Ushauri: Kuwe na mbadala wa kufunga line za ziada kwa kupiga *106#

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,028
Naona mwamko umekuwa mdogo kwa watu kwenda kufunga line za ziada katika ofisi za mitandao, sio kwamba hatuwezi kwenda ila mambo yametinga jamani maana awamu hii ni kazi kazi kitu kinachonyima wengi muda wa kwenda hizo ofisi.

Ningependa kuwasilisha maoni yangu kwamba tunavyopiga *106# kuwe na option ya kufunga laini za ziada ili kuwekeana uwepesi katika zoezi hili la kumiliki laini moja kwa kila mtandao.

Ni kitu ambacho kinawezekana kabisa hivyo kianze kutekelezwa ili kuwe na wepesi na kuondoa kero za kwenda huko maofisini

Nawasilisha
 
Kweli kabisa mkuu,
Mimi kuna mtu anatumia line iliyosajiriwa kwa kitambulisho changu.
Nimepiga simu Airtel huduma kwa wateja wasitishe huduma katika namba hiyo majibu yao wananitaka niende ofisini kwao vinginevyo hawawezi kusitisha huduma.
Nimewaambia nipo mbali zaidi ya 150km na mambo ni mengi bado wameniambia nifike Ofisini kwao.
Waliangalie hili si kila muda nina muda wa kufika Ofisini kwao.
 
Halafu mtu akikuuz unamvizia unachukua simu yake unamfungia line.C unajua binadamu tunavyojua kutumia fursa tena.Labda kama hilo zoez litahusisha na utumiaji wa nywila za huduma za pesa mtandao
 
Back
Top Bottom