyanja tofauti kimaendeleo..za uchumi,sanaa michezo na utamaduni,likifanyika hili litaleta muingiliano wenye tija kwa taifa.

Kwa namna ya pekee tuombe muhimili wa bunge muanzishe hoja hii muhimu bungeni,kwani ni wengi tulio ndani ya nchi na wengi wapo nje ya nchi wanalitamani jambo hili nyeti na kulisubiri,wengine wamethubutu na wameweza sisi ni nani tushindwe?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom