Ushauri kuhusu usalama barabarani

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,381
Njia nzima siku hizi za mijini na zile za barabara kuu wamejaa askari wa usalama barabarani. Serikali inatumia pesa nyingi kuwalipa hawa ili waongoze magari lakini pia wakamate vyombo vibovu.

Ushauri wangu ni kwamba kuwe na control center na traffic wawe kwenye exit point. Ile control center inakuwa na screens zinazoonyesha picha ya jiji zima na barabara kuu zinazotoka kwenye camera zilizofungwa barabarani. Kisha wahalifu na wavunja sheria wakamatwe kupitia hivyo.

Kuhusu taa za kuongozea magari hizi zinatakiwa ziwe centrally controlled kutoka kwenye hiyo center inayotazama jiji zima. Hii itaondoa askari kwenye mataa na kunusuru maisha yao.
 
Kweli kila mtu na mawazo yake. Nchi iliyoshindwa kuweka mashine ya X-Ray kila wilaya leo hii inashauriwa kuweka kamera barabarani, sijui kwa hela zipi....za majipu au hizi za pension tunazotaka kudhulumiwa tudhalilike?
 
Kwahiyo hakuna linalowezekana kwa sababu umedhulumiwa pension. Hii tunazungumza itaongeza pia mapato na kupunguza rushwa.
 
Kwahiyo hakuna linalowezekana kwa sababu umedhulumiwa pension. Hii tunazungumza itaongeza pia mapato na kupunguza rushwa.

Mnayozungumza wewe na nani bwana, sema unayozungumza. Mapato yataongezwa na camera? Hii ni stori ya ndoto yako. Barabara hazina lami wala taa, leo camera jiji zima. Kama wapi kwa mfano? Maana unazungumzia kamera kama tunaongelea mikungu ya ndizi kwamba tutaenda Marangu na Bukoba tukajaze mafuso tusambaze mitaani
 
Raha sana, wewe ukisema pesa mnayotaka kudhulumiwa mlikuwa wangapi? Ni wewe peke yako! Sipendi ujinga wa kuhangaika na grammar badala ya point. Kuna huu mradi wa DART umeanza na miradi mingine kibao. Ukifuatilia mataifa mengi yenye mifumo ya camera barabarani yamepunguza ajali lakini pia mapato kutokana na faini za barabarani na utunzaji barabara umeimarika.
 
Wazo zuri ila unadhani linaendana na barabara zetu?

Unadhani liwe kipaumbele cha kwanza????

Unadhani wataweza kuzihudumia hizo kamera?

Unadhani tuna umeme wa uhakika???
 
Back
Top Bottom