Ushauri: Kupunguza ajali, Ijengwe barabara nyingine mkabala na iliyopo

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Juzi kwa mara ingine tumepoteza roho za ndugu zetu zaidi ya ishirini hapo Morogoro kwa ajali mbaya iliyohusisha basi la abiria na Lori.

Ukiangalia kwa kina hapa unakuta pamoja na mambo mengine mengi,ufinyu wa barabara nalo ni tatizo...serikali itupie macho eneo hili.

Tufikirie tu barabara yenye kilometa zaidi ya alfu moja.. inayotumiwa na magari zaidi ya alfu moja kwa siku..lets say kutoka Mwanza to Dar....Tunduma to Dar....Namanga to Dar..nk

Bara bara hii gari zipishane kwa kupeana gape la mita mbili tu tena zote zikiwa high speed ni hatari tosha!

Pongezi kwa serkali kwa kutanua barabara kutokea kimara mwisho hadi Kibaha maili moja..hapa si tu wameondoa folenizisizo lazima lakini pia wameondoa kabisa ajali hasa zile za uso kwa uso..!

Ushauri sasa kwa Tanroad..kwa kuepuka gharama za ujenzi na upembuzi yakinifu...kuanzia kibaha maili moja sasa paanze kujengwa barabara nyingine iende sambamba na hii iliyopo kuelekea Mlandizi, Chalinze, Morogoro ili sasa gari zinazokwenda bara ziwe na upande wake wa kushoto na za kutoka bara kuja mikoa ya Pwani ziwe na upande wake wa kulia,hili litasaidia sana kupunguza ajali na vifo.

Bajeti ifuatayo zoezi hili liendelee kutoka Morogoro hadi Dodoma na pia Morogoro to mikumi then ilula to Tunduma. Hivyo hivyo baadae nchi nzima kuwe na bara bara hizi yaani mbili kwa nne.nina hakika hii itasaidia na ndio mataifa mengi makubwa duniani baadhi yao ni kama UAE,Japan,Us,Malaysia nk wapo miaka mingi kwenye utaratibu huu.

Nawasilisha
0716399767.
 
Wako bize kusaini mikataba na maadishi ya matirioni ya pesa..ila kinachoonekana mpaka sasa ni maneno na propaganda zisizo na tija.

Kwaufinyu wa akili huwa wanaamini ajali husababishwa na uzembe wa dereva nakisahau kabisa kuwa miundombinu isiyo kidhi mahitaji nayo ni tatizo kubwa.

Walichobakiza sasa ni kuendeleza iliyoanzishwa na JPM na propaganda za kulaghai watanganyika.

#MaendeleoHayanaChama
 
Huo ni ukweli usiopingika. Kwa wale wanaoishi nje ya Tanzania watayakinisha kuwa kweli Tanzania "highway" zetu ni nyembamba sana na ni tatizo kuwa hivyo tika dunia ya kisasa ya haraka haraka.

Ni wakati muafaka, barabra kuu zote za kuunganisha mikoa ziwe gari hazipishani ziwe, japo kwa uchace, ni four way lanes kwa kuanzia, mbili za kwenda mbili za kurudi na kati kati yao hazikutani. Wenzetu duniani huko, sasa hivi highways zinakua kwa uchache ni "8 lanes", nne za kwenda na nne za kurudi na hakuna barabara inayozikatiza, hutumika "change overs".

Ni vyema kabisa tukaanza na Morogoro Road, Dar-Morogoro". Hatuna ujanja wa kupunguza ajali bila kufanya hivyo. Ingawa na nazo hazitazuia kabisa (100%) ajali lakini zitapunguza sana na itabaki ku deal na matatizo mengine ya barabarani kama vile ya ulevi kwa madereva na udereva usio udereva.
 
Mimi naogopa hata kusafiri,mpaka inapobidi. Misiba ya ndugu wa mbali piga chini.

Unaposafiri iwe kwa private au public transport ni kama unakabidhi uhai mapokezi kisha unaingia ndani ukifanikiwa kutoka unapewa uhai wako unaondoka zako.

Kuna kosa kosa kibao ambazo haziwagi ajali. Mnashukuru Mungu. Mpaka lini?
 
Mimi naogopa hata kusafiri,mpaka inapobidi. Misiba ya ndugu wa mbali piga chini.

Unaposafiri iwe kwa private au public transport ni kama unakabidhi uhai mapokezi kisha unaingia ndani ukifanikiwa kutoka unapewa uhai wako unaondoka zako.

Kuna kosa kosa kibao ambazo haziwagi ajali. Mnashukuru Mungu. Mpaka lini?
Kweli ni hatari.
 
Back
Top Bottom