yutong
JF-Expert Member
- Apr 15, 2011
- 1,601
- 338
Binafsi nimevutiwa sana na gari ya aina ya BMW 3 Series (318i) na Subaru Impreza. Lakini kabla sijafikia uamuzi ni gari gani ninunue kati ya hayo mawili ningeomba ushauri wenu wana-JF hapa jamvini na mnipe sababu za kiufundi kuhusu magari yote hayo mawili kila moja hasara na faida zake. Ningependa sana kuangazia hasa katika gharama za uendeshaji wa magari haya mawaili yahani subaru na BMW. Pia ingaliwe katika upatikanaji (availability) wa spear parts (bei si tatizo) na pia upatikanaji wa mafundi wa kurepair, kutengeneza na kufanyia service ya aina hiyo ya magari na ni wapi wanapatikana. Kwa kifupi kuhusu ulaji wa mafuta bi hivi: BMW ni 1890cc pia ni 5AT&MT mode (ulaji wa mafuta ni kilometa 9.8 kwa lita), na Subaru Impreza ni 1500cc. Naombeni ushauri wenu na ni-taapriciate kwa ushauri wenu. Naomba kila anayetoa ushauri ani-tag ili niweze kupata ujumbe kwa urahisi.