Ushauri kusaidia uwekezaji Magufuli ajiri mfanyabiashara kwenye wizara hii

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Kwenye wizara wa biashara na hata viwanda nashauri Magufuli aajiri mfanyabiashara kupunguza uoga ambao upo kwa uwekezaji. Unahitaji mtu ambaye anaelewa uoga huo na mwenye credibility ya kuzungumza na mwekezaji. Ni ngumu mwekezaji kumwamini mwanasiasa ambaye hana uzoefu wowote ule na ni ngumu kwa mwanasiasa tu wa kawaidia kuaminika.

Uwekezaji wa ndege na treni itachukua miaka 5-10 kuanza kuingiza faida na hasara ina maana kwamba tutahitaji kodi zaidi. Sasa tujiulize kodi itatoka wapi kama uwekezaji ndiyo hivi. Tatizo la Tanzania pamoja na mambo kwenye uwekezaji ni uoga wa serikali kubadilisha sheria katijkati ya uwekezaji au kuingia kwenye ushindani na makampuni ya serikali au wanasiasa kuingilia uwekezaji kwa sifa tu bila kufuata sheria. Wawekezaji wanataka kiongozi ambaye watamuamini.

Lakini vilevile serikali ijitahidi iwe na sheria ambazo hazibadiliki kila mwaka ili wawekezaji waweze kukopa na kuwa na estimates nzuri za mapato
 
..Magufuli alikosea kumfukuza kazi Mh.Mwijage.

..na kosa la Mwijage lilikuwa kuchelewa kutekeleza maagizi ya vitisho ya kutaifisha viwanda vilivyokuwa vimebinafsishwa.
 
Sector hiyo ilimfaa mtu kama mengi(RIP) ila kwa Sasa wangempa mtu kama a. Mufruki yatosha

Ova
 
..Magufuli alikosea kumfukuza kazi Mh.Mwijage.

..na kosa la Mwijage lilikuwa kuchelewa kutekeleza maagizi ya vitisho ya kutaifisha viwanda vilivyokuwa vimebinafsishwa.
Mh. Mwijage alimasta Sana ile wizara. Yani alikuwa anaipeleka Kama inavyotakiwa.

Tatizo ilikuwa ni yale "mabibo"...seems tapping ilianza zamani.
 
Nyie mnataka kumtoa kwenye reli ngojeni kwanza atoe ubatizo wa moto kwa makamba na wenzake ndiyo tuje huko kama bushingwa kashindwa
 
Back
Top Bottom