Ushauri kuhusu chanzo kipya cha kodi kuwapunguzia mzigo wafanyakazi

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Mtakumbuka kwamba tangu serikali iondoe kodi ya kichwa miaka ya mwanzo ya utawala wa Mkapa ilibidi hiyo deficit kwa kiasi kikubwa ifidiwe na mishahara ya wafanyakazi. Ilibidi wafanyakaxi wabebe mzigo wa kodi ile ya kichwa.

Najua kodi ya Ongezeko la thamani VAT ilianzishwa ili kila mtu alipe kodi indirectly kupitia ununuzi wa bidhaa lakiki hili eneo bado halijawa na ufanisi sana kwani mfanyakazi huyuhuyu anajikuta analipa kodi ya VAT pia wsksti wskulima, wafanyabiashara ndogondogo yaani wachuuzi hawalipi kodi ya mapato wakati wanatengeneza pesa za kutosha tu.

Hata wafanyabisshara waliosajiliwa TRA nao wengi hawalipi kodi stahili kwa sabanu ya rusha na inefficiency ya TRA. Matokeo yake upungufu huu wa TRA anabebeshwa mfanyikazi.

Ndio maana nashauri turudishe ule utaratibu wa kila mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na mwenye afya njema (ukiacha wazee wenye miaka 70 and above na wanafunzi) alipe kodi awe na kazi au la.

Mfano tunaweza kuanza na 10000 tu kwa mwaka. Tukipata watanzania mil 20 waliokuwa hawalipi kodi ya mapato na kuanza kulipa tutakuwa tumetengeneza 200.000.000.000. Tumia kiasi fulani kwenye hii pesa kupunguza asilimia 10, kwenye zile asilimia 30 na 25 n.k kwenye kodi za wafanya kazi.

Wakati huo TRA wahakikishe wanakusanya kodi stahili toka kws wafanya biashara wote. TRA wakiendekea kuwa inefficient, ibinafshishwe! Ndioo!! tuwape kazi wenye uwezo watusaidie kuweks mifumo ya kisasa ya ukusanyaji kodi!
 
Wazo zuri
Lakini lazima iangaliwe pros na cons zake,je ni Watanzania asilimia ngapi hyo buku 10 wanaweza ipata,maana kiukweli kuna sehemu especialy vijijini elfu 10 ni ishu, labda msimu wa mavuno.
 
Back
Top Bottom