SoC01 Ushauri: Kupunguza miaka ambayo Wanafunzi hutumia katika masomo ili kukuza Uchumi

Stories of Change - 2021 Competition

Maxing maxed

Member
May 6, 2021
6
12
Kutokana na mabadiliko ya kitekinolojia na mabadiliko ya jamii kiujumla nilazima kuwepo na namna ya kubadili mfumo mzima wa elimu hasa katika kupunguza idadi ya miaka ambayo wanafunzi hutumia katika masomo.

Kwa mwanafunzi kufikia chuo kikuu mwaka wa tatu itakuwa imemchukua zaidi ya miaka 15 akiwa masomoni. Na kutokana na kutokuwepo kwa uhakika wa kuajiriwa basi itampasa mtu huyo kuanza kutafuta namna ya kujiajiri ambapo pengine itamchukua tena miaka kadhaa ambapo ndio ataanza kufanya vizuri kiuchumi na ndipo hapo atakapoanza kuifaidisha jamii na serikali kiujumla.

Sasa ingekuwa vizuri mtu huyu apunguziwe miaka anayoitumia katika masomo yake na kisha kujikita katika kujenga uchumi binafsi huku akikuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Jamii ya Watanzania inaamini mtoto mwadilifu ni yule anayefata njia sahihi za masomo. Yaani jamii inamtaka mtoto aanze kwa kusoma mpaka darasa la saba, kisha afaulu kwenda kidato cha kwanza ambapo atasoma hadi kidato cha nne, kisha aende kidato cha tano mpaka cha sita, na kisha aende chuo kikuu... kwa kufuata njia nyoofu kama hiyo basi jamii huamini mtoto huyo yuko katika njia sahihi.

Kutokana na hilo ingependeza ikiwa miaka ya masomo ingepunguzwa ili kuwezesha wengi kufikia matazamio hayo ya Wanajamii.

Kwa kupunguza miaka ya masomo kwa wanafunzi; serikali itafaidika kwa kukua kwa uchumi wa nchi uliotokana na ongezeko la nguvukazi katika jamii, pia jamii itafaidika kwa matunda yatokanayo na vijana wao kufanya kazi za kiuchumi na pia wazazi watasomesha watoto wao kwa muda mfupi kiasi kwamba hawataumia sana kiuchumi na watoto wao wengi watapita njia iliyosahihi.

Bila kusahau wanafunzi pia watafaidika kwasababu watapata muda mwingi wa kujipanga kiuchumi kwasababu hawatabanwa na masomo.

kura yako ndugu 😋
 
kura yako ndugu
Mpaka kufika chuo inamchukua miaka 18 yaan kutoka awali mpaka la saba miaka nane jumlisha miaka 6 ya advancebna orlevel unapata miaka 14 jumlisha miaka mitatu ya chuo jumla miaka 17 na mwaka mmoja wa kusota miaka 18
 
Back
Top Bottom